Watambue Wasanii wa Bongo Fleva waliopiga kelele hadharani kupinga Roma Mkatoliki Kutekwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,275
2,000
Profesa J na Ney wa Mitego walijitokeza hadharani kuonyesha masikitiko yao na kupinga Roma Mkatoliki Kutekwa Yeye na watu wengine pale Studio, na walipaza sauti zao ili arejeshwe akiwa hai.

Jambo hili lilimfanya aliyekuwa RC wa Dar es Salaam Paulo Makonda kutangaza kwamba Roma atarudishwa kabla ya Jumapili, kauli hii iliwashtua wengi wasijue atarudije na atarudi kutoka wapi, ni kweli kabla ya Jumapili ile Roma akatupwa na kuokotwa na watu wema.

Hoja yangu kwa leo siyo hii, bali ninataka kujua Wasanii wengine wa Tanzania waliopiga kelele na kupinga msanii mwenzao ambaye si Mwanasiasa Roma kutekwa na kutaka aachiwe huru.

Unaweza kuweka majina ya wasanii hao hapa ili tuwatambue

FB_IMG_1622734620152.jpg

 

maddox

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
389
1,000
Haya tuhitimishe kwamba alitekwa na wanasiasa........yaani hapo kwa ufupi ni kwamba mchuma janga hula na ..........malizia..............unataka Vita ya mawe kwenye nyumba ya vioo
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,275
2,000
Haya tuhitimishe kwamba alitekwa na wanasiasa........yaani hapo Kwa ufupi ni kwamba mchuma janga hula na ..........malizia..............unataka Vita ya mawe kwenye nyumba ya vioo
Hoja yangu si hii unayotaka kunipeleka , lengo ni kuwajua wasanii waliopinga Roma kutekwa kama kichwa cha habari kinavyojieleza
 

maddox

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
389
1,000
Hoja yangu si hii unayotaka kunipeleka , lengo ni kuwajua wasanii waliopinga Roma kutekwa kama kichwa cha habari kinavyojieleza
Du.......unaeza kuta huyu ni mbaba na familia badala ajikite kutafuta ugali Yuko busy na tigo extreme yake kujua wasanii waliopinga kutekwa Kwa Roma........kuwa mwanaume kazi kweli kweli naona vivulana vinaleta balehe hapa jf
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,874
2,000
Tumpigieni kura Roma na net kwenye tuzo za BET,

Afu Ney ana matusi jamaal Daah afu ndo msanii wa CHADEMA
 

Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
311
500
Hoja yangu si hii unayotaka kunipeleka , lengo ni kuwajua wasanii waliopinga Roma kutekwa kama kichwa cha habari kinavyojieleza
Nyinyi mbona hamkupinga ,Au unamaanisha zile #hashtags zenu?

Hakuna namna ambayo naweza mshauri mtu anaejenga future yake kusimama na upinzani katika nchi kama hii (Tanzania),wao wanataka ujitoe hadharani kupinga ila unapokamatwa hawatoki hadharani kukusaidia,badala yake wakakimbilia mitandaoni kuweka hashtags. Zile hashtags za #Freemdude zilimsaidia nini kijana wawatu aliejiingiza kwenye siasa bila kuwa nguvu yoyote?Familia yake mnaijali kwa lolote?

Watu ambao ni waoga hata ukisema ukalianzishe hawakupi support badala yake wanarudi nyuma.

Kwa tz hii kama una kitu cha kupoteza,ni bora usimame na watawala tu ili mambo yako yanyooke, Watz hawana shukrani, leo utasema usimame kuwatete ila career yako ikiharibiwa kwa urasimu wa Serikali watkucheka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom