Watanganyika, ni sisi tumeing'ang'ania Zanzibar au ni wao wametuganda kama kupe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanganyika, ni sisi tumeing'ang'ania Zanzibar au ni wao wametuganda kama kupe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Aug 3, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mtu unaamka nyumbani kwako asubuhi, pamoja na mawimbi na dhoruba hutulii kwako...unavuka bahari kuelekea nyumbani kwa mwenzio. Jioni baada ya kusetiriwa na kuchuma unachoweza huko ugenini unafunga safari, unavuka tena bahari hadi nyumbani kwako na kuuchapa usingizi mwonono ukisubiri kesho yake uende kuchuma tena.

  Cha ajabu ni kuwa pamoja na kufaidi vya mwenzio, huachi kulalama kwamba kakung'ang'ania huku uhuru unao wa kuamua utakachoona kinakufaa! Ama ni kama yale ya kupe...jua linampiga mchana wote toka asubuhi hadi jioni lakini kamng'ang'ania ng'ombe kwani afanye nini? Aache kunyonya? Tofauti na Wazanzibari, kupe halalamiki.
   
 2. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sasa mkuu wewe unaona hatima ya hii kitu itakuwaje??? Maana Wazenj wanataka talaka, wenye mamlaka wanadai 'jadili mambo yote, lakini si muungano. Mwisho wake ni nini??
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Dawa ni moja tu, ama ni serikali moja au hakuna Muungano. Hilo la Wazenj kutaka talaka ni geresha tu...salama yao ni ndani Muungano kama salama ya mafisadi ilivyo ndani ya CCM.
   
 4. a

  abousalah2 Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee uwache kujidanganya! Subiri ule uke naona mataptap yanakupumbaza! Znz itaishi bila pumzi za tanganyika!
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wanangu, kulalamika lalamika au kupeana majina mabaya si jibu. Heri wale wanaoona kuwa kuwe na serikali moja kuliko wanaotaka kujitenga au kuwa na serikali tatu. Kama sisi tunapendana na kuaminiana kama ndugu wa nchi na bara moja, tunashindwa nini kuwa mwili mmoja? Ingawa wazanzibari wamekuwa wakifikiri kuwa nje ya muungano wanaweza kuishi vizuri zaidi huku wabara nao wakiwaona wazanzibari kama kupe, ukweli ni kwamba hakuna mshindi katika uamuzi wa kuuvunja muungano. Ila kama mtaona kuuvunja ni jibu fanyeni hivyo muone nani atalia na kucheka kwanza.
   
 6. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  kupe huyu ananikumbusha kisa cha mjomba na shangazi.
  Mjomba alikuwa ana mali nyingi,
  mchapa kazi mzuri,
  lakini mlevi umbwa,
  malaya mbwa,
  mzembe mbwa,
  lakini si mtu wa ugomvi.

  Sasa kila akirudi matembezi,
  kalewa bwiii,
  shangazi humsachi mifukoni,
  na kumwibia kila senti,
  asubuhi kukicha shangazi,
  huuliza fedha ya matumizi,
  mjomba kucheki mifukoni,
  ana shs 1000 tu,

  Shangazi humjia juu,
  hela unachuma unahonga,
  mjomba huwa hana cha kusema,
  hadithi hiyo,
  iliendelea kujirudia mpaka........... jaza mwenyewe
   
 7. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Msalagambwe kisa chako kinafikirisha ingawa hakuna nafuu kati ya mjomba wako kihiyo na shangazi yako kibaka. Mwanangu nadhani tumekuelewa kama siyo kukulewa. Ila ukiangalia kinachoendelea mjomba anasachiwa na mafisadi na wawekezaji na si shangazi yako aitwaye Zenj. Yeye angependa awe mshikaji wa kumweka nyumba ndogo toka Arabuni ingawa hajui kuwa hawa jamaa ni wabaguzi na wakatili.
   
 8. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Let Znz go. Hakuna faida ya Muungano huu usio na haki sawa.
   
 9. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Nimefurahi kumalizia simulizi kwa,
  kusema wazi juu ya shangazi,
  shangazi huvuta pochi,
  na kulala na kula na maghaibhu,
  uzuri wa sura zao adhani,
  hata roho zao nzuri kuliko ya mjomba,
  Ukweli wana roho za mazimwi,
  si muda atakuwa kitanzini,
  kisa rangi yake na nywele za katani,
  watamzalisha bila majira lakini,
  hatakuwa mmoja wao.

   
 10. C

  Cheida Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefurahi sana uwepo wa mada hii, ila munafaham kama wakati unaongea?ikiwa mbatata, vitunguu jiulize je watu hupewa bure, munasahau hata kuipenda na kuitafuta Tanganyika, kama munadhani waznz wanaung,angania huu muungano kwanin mh kikwete hatmki km mgogoro wa kikatiba ni kutoa kiti cha umoja wa mataifa kwa wenyewe na kuwaachia huru kama mwanzo, na kama kunahitajika muungano ni kimkataba tu na sikikatiba, munasahau waliosema yakwamba Znz ipo karibu Na Dubai na vitu kuja kuchukua Znz, jiulize iweje leoooo
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanangu Cheida mawazo yako ni ya kitumwa. Usidhani hiyo Dubai mnayoabudia kusifia na kusifiwa iko hivyo. Haina tofauti na Marekani. Wengi wakiona Los Angeles na filamu zake mulua hudhani Marekani yote iko hivyo.

  Kama wazanzibari hawataki huo muungano si watamke wao waone kama ni rahisi? Hicho kiti unachosema kuchukua UM si big deal. Hata mkichukua bado kile cha Tanganyika kitakuwepo kama ambavyo kilikuwapo kabla ya chenu kuchongwa.

  Kimsingi, Karume kwa kuogopa kitisho cha kuvamiwa na kupinduliwa na waarabu mnaowaabudia aliamua kuomba msaada wa kuungana na bara. Sasa hapa tatizo la bara liko wapi kama siyo znz kuletwa kwenye ndoa hii inayogeuka kuwa ndoana na shida zake?
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,058
  Trophy Points: 280
  Cheida,

  ..miaka michache ijayo bandari ya Znz itakufa kutokana na ushindani toka bandari za Lamu na D'Salaam.

  ..Zanzibar achaneni kabisa na ndoto za uchumi unaotegemea bandari.

  wa-Znz ombeni MUNGU awajaalie mafuta, au ikiwezekana imarisheni utalii, na mambo yenu yatakuwa safi.
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Hizi hadithi zote nzuri, zinafurahisha... lakini Muungano wa nchi mbili mnaushusha hadhi na kuufananisha na viroja katika jamii yetu huku mitaani?

  Kuna wengine wanazungumzia Muungano kama mke na mume na talaka!!!

  Ndio sababu watawala nao pia wanaendelea kufanya usanii linapokuja suala la muungano. Inabidi tuwe serious kidogo.

  Sasa niulize hivi: Huyu ng'ombe anapenda kung'ang'aniwa? Anajisikia raha kung'ang'aniwa na kupe? Kama jibu ni hapana , kwa nini ng'ombe hachukui hatua dhidi ya huku kung'ang'aniwa?

  Pia huyu mjomba anapata nini kutoka kwa shangazi kiasi aendelee kuwa pamoja na huyu shangazi?
  Au mjomba anapenda kupata mnyanyaso na matusi? Au mjomba huwa saa zote amelewa,hajitambui na hivyo haelewi anachokifanya au kufanyiwa?

  Kuna nchi ziliungana, Malaysia na Singapore. Walipoona muungano ni kuzinguana tu, walivunja muungano huo. Leo Malaysia na Singapore zote ni nchi zenye neema na zinazoheshimiana. Na kila moja inajiendesha kivyake.

  Zilinganishe nchi hizo kiuchumi,idadi ya watu,eneo na hatua waliyopiga kimaendeleo leo. Tuache kufanya mambo kiutani utani.

  Links. 1. http://en.wikipedia.org/wiki/Singapore_in_Malaysia

  Link 2. http://en.wikipedia.org/wiki/Singapore

  Link 3. http://en.wikipedia.org/wiki/Malaysia

  Link 4. http://dinmerican.wordpress.com/2010/09/25/malaysia-singapore-relations-putting-the-past-behind-and-moving-forward/

  Link 5. http://www.bloomberg.com/news/2010-11-10/singapore-seen-overtaking-malaysia-45-years-after-split-left-lee-in-tears.html
   
 14. T

  Tata JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Watanganyika tunajidanganya kudhani kuwa Zanzibar itakufa au kuathirika ikiondoka kwenye Muungano. Kuna nchi ndogo zaidi ya Zanzibar zinavyojiendesha kwa uhuru na zimepiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi na wananchi wake wana maisha mazuri kuliko haya maisha ya kimaskini ambayo yapo ndani ya hiki kinachoitwa Muungano. Kimsingi Zanzibar inaweza kabisa kuwa na maendeleo makubwa zaidi iwapo itaondoka kwenye muungano.

  Tatizo ninaloliona hasa kwa kuwasikiliza kwa makini wazanzibari (ukiondoa wana unamsho) ni kuwa hawaongelei kuuvunja muungano ila mara utawasikia wanazungumzia muungano wa serikali tatu, mara wa mkataba yaani kwa ufupi wanataka muungano uendelee ila kwa muundo tofauti na huu uliopo.
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ushaona mbara yuko zenji anawekeza.. Wapemba kibao wako bara wana majumba ya kupangisha mahoteli maduka vituo
  vya mafuta... Sasa niambieni nani anafaidi hapo.. Sie wabara ndio tunaonyonywa lakini cha ajabu wazenji ndio walalamikaji hata siwaelewi
   
 16. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Wote tuna madudu yamejaa tele, yanatusumbua sana kiasi kwamba, hatujui tufanye nini. Sisi huku Bara tunajua mbaya wetu ni ,
  Serikali kichaa ya CCM Huko visiwani mbaya wao ni Bara, Kwetu bara Zanzibar si tatizo hata kidogo.

  Muungano ukivunjika leo, tutakacho miss kutoka Zanzibar, ni maembe tu. Kupata maendeleo ya Singapore, inawezekana lakini si kwa kujiunga OIC, Waziri mkuu wa Singapore kwanza kabisa, aliwatia adabu Wasingapore na kuondoa, Udini,Ukabila na makundi yote ya kiimani, Kisha akaweka sheria kali kuzuia mtu yeyote, kutumia vigezo vya dini, rangi na historia yake, kuleta madai ya aina yeyote ile.
  Utawla wake ulikuwa wa Chuma wenye, mlengo wa kimagharibi, japo yeye ni Mchina.

  Cha mwisho na kikubwa, aliruhusu Mabepali kuja kuwekeza, Kampuni ya kwanza kuwekeza Singapore, Tax Free ilikuwa Texas Instrument, wale watengeza Calculator maarufu duniani Mabepari wengi ni wala nguruwe, Pia, alipiga marufuku aina yeyote,
  ya Umalaya, ukahaba na uasherati, hata kuwa mssenge tu ni kosa la, kukuweka jela Singapore.

  Naijua Zanzibar ilivyo maisha yake ya kila siku, utamaduni wake mazoea na vitabia, hayo niliyoyasema, yawezekana lakini ni ngumu sana, kuyatekeleza hasa ukizingatia hali, ya udini na msimamo mkalia, wa kupinga mawazo mengi ya kimagharibi. Dubai nao wamelegeza msimamo wao, naamii hata uislamu umewekwa pembenikidogo,

  Mara 4 nimepanda ndege yao, ya Emirates nakula Baken kama kawa, nakuywa ulabu Bia na wine mpaka, nakaribia kupendeza,
  hakuna uislamu mle ndani ya ndege, ni maisha kama huku Ughaibhuni.

  Mko tayari kumeza hizo taka?
  Au mtaishia kuwa kama Yemen?
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Mbona unaungumza kama mjomba? ushakunywa ulabu?

  Halafu unaungumza na nani? mta...mta!!
  Mkuu usijifanye kama "sheikh Yahya"....ndio nikasema tuache utani utani.
  Unasema inawezekana kupata maendeleo ,lakini.....

  Halafu unasema unaijua vyema Zanzibar, kazi yao kula urojo tu, au vipi?
  Nililolisema au nnalotaka lionekane ni kuwa ngo'mbe au mjomba anaweza kumfukuza kupe/ shangazi kama Malysia alivyofanya kwa Singapore.

  Wachangiaji wengi ambao tunahisi ng'ombe ananyonywa damu, tunaishia kusema wajikate, waitishe kura ya kujitoa. Jambo ambalo tunalikimbia kuliona ni kuwa ipo option ya kuwafukuza pia. Tuitumie hii kama tumewachoka wala urojo.
   
Loading...