Watanganyika someni ujumbe huu kutoka Zanzibar

Hakuna cha muungano wa mkataba wala nini,hapa ifanyike referendum na maamuzi yaheshimiwe! Kama ni kuvunja muungano ndiyo maamuzi yatakayofikiwa basi na uvunjwe tu kwa roho safi!

Lakini wazanzibari watalalamika mpaka lini si bora wawashawishi baraza la mapinduzi wapitishe maamuzi ya kuvunja muungano basi tuone kama kuna mtu atakayewabishia?

Mbaya zaidi hata makamu wa raisi wa Zanzibar nae analalamikia muungano na mawaziri wake sasa sijui nataka wafanye nini wananchi wake...
 
Sultani keshamcash Jk so Wazenji Soon Mtakuwa chini ya Sultan wenu mnaye mlilia
 
Kuna bandiko moja linasomeka kuwa: "Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani ya muungano ni lazima".
Hii kwangu Mtanganyika haitoshi.

Mimi nataka "Zanzibar yenye mamlaka kamili nje ya Muungano".
Tuwe nchi mbili jirani. Tutaishi vizuri tu.
 

Waache wachome makanisa.....siunaona meli zinavyo zama.......! Nyumba za ibada zinakosa gani ugomvi wa huyu na yule?

Kibanga Msese
 
Wakimalizana na Watanganyika watagundua kwamba kuna Wazanzibari na Wazanzibara
 
hao mimi nilsha wapuuza kitambo!! haingi akilini wanadanganywa na mtu hata siasa hajui kumbe yeye anautaka URAIS wa ZANZIBAR!! MAALIM ana mambo! sasa anata atawale masikini wale sijui itakuwaje. waende zao wakapumue tuiwaone kama hawajaja kununua chapati kariakoo.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amembana Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Mkongwe (Cuf), Ismail Jussa aeleze kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa mkataba unavyopaswa kuwa na mgawanyo wake wa madaraka.
Jaji Warioba alichukua hatua hiyo baada ya Jussa kusimama na kutoa maoni ya kutaka mfumo wa Muungano wa mkataba, wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikichukua maoni ya Wawakilishi mjini Zanzibar jana.Alimtaka Jussa atoe mfano angalau mmoja au miwili ya uendeshaji wa serikali ya mkataba ili Tume yake ipate ufahamu katika mapendekezo yake.

Jussa alisema anayo mifano zaidi ya 100 lakini akadai wakati ukifika serikali zinazohusika zitakaa na kuja na fomula ya mgawanyo huo pamoja na uendeshaji wake kimadaraka.

Hata hivyo, Jaji Warioba kwa upande wake akionekana kutoridhika na maelezo hayo ya Jussa alimtaka kuiambia Tume alivyojiandaa na Muungano wa mkataba kinyume na mfumo dola uliopo.

“Bwana Mwakilishi hebu tupe lau mfano mmoja au muundo wa uendeshaji wa Muungano wa serikali ya mkataba ili uweze kukidhi haja yako na kutuonyesha njia” alisema Jaji Warioba.

“Hebu tuweke wazi juu ya utashi wa mpango unaofikirika wa kuwa wa serikali ya mkataba, nafikiri unachokusudia ni kutaka kuvunja Muungano uliopo” alisema Warioba.
Hata hivyo, Jussa alibaki katika msimamo wake huku akisisitiza kuhusu kukaa kwa serikali mbili na kutoa mfumo wa uendeshaji wa serikali ya mktaba.

Akifafanua, Jaji Warioba alisema kimsingi kudai Zanzibar iwe na mamlaka kamili, huku Tanganyika nayo ikiwa na mamlaka yake ni sawa na kuvunja muungano kwa kuwa kila upande utalazimika kuwa na kiti Umoja wa Mataifa (UN).

“Tanganyika na Zanzibar zikiwa kila moja ina mamlaka yake hakutakuwa na neno Muungano, ndiyo maana nasema nisaidiwe juu ya kupata mfumo wa kuendesha Muungano unaotakiwa chini ya mkataba” alisema Jaji Warioba.

Akiwekea mkazo katika hoja iliyotolewa na Jaji Warioba, mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo, Paramagamba Kabudi, alisema inasikitisha kuona hadi sasa wanaotaka Muungano wa mkataba wanashindwa kutoa rasimu ya mfano wa serikali ya mkataba ili kuisaidia Tume juu ya kile wanachokitetea.

Wakitoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM na CUF waligawanyika pande mbili huku wale wa CCM wakitetea mfumo wa serikali mbili na wa CUF wakitaka Muungano wa mkataba.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha alisema muundo wa Muungano wa serikali mbili ndiyo muafaka kwa kuwa umeonyesha faida katika masuala ya ulinzi na usalama lakini pia ukijenga umoja wa kitaifa.

Akishauri Nahodha alisema hata hivyo ni vyema ikafika mahali kukawa na mabunge mawili , moja dogo litakaloshughulikia mambo ya Muungano na jingine lishughulikie mambo ya Tanganyika.

Aidha alitaka nafasi ya Rais wa Muungano itolewe kwa zamu kila upande uwe na kipindi cha miaka kumi.

“Mgawanyo wa mapato usiangalie idadi ya watu kwa vile hata kama Serikali moja ikiwa na watu wawili bado ina jukumu la kuwapatia maisha bora na huduma wananchi wake” alisema.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar Said Ali Mbarouk alisema mfumo wa sasa wa Muungano una matatizo kwakuwa kuna mambo ambayo si ya Muungano lakini yanasimamiwa na Muungano kinyume na makubaliano ya mwaka 1964.

Aliyataja baadhi ya mambo aliyodai yanayoleta mkanganyiko kuwa ni utalii, maliasili, habari na michezo ambayo alisema yanahitaji kuwekewa utaratibu na kuzungumziwa kwake katika medani za kimatifa.

Waziri asie na Wizara Maalum Machano Othman Said alitaka mfumo wa Muungano wa sasa uendelee na kutaka Rais wa Zanzibar kubaki kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza alitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka sawa na Rais wa Muungano pamoja na Zanzibar kupata nafasi ya kujiunga na jumuiya ya OIC na nyingine za kiuchumi duniani.

Tume ya mchakato wa ukusanyaji wa maoni inayoongozwa na Jaji Warioba ipo visiwani Zanzibar na tayari imekutana na wananchi katika mikoa ya Kaskazini Unguja na Pemba.
 
Hakuna cha muungano wa mkataba wala nini,hapa ifanyike referendum na maamuzi yaheshimiwe! Kama ni kuvunja muungano ndiyo maamuzi yatakayofikiwa basi na uvunjwe tu kwa roho safi!

Lakini wazanzibari watalalamika mpaka lini si bora wawashawishi baraza la mapinduzi wapitishe maamuzi ya kuvunja muungano basi tuone kama kuna mtu atakayewabishia?

umebaki kuwa ni muungano wa baadhi ya viongozi
 
Umefanya la maana kuweka hizo picha maana watu bichwa dafu wataelewa nini tunataka sisi wazanzibari
 
Adui namba moja wa watanganyika ni CCM, ndiyo yenye sera ya serikali mbili na kuukumbatia muungano feki huu, watanganyika tuungane tuiondoe CCM madarakani kisha tuwape wazanzibari kile wanachokitaka yaani tuuvunjilie mbali huu muungano na manung'uniko toka pande zote yataisha.
 
Back
Top Bottom