Watanganyika tufanye juhudi za kuvunja muungano wa tanganyika na zanzibar

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
12,530
2,000
Ndugu wana JF pamoja na kujua kuwa kuna watu wangependa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uendelee kuwepo nimeona nilete hii mada hapa ili nipate mawazo ya wadau wa JF juu ya muungano huu amabao kwangu naona ni wa gharama zisizo na lazima na usio na faida yoyote kwa pande mbili. Japo kuna mengi yanayonikera kwenye muungano huu haya hapa ndio haswa yanayonitia kichefuchefu:

Kwa nini Zanzibar imepewa upendeleo wa kuwa na wabunge wengi sana kwenye bunge la muungano ukilinganisha na idadi yao ya watu? Kwa maoni yangu ingetosha Zanzibar yote kuwa na wabubge watano tu. Wawili Pemba na watatu Unguja. Ukiangalia matokeo ya uchaguzi uliopita mbunge wa Zanzibar anachaguliwa kwa wastani wa kura 4000-6000 kwa mshindi. Idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na wabunge wa huku bara. Ndio kusema kama hali hii ingelikuwa huku kwetu basi labda kila mtaa ungekuwa na mbunge. Hizi ni gharama zisizo na maana na ni sababu moja ya kuvunja muungano.

Kila siku tumekuwa tukisikia malalamiko ya Wazanzibar kuhusu mafuta na rasilimali nyinginezo wakitaka ziwe zao kama dhahabu zilivyo zetu. Wanataka rais wao atambuliwe kama amiri jeshi mkuu na kupigiwa mizinga. Sasa kama wanataka mamlaka yote hayo kwa nini tusiachane nao wakaangali mustkabali wao na sisi tungahangaika na wetu?

Najua kero zipo nyingi lakini naomba tuchangie ili tujuzane kama kweli muungano huu una manifaa yoyote kwetu.
 
Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,266
2,000
... muungano huu amabao kwangu naona ni wa gharama zisizo na lazima na usio na faida yoyote kwa pande mbili.
Unasema pande zote hazifaidiki, unajuaje Zanzibar hawana faida na huu Muungano? Zanzibar wananufaika zaidi, tusiwaongelee Zanzibar, tujisemee sisi , kwamba Muungano ni zigo la hasara na uonevu mkubwa sana kwetu sisi Tanzania Bara.

Lakini mwisho wa siku, ni mkenge ambao tuliuvaa wenyewe, kupitia huyu mwakilishi wetu "Baba wa Taifa." Hatuna wa kumlaumu katika hili.
 
Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,686
0
Ndugu wana JF pamoja na kujua kuwa kuna watu wangependa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uendelee kuwepo nimeona nilete hii mada hapa ili nipate mawazo ya wadau wa JF juu ya muungano huu amabao kwangu naona ni wa gharama zisizo na lazima na usio na faida yoyote kwa pande mbili. Japo kuna mengi yanayonikera kwenye muungano huu haya hapa ndio haswa yanayonitia kichefuchefu:

Kwa nini Zanzibar imepewa upendeleo wa kuwa na wabunge wengi sana kwenye bunge la muungano ukilinganisha na idadi yao ya watu? Kwa maoni yangu ingetosha Zanzibar yote kuwa na wabubge watano tu. Wawili Pemba na watatu Unguja. Ukiangalia matokeo ya uchaguzi uliopita mbunge wa Zanzibar anachaguliwa kwa wastani wa kura 4000-6000 kwa mshindi. Idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na wabunge wa huku bara. Ndio kusema kama hali hii ingelikuwa huku kwetu basi labda kila mtaa ungekuwa na mbunge. Hizi ni gharama zisizo na maana na ni sababu moja ya kuvunja muungano.

Kila siku tumekuwa tukisikia malalamiko ya Wazanzibar kuhusu mafuta na rasilimali nyinginezo wakitaka ziwe zao kama dhahabu zilivyo zetu. Wanataka rais wao atambuliwe kama amiri jeshi mkuu na kupigiwa mizinga. Sasa kama wanataka mamlaka yote hayo kwa nini tusiachane nao wakaangali mustkabali wao na sisi tungahangaika na wetu?

Najua kero zipo nyingi lakini naomba tuchangie ili tujuzane kama kweli muungano huu una manifaa yoyote kwetu.

Inatia Hasira Pemba yenye watu 350,000 inakuwa na wabunge 18! Kama ingekuwa hivyo sijui ubungo ingekuwa na wabunge wangapi maana waliojiandikisha tu walikuwa laki nne!
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068
2,000
Unasema pande zote hazifaidiki, unajuaje Zanzibar hawana faida na huu Muungano? Zanzibar wananufaika zaidi, tusiwaongelee Zanzibar, tujisemee sisi , kwamba Muungano ni zigo la hasara na uonevu mkubwa sana kwetu sisi Tanzania Bara.

Lakini mwisho wa siku, ni mkenge ambao tuliuvaa wenyewe, kupitia huyu mwakilishi wetu "Baba wa Taifa." Hatuna wa kumlaumu katika hili.

Siungi mkono kuuvunja muungano, lakini kutokana na jinsi wenzetu wanavyolalamika kuna wakati tunaweza kulalamika kuuvunja muungano. Wao wanaona kama sisi ni wa bara ni kikwazo kwa maendeleo yao na pia tunawanyonya na tunawategemea wao.

Kwa msingi huo ni wazi kuwa wanaweza kujiendeleza na kujimudu wenyewe.....na wanaona kuwa kwa sababu wao wana mafuta sisi tutawategemea wao.

Kweli ni heri Tanganyika irudi na Zanzibar, iache iende. Wao wanataka mwarabu aje awatawale na awaletee misaada, kitu hicho bara kina wanalakini kidogo.
 
bona

JF-Expert Member
Nov 6, 2009
3,799
2,000
ndhan kuna sababu za msingi kabisa kwa sisi wabara kutaka muungano uvunjike, kwanza wenzetu wanafaidika sana na huu muungano, nchi ya wau wachache lakini pesa za maendeleo kiuwiano wa watu na kiwango si sahihi, hata hivyo wanadhan kua watafaidika zaidi iwapo muungano utavunjika kwa sababu wataenda kwa waarabu wajitambulishe kua wao ni waislam sana wapewe misaaada, kikubwa kwao ni tamaa ya misaaada zaidi sio kama wanauwezo wa kufanya kazi na kujiletea maendeleo! so tuna ambition tofauti tuachane nao, hata nafasi za serikalini wao wako wachache lakini wanatoa viongozi wengi!
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,506
2,000
Hayo yalikuwa makubaliano ya J.K.N na A.K wakati wanaunda muungano.

Hamna watanganyika katika nchi hii,kuna Watanzania na wazanzibari.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom