Watangazaji wa ITV na Kiswahili potofu!

K-Boko

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
697
218
Hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu tumekuwa tukisikia Kiswahili kibovu kikitumiwa na baadhi ya watangazaji wa ITV na hasa matumizi ya neno "Lakini". Kwa mfano, mmoja wao alisema: "...Watazamaji na wasikilizaji wetu mnaojiunga sasa na ITV, Radio One Stereo 'lakini' Capital Radio...."

Sasa hapo neno "lakini" linaingiaje?
 
muhulize mama yako, au kafungue TV yako ukatangaze kiswahili sanifu. mbwa wewe
 
Mteule huteuliwa na kiongzi ngazi za juu mfano viti maalum vya cdm na kuchagiliwa huwa ni kwa kupiga kura
 
Hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu tumekuwa tukisikia Kiswahili kibovu kikitumiwa na baadhi ya watangazaji wa ITV na hasa matumizi ya neno "Lakini". Kwa mfano, mmoja wao alisema: "...Watazamaji na wasikilizaji wetu mnaojiunga sasa na ITV, Radio One Stereo 'lakini' Capital Radio...."

Sasa hapo neno "lakini" linaingiaje?
Pengine hiyo 'lakini' ni freudian slip of tongue hainishangazi sana kwa hawa watangazaji wetu na lugha ya kiswahili. Ila nashangaa sana ninapomsikia mtangazaji akisema: .........majeruhi watatu wa hiyo ajali walikimbizwa hospitali na njiani mmoja wa majeruhi aliweza kufariki!
Kiswahili kibovu sana cha matumizi ya 'kuweza'
 
Sio slip of the tongue kwa sababu wanalirudiarudia na sio mmoja. Hayo maneno mawili "lakini" na "kuweza" wanayatumia vibaya hadi inakera!
 
jamani matusi yanatokea wapi tena hoja zote zilizotolewa ni za msingi ila si busara kutaja jina la mlengwa tafadhalini
 
Masako pia huwa anashindwa kutofautisha alama za kufungua na kufunga semi (inverted commas) na mabano (brackets) anaposoma vichwa vya magazeti kwenye kipindi cha Asubuhi.
 
Hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu tumekuwa tukisikia Kiswahili kibovu kikitumiwa na baadhi ya watangazaji wa ITV na hasa matumizi ya neno "Lakini". Kwa mfano, mmoja wao alisema: "...Watazamaji na wasikilizaji wetu mnaojiunga sasa na ITV, Radio One Stereo 'lakini' Capital Radio...."

Sasa hapo neno "lakini" linaingiaje?
Lakini inatumiwa sivyo, na siku hizi hata mwanasiasa namba moja naye hotuba zake ni hivyo hivyo, lakini... lakini
 
Back
Top Bottom