WATANGANYIKA na kura ya maoni..Je ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WATANGANYIKA na kura ya maoni..Je ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Apr 15, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Je WaTanganyika mnasemaje kwa hili la serikali tatu ya TANGANYIKA ya ZANZIBAR na ya shirikisho au MUUNGANO ???
  Tayari mabango yameanza kutawala maandamano yanayofanyika Zanzibar wakidai iletwe kura ya maoni kuulizwa wananchi kama wanataka muungano au wanataka serikali tatu na hapa Tanganyika Mtikila amesikika na kusema mpaka anatoka kipovu akijaribu kuitilia nguvu hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika ambayo Nyerere aliizima inasemekana katika makubaliano ya Muungano hakuna kipengee kinachoonyesha kuzimwa kwa Tanganyika au Zanzibar ,hivyo katika hizo articles za Muungano hapajaonekana kufutwa kwa Serikali ya Tanganyika .
  Maoni yenu katika hili baada ya kuona hayo makubaliano nini kifanyike ili kuihuisha serikali iliyofunikwa wakati ipo ?? Je mafisadi nao watakuwa tayari kuikubali kuzinduliwa kwa Serikali ya Tanganyika kwani inaonekana wanajificha katika serikali ya Muungano ambayo haina dira ni wizi mtupu.
   
Loading...