Watangazaji wa BBC, DW na kwingineko achaneni na matumizi ya neno hili

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
Halo JF,

Kumekuwa na matumizi mabaya ya neno "Angalau" kunakopigiwa upatu na radio za kimataifa za BBC, DW, VOA nk.

Wenyewe wamehamisha moja kwa moja kutoka lugha ya Kiingereza "Atleast" likimaanisha angalau.

Mfano utasikia watu ANGALAU mia tano wakoseshwa makazi huko Burkina Fasso.

Kiswahili sahihi ni kuwa watu TAKRIBAN mia tano wakoseshwa makazi huko Burkina Fasso.
 
Sasa hilo Angalau linamakosa gani?

Kiswahili hakikuwi?
Ukitukia angalau inaonekana kama unatamani ingelikuwa zaidi ya hapo
Angalau lina maana ya at least lakini ni katika muktadha fulani tu, nyingine haifai

Mfano unaweza kusema
"Kila mfanyakazi awe analipwa angalau sh.laki moja kwa mwezi." Hapo ni sawa

Ila ukisema "Angalau watu 10 wamefariki kwa kipindupindu". Inaleta ukakasi

Ingetakiwa " Watu wasiopungua 10 wamefariki kwa kipindupindu"
 
At least humaanisha kadirio..

Hivyo ikisemwa INAKADIRIWA.... italeta maana.

Neno angalau humaanisha afadhali, ahueni and so of likes
 
Maneno ya kiswahili hutumika kimakosa maeneo mengi,na watu aghalabu hurudia makosa hayo bila kufahamu eneo la kuweka neno husika..
 
Neno 'Angalau' halina makosa yoyote. Neno hilo ni tafsiri ya moja kwa moja ya neno la Kiingereza, 'At least'.

Neno 'Takriban' ama 'Takribani' kwa lugha ya Kiingereza ni 'Approximate' na si At least. Neno 'Takriban' lina maana ya idadi inayokaribiana na idadi kamili (idadi ya makadirio).
 
Ukitukia angalau inaonekana kama unatamani ingelikuwa zaidi ya hapo
Angalau lina maana ya at least lakini ni katika muktadha fulani tu, nyingine haifai

Mfano unaweza kusema
"Kila mfanyakazi awe analipwa angalau sh.laki moja kwa mwezi." Hapo ni sawa

Ila ukisema "Angalau watu 10 wamefariki kwa kipindupindu". Inaleta ukakasi

Ingetakiwa " Watu wasiopungua 10 wamefariki kwa kipindupindu"
Hapo angalau umedadavua kidogo
 
Neno 'Angalau' halina makosa yoyote. Neno hilo ni tafsiri ya moja kwa moja ya neno la Kiingereza, 'At least'.

Neno 'Takriban' ama 'Takribani' kwa lugha ya Kiingereza ni 'Approximate' na si At least. Neno 'Takriban' lina maana ya idadi inayokaribiana na idadi kamili (idadi ya makadirio).
Sasa huoni takriban ndiyo sahihi
 
Back
Top Bottom