Watangazaji wa Clouds punguzeni kujiona mmefanikiwa sana, ninyi ni mafacilitator hamuwezi kuwa mnajua kila kitu

Twinawe

JF-Expert Member
Oct 3, 2016
2,363
5,108
Huwa nafatilia Clouds Media sana hasa vipindi vya PB, XXL, Jahazi, Amplifaya, Sports Extra, Ala za Roho na Njiapanda.

Watangazaji wa hivi vipindi wana kitabia cha kujiona wamefanikiwa sana kimaisha wameptia changamoto kiasi wanaweza kumshauri mtu yeyote kuhusu maisha(kujiajiri wakati wao wameajiriwa)

Kitu kingine wana tabia ya kuongelea mambo yanayohitaji ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wanasahau wao ni facilitators tu.

Badilikeni Clouds
 
Uwa nafatilia clouds media sana hasa vipindi vya pb,xxl,jahazi.amplifaya.sports. diva na njiapanda.

Watangazaji wa hivi vipindi wana kitabia cha kujiona wamefanikiwa sana kimaisha wameptia changamoto kiasi wanaweza kumshauri mtu yeyote kuhusu maisha(kujiajiri wakati wao wameajiriwa)

Kitu kingine wana tabia ya kuongelea mambo yanayohitaji ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wanasahau wao ni facilitator .

Badilikeni clouds
Jamaa kila kitu wanajitia wanajua,si wanaume si wanawake
Pia utawasikia"wewe gari yako unaosheaga wapi?..Mimi yangu sinza..na wewe diva?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kila kitu wanajitia wanajua,si wanaume si wanawake
Pia utawasikia"wewe gari yako unaosheaga wapi?..Mimi yangu sinza..na wewe diva?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mamburula tu yale walahi ukifumua ofisi nzima pale hamna mwenye cheti cha uamdishi wa habari walahi,wachache ndio wamesomea na ni kundi la wahuni ambalo kusaga kaliokota huko na kuja kulimwaga pale ndio maana hayana weledi walahi

Mtu mwenye weledi pale ni millard, Gadna Habash wengine wote ni waganga njaa tu walahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mamburula tu yale walahi ukifumua ofisi nzima pale hamna mwenye cheti cha uamdishi wa habari walahi,wachache ndio wamesomea na ni kundi la wahuni ambalo kusaga kaliokota huko na kuja kulimwaga pale ndio maana hayana weledi walahi

Mtu mwenye weledi pale ni millard, Gadna Habash wengine wote ni waganga njaa tu walahi

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti Jose Mara nae mtangazaji..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni tatito sugu la Watangazaji na waandishi wa habari Tanzania. Niliwahi kuangalia kipindi cha jamaa mmoja anajiita ni muandishi nguli, jina ni Mjengwa.Anaalika mtu kumuhoji, lakini yeye ndiye anaongea saaanaa, na kutoa maelezo meengi kuliko aliyeitwa kuhojiwa, nikajiuliza huu ndio uandishi au uana habari gani?

Nikaangalia clip moja ya muandishi iko humu JF, huyu facilitator aliuliza swali refu, na akatoa maelezo meengi, nikamuangalia mtaalam anasubiri kujibu jamaa amalize swali, alilijibu kwa sentensi moja tu akawa amemaliza. Nikabaki nacheka tu peke yangu.

Unamualika mtaalam kumuhoji, facilitator jiandae maswali yatakayo ishibisha jamii au audience yako. Na ukiwa huna maswali basi alika watazamaji wakusaidie kuuliza, au kabla hujaandaa kipindi tafuta watu wenye uelewa na unachotaka kuongea wakusaidie kuuliza maswali yenye substance,au rusha kipindi online watu waulize FB,tweeter na kadhalika.

Lakini wao wanaongea kuliko waliyemualika, badala mtaalam wa mada ndiye awe muongeaji mkuu, unakuta facilitator ndiye anaongea sanaa kuliko aliyealikwa, sasa ulimualika wa nini huyo mtaalam?

Sijui wote huwa wanahitimu chuo kimoja au ndio miongozo ya taaluma yao yako hivyo?
 
Wanakera sana wanaonaga wanaweza kila hustle
Yaani Ukitaka kujiona wewe masikini sikiliza hiyo radio.
Kuna huyu bidada wa power breakfast....
Anajikutaga sijui nani. Utafikiri analipwagwa milioni 100 kwa mwezi.
afu wote wanajifanya wanamaisha mazuri.
Ila kwa sasa nimeacha kuisikiliza hiyo radio mawingu
 
Ukizungumzia Clouds ni kama unazungumzia mashoga like Harry kapiga,Bdozen etc endelea kusikiliza hiyo redio mkuu nawewe utageuka shoga utakua shoga then watakuajiri ukapambane na hao unaosema wanajiona.
 
Matangazo ni mengi mpaka inaboa kusikiliza ingawa tunajua radio huwa zinaendeshwa kwa matangazo but kwa klaud its too much
Binadamu tumezaliwa na masikio 2 lakini mdomo mmoja hivyo basi linapokuja suala amealikwa mtaalamu Inabidi tumsikilize zaidi kuliko kuongea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Radio ya vijana wanao baree ile ambao hawajui A to Z kuhusu maisha mtu mwenye akili timamu na upo mature huwezi kukaa kusikiliza upumbafu wao ambao wanajadili, story zao ni zakibunuasi bunuasi kama za kijiweni kwa wavuta bangi, mfano eti mtu alianza na mtaji wa elfu hamsini in two year leo ana miliki 40 million, ukiuliza alikopa eti hapana ni juhudi tu sasa hizi si story za wavuta bange kijiweni maana story hazina uhalisia kabisa

Wale kina kapiga nk waongea kuhusu mafanikio nakujiajili ili hali na wao wameajiliwa miaka nenda rudi wapi kufanya maisha ya ujanja ujanja mjini tunawangalia tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom