Watangazaji wa Redio hasa wasomaji wa magazeti pateni mfano wa watangazaji wa Redio Maria

Vyura99tu

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
1,640
1,747
Wadau na wasikilizaji wa habari.

Nimekuwa msikilizaji wa hasa kwenye kipindi za yaliyokujia magazetini.

Ni jambo linalotiashiria kutokuwa na watangazaji/wasomaji makini. Au kwa namna nyingine hawakusoma kiswahili fasaha wanakuwa kama wageni wasiojua Kiswahili.

Mfano tu wa wasomaji wa Mkatavi. Kwa ujumla hawako makini na jinsi ya usomaji aidha atarudia neno la kiswahili akitafakari jinsi ya kulisoma wakati limeandikwa vizuri na kwa maandishi makubwa tuu! Isitoshe ataweka Aa, aah aah nyingi tu! Ukija kwenye kutamka kurasa za magazeti utasikia mbele, nyuma! Kwanini usitamke ukurasa wenyewe?

Pia pale inapofikia labda kuna habari inayohusu chama fulani anafunika maneno, na pale pa chama kusifia atasoma kwa herufi.

Watangazaji/wasomaji wa Redio Maria wako makini na hutamsikia akikosea kusoma hata neno na hakuna aah, aah! Nawasifu kwa kweli wako makini.

Jaribuni kufuatilia na kujisahihi katika usomaji wenu.

Kiswahili lugha ya Taifa.
 
Siku hizi si wanaperuzi na kudadisi??
Basi lugha iliyoandikwa inabadilishwa…….
 
Back
Top Bottom