Watambue Wachezaji wa Taifa Stars waliowazawadia Magoli mazuri Matatu Congo DR leo pale kwa Mkapa Temeke Dar es Salaam Tanzania

Kabla ya yote nianze kwa Kusema kuwa Mimi ni Shabiki Kindakindaki wa Simba SC ila katka Uzi huu naweka Ushabiki wangu huo pembeni na nasema Ukweli mtupu ambao najua utawaumiza baadhi au hata wengi hapa

Goli la Kwanza

Aliyechomesha ni Kipa Aishi Manula

Maoni yangu ni kwamba kwa sasa apumzishwe na Wadake wengine kama Metacha Mnata kwa Taifa Stars na kule Simba SC awe anadaka Beno Kakolanya.

Goli la Pili

Aliyechomesha ni Beki Shomary Kapombe

Maoni yangu sasa ifike muda kuanzia Taifa Stars hadi Simba SC huyu Beki apumzishwe au aachwe na awe anaanza ama Israeli Mwenda au Kibwana Shomary.

Goli la Tatu

Waliochomesha ni Mabeki Dickson Job na Bakari Mwamnyeto

Maoni yangu ni kwamba ikiwwzekana Dickson Job awe anacheza namba za pembeni kwani Ufupi wake unatoa Faida Kubwa kwa Washambuliaji Warefu na Mahiri.

Beki Bakari Mwamnyeto afundishwe kutokupenda kutumia sana Nguvu bila Akili mara kwa mara kwani Mapungufu yake haya huwa yanamgharimu na Kuzigharimu pia Timu zake anazozichezea.

Tafadhali Maoni yangu yaheshimiwe!!
nawe kumbe ni tango pori. Unaongea utafikiri ww pekee ndiyo uliangalia ile mechi. Au umesimuliwa nawe ukaja kuhemka humu.

Kumbafu!
 
Back
Top Bottom