Watangazaji wa kipindi cha Sebuleni cha Clouds Plus wamegeuzwa wasemaji wa Serikali badala ya wachambuzi

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Pengine kutokana na hulka ya JPM kufanya teuzi mbalimbali za wasaidizi wake kutoka vyombo mbalimbali vya habari inawezekana kabisa hii dhana imewaondolea weledi baadhi ya watangazaji wengi wa vyombo hivi na kuamua kujikita katika kuwa wasemaji wa serikali na badala ya kuwa wachambuzi wa habari.

Msukumo huu pia naona umepelekea wengi wao kuamua kujiingiza katika siasa za kuwania ubunge ili hali wakijua kabisa hawawezi kuvuka hata hatua ya mwanzo ila wamehadaika na kauli wanazoambiwa kuwa wanatakiwa kuonekana wakifanya jambo fulani kusudi waonekane na ngazi za juu.

Tukirudi kwenye mada, pamoja na kupoteza mvuto wa kufuatilia vyombo vingi vya habari kutokana na taarifa zao kuwa za upande mmoja, leo nilijikuta naangalia kipindi cha Sebuleni kinachorushwa na TV Clouds Plus na mada waliyokuwa wanajadili ni kuhusu Serikali kuamua kulipa malimbikizo ya madeni ya pesa wanazodai wakulima wa korosho zaidi ya mwaka sasa.

Watangazaji wametumia zaidi ya dakika 20 wakieleza manufaa ya serikali kufanya malipo na ahadi ya kumaliza deni hilo kabla ya mwisho wa mwezi huu. Katika Dk. 20 zote hakuna uchambuzi uliofanyika hata chembe bali waliishia kutoa taarifa kama wasemaji wa serikali na kusifia tu.

Hii inamaanisha kwa mtu asiyefahamu historia ya majanga yaliyowapata wakulima wa korosho mwaka jana kutokana na uzembe wa serikali hawezi kupata habari ya kweli hata chembe.

Ushauri kwa wenye vyombo hivi vya habari, wawaangalie hawa vijana waliogeuza vipindi kuwa majukwaa ya kujineemesha kisiasa kabla hawajapoteza watazamaji.

Nawasilisha
 
Watu wanachungulia fursa. Awamu hii kama unakipaji cha unafki basi utakula meza moja na wakuu. UNAFKI awamu hii unalipa
 
Back
Top Bottom