Watangazaji na Wachambuzi wa Habari za Michezo wa 'hovyo hovyo' huenda wakawa wanapatikana Tanzania tu pekee

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,462
108,617
Yaani tukio la Bernard Morrison Kuvua Bukta yake, kubakia na Chupi ya Njano huku Bukta akiiweka Kichwani mwake linajadiliwa kwa dakika 120 ila tukio la Tonombe Mukoko la Kumpiga Kiwiko kibaya John Boko ambacho kingeweza Kumjeruhi vibaya kwa Kumvunja Pua au Kumng'oa Meno yake au hata Kumsababishia Kifo limejadiliwa kwa dakika 10 tu.

Naelekea kuacha Kusikiliza Vipindi vya Michezo vya Redioni na Wachambuzi wao kwani huko sasa Kumevamiwa na Watu wa 'hovyo hovyo' tupu ambao wamejaa Chuki, Unafiki na Mahaba kwa Timu iliyolaanika na iko katika Mkondo wa Maji Bahari kuelekea Daraja la Salenda kupitia Muhimbili Hospitali.
 
Wana ufara mwingi sana hao wachambuzi, mfano metacha kunyoosha dole la kati jemedari aliongelea dakika chache

Ila kosa la mkude alisimamia kidete bila kujua ata anatuhumiwa na nini, jana ivyo ivyo kwa morisson naona kashikia bango

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Yaani tukio la Bernard Morrison Kuvua Bukta yake, kubakia na Chupi ya Njano huku Bukta akiiweka Kichwani mwake linajadiliwa kwa dakika 120 ila tukio la Tonombe Mukoko la Kumpiga Kiwiko kibaya John Boko ambacho kingeweza Kumjeruhi vibaya kwa Kumvunja Pua au Kumng'oa Meno yake au hata Kumsababishia Kifo limejadiliwa kwa dakika 10 tu.

Naelekea kuacha Kusikiliza Vipindi vya Michezo vya Redioni na Wachambuzi wao kwani huko sasa Kumevamiwa na Watu wa 'hovyo hovyo' tupu ambao wamejaa Chuki, Unafiki na Mahaba kwa Timu iliyolaanika na iko katika Mkondo wa Maji Bahari kuelekea Daraja la Salenda kupitia Muhimbili Hospitali.
ukiacha upolisi ambao weng ni divisheni 4 , waandishi wa habari wengi ni divisheni 4 mpaka zero.
Hawajui zaidi ya kusoma blog za watu na kutafsiri kwa kiswahili kama clouds wafanyavyo.
 
Mbona kama Ilikua ya blue au mimi ndo niliona vibaya ?? ..
Kwanini mnakuwa Wabishi nyie? Alivalia Chupi Rangi ya Njano nendeni ( ingieni ) huko YouTube muone. Mnaboa na Kunichosha sasa.
 
Back
Top Bottom