watangazaji redio/tv wajifunze zaidi!

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,492
7,515
jumatano na alhamisi asubuhi baada ya uefa champions league nilikuwa nasikiliza redio fulani. ilipofika kwenye kipengele cha habari za michezo wakizungumzia michuano hiyo wale watangazaji waligusia matokeo ya timu ya arsenal na barcelona pekee na kuacha yale ya shakhatar na roma hiyo j5. alhamisi wakarudia makosa hayo wakatangaza matokeo ya tottenham vs milan pekee na kuacha yale ya shalke vs valencia.
sasa najiuliza hawa watangazaji ni mawakala wa timu za Uingereza au!?

makosa mengine ni utamkaji wa makosa wa majina mfano Ouattara wa ivory Coast kuna mtangazaji alikuwa anatamka Katara. sasa najiuliza hivi hawa jamaa huwa hawasikilizi au kuangalia habari kutoka kwenye vyombo vingine vya habari kusikia jinsi majina ya watu na miji yanavyotamkwa au waandaa habari wanawaletea tu makaratasi na wao wanasoma. maana sipati picha mfano mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou kuutamka kwake kama haujawahi kuusikia ukitamkwa maana ni zaidi ya kusoma hapo.
Inabidi wachukue muda wao kujifuna zaidi kuondokana na makosa kama hayo ya ushabiki na makosa mengineyo.
http://www.google.com/url?sa=t&sour...sg=AFQjCNHikfIEHSGyj6ufVZj1OL4eEjf9BA&cad=rja
 
Wengi wao wanatia hata huruma ukiwasikiliza. Inaelekea ni wavivu wa kujisomea hata magazeti. Pia wengi wao upeo wao ni mdogo ktk uelewa wa mambo. Hasa hawa wa TV, Radio na Magazeti ya udaku.
 
They don't practice a really media proffessionalism, nadhani elimu ni kikwazo.
Yo..yo...nyiingi mno, dot.com inawasumbua sana.
 
Back
Top Bottom