Watangazaji wa TV pandeni jukwaani kupigia kampeni CCM, tuachieni kazi yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watangazaji wa TV pandeni jukwaani kupigia kampeni CCM, tuachieni kazi yetu.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kasyabone tall, Aug 23, 2010.

 1. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Kitu kinachonikera kwa tv zetu zote hasa wa startv na TBC ni pale wanapoacha kazi yao na kujiingiza kupiga kampeni. Wanaeleza hisia juu ya chama fulani kuliko kufanya kazi ya kuripoti kile kinachotokea. Utasikia mtangazaji anatangaza chama cha CCM kimenitoa mbali, hii ni kauli ya ushabiki juu ya chama, Kitu amabacho kinaonyesha huyu mtangazaji hawezi kuripoti vizuri kwa chama cha upinzani kama Chadema ambacho hakija mtoa mbali. Lakini kinachochangia yote haya ni ukosefu wa elimu kwa watangazaji wetu. Nafikiri sasa ni wakati mzuri wa vyombo vya habari kutungiwa sheria juu ya kuripoti habari za uchaguzi, Kama sivyo vyama vya upinzani vitashindiwa kwenye vyombo vya habari.
   
 2. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Watafahamu baadaye kuwa hivyo si vizuri. Mwalimu wao mwenyewe kipofu
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  In short media zetu zilivamiwa muda tu, sasa untegemea nini!!

  Hawaelewi role yao kwa jamii hasa katika kipindi hiki....!!!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nawashangaa StarTV kufanya ushabiki huo, wakati wao ni purely for commercial broadcasting tv!..au wanadhani watakaowalipa vizuri ni ccm tu?...huwa nawaangalia siwamalizi!
   
Loading...