Watangazaji wa TV/Radio wasiwe wnaapotosha watoto

maiyanga1

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
1,317
1,790
Niko na watoto wanaangalia AZAM TV UTv kipindi cha watoto. Mtangazaji anauliza mlima Kilimanjaro uko mkoa gani? Anawaambia wachague jibu kati ya Tanga, Moshi na Arusha. Watoto wangu wakahamaki kwamba hakuna mkoa wa Moshi.

Watoto wakaanza kujibu. Wakwanza akasema Moshi, Mtangazaji akasema umekosa, mwingine akajibu Tanga, akaambiwa amekosa, mwingine akasema Arusha akaambiwa amekosa, baadaye mmoja akajibu Kilimanjaro akaambiwa amepata wakati Kilimanjaro haikuepo katika majibu yake.

Mara nyingi kumekuwa na tatizo hili sio kwa vipindi vya watoto tu.
 
Ni kweli kunakuwa na upotoshaji vipindi vya watoto, kuna siku kipindi cha watoto TBC walifundisha herufi 's' inasomeka 'se' watoto wangu kuwauliza wanasema ni 'sa' mi mwenyewe najua ni 'sa'
 
Tatizo la watangazaji/waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali hapa nchini hawaja-specialize kwenye mambo yawanayofanya.

Mwandishi anatoka chuoni hana elimu ya siasa ila anafika kwenye chombo cha habari anaanza kuchambua siasa, hivyo hivyo kwenye mambo kama michezo, biashara, elimu kwa jamii.

Ndiyo maana wengi wamekuwa wapumbavu kwenye 'carrier' yao na wanaonekana kama hawajui kitu.
 
Niko na watoto wanaangalia AZAM TV UTv kipindi cha watoto. Mtangazaji anauliza mlima Kilimanjaro uko mkoa gani? Anawaambia wachague jibu kati ya Tanga, Moshi na Arusha. Watoto wangu wakahamaki kwamba hakuna mkoa wa Moshi.
Watoto wakaanza kujibu. Wakwanza akasema Moshi, Mtangazaji akasema umekosa, mwingine akajibu Tanga, akaambiwa amekosa, mwingine akasema Arusha akaambiwa amekosa, baadaye mmoja akajibu Kilimanjaro akaambiwa amepata wakati Kilimanjaro haikuepo katika majibu yake.
Mara nyingi kumekuwa na tatizo hili sio kwa vipindi vya watoto tu.
Huenda lengo lake lilikuwa watoto waseme kati ya machaguo aliyoyatoa hakuna jibu sahihi. Hii inaruhusiwa
 
Tatizo la watangazaji/waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali hapa nchini hawaja-specialize kwenye mambo yawanayofanya.

Mwandishi anatoka chuoni hana elimu ya siasa ila anafika kwenye chombo cha habari anaanza kuchambua siasa, hivyo hivyo kwenye mambo kama michezo, biashara, elimu kwa jamii.

Ndiyo maana wengi wamekuwa wapumbavu kwenye 'carrier' yao na wanaonekana kama hawajui kitu.
Huko kwenye michezo ndio balaa kabisa. Wengi wanakosea kutamka majina ya timu na miji. Nilishangaa kumsikia Mtangazaji anasema Liverpool majogoo wa jiji la London. Pia wengi wanavyotamka jina Barcelona kwa ufupi. Wenyewe wanaita Barca wanaitamka "Basa" wakwetu unawasikia wanatamka Baka. Hata hawajihangaishi kusikiliza wenye majina yao wanatamkaje.
 
Kwenye utungaji wa maswali ya kuchagua hilo ni swali zuri kama miongoni mwa machaguo yangekuwa Moshi na Kilimanjaro. Upotoshaji binafsi sijauona.
 
Huko kwenye michezo ndio balaa kabisa. Wengi wanakosea kutamka majina ya timu na miji. Nilishangaa kumsikia Mtangazaji anasema Liverpool majogoo wa jiji la London. Pia wengi wanavyotamka jina Barcelona kwa ufupi. Wenyewe wanaita Barca wanaitamka "Basa" wakwetu unawasikia wanatamka Baka. Hata hawajihangaishi kusikiliza wenye majina yao wanatamkaje.
Kubaya sana huko kwenye media.
 
Back
Top Bottom