Watambue Wachezaji wa Taifa Stars waliowazawadia Magoli mazuri Matatu Congo DR leo pale kwa Mkapa Temeke Dar es Salaam Tanzania

Galileo_Gaucho

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,878
2,000
Goli la kwanza Mtoa pasi jinga kabisa he had a chance his partner kapombe mbali mno na half of our players walivuka nusu yetu, goli la pili ni jumuishi kimakosa pembeni na ndani ya sita marking ya opponents, la tatu ni jumuishi pia na bad luck kipa hakujua ana bekivwafupi na opponents warefu hivo kila set piece alioaswa alenga kucheza ndani ya sita si kwenye goal line.

Tumepigwa siku ambayo mpinzani hajaupiga mwingi bali katumia nafasi na akili kubwa ya mpira kuliko papara.

Hongera DRC ushindi laini kwao kuliko mechi zote zao za awali.

Tumeingia na kujiamini na kwa plan ya kushinda, kuwa tunaweza, bila heshima na kujua umuhimu wa draw kwetu na uwezekano wa kufuzu.

Wapi Etiene!!!!
 

Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
974
1,000
Nikaa kwenye vijiwe vyetu vya kahawa utasikia u Simba na uyanga ooh Feisal toto sio wa kiwango cha nchi hii. Mara utasikia manula ilibidi akawe kipa wa timu kubwa kama mamelodi. Tuajiri wataalamu wa soka kuibua vipaji vya soka
 

Bukali

JF-Expert Member
May 7, 2018
1,124
2,000
Acha uongo goli la kwanza ni Dickson Job alipiga pasi ambayo haikumfikia kapombe na kuwahiwa na mchezaji wa Congo aliyekokota mpira na kutoa pasi kwa Mbokani aliyemuona mfungaji wa bao musuaku na kumpa pasi nzuri aliyetupia mpira kambani.
Elewa,kipindi anatoa pasi, golie alikuwa golini alitakiwa kufanya kazi yake.
 

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,588
2,000
Goli la kwanza kachomesha Dickson Job baada ya pasi yake aliyolenga kumpasia Kapombe kuwa intercepted na wachezaji wa Congo
Kweli kabisa. Hakuwa na sababu ya kulazimisha pasi ndefu wakati kuna mchezaji mwingine alikuwepo karibu ambae angeweza kupeleka mpira kwa Kapombe.
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
3,101
2,000
Elewa,kipindi anatoa pasi, golie alikuwa golini alitakiwa kufanya kazi yake.
Nielewe mara ngapi hakuna goli la kipa hata moja yote ni uzembe wa mabeki hawakufanya majukumu yao ipasavyo....Job alipiga pasi isiyokuwa na nguvu lakini lengo lake halikuwa baya maana alikuwa anaanzisha mashambulizi kwenda mbele bahati mbaya mpira haukufika ukawahiwa na mchezaji wa Congo...hakuna lawama tena Manula kajitahidi sana....yaani wewe ndio ungekuwa golikipa ungefanyaje ili kuzuia goli?
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
3,101
2,000
Sasa inahusiana vipi na mechi ya Stars v DRC? Kuna haja ya kuweka viwango vya elimu mtu kuwa member wa JF
Utakuwa umetunyima haki sisi tusiokuwa na elimu lakini tuna busara na akili mkuu...huyu unaweza kuta ana elimu kubwa kukuzidi!!!
 

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
9,262
2,000
Pamoja na hao, Mbwana Samatta ifike mda sasa kama taifa tuache kumuonea haya kumuweka bench, hamna kitu pale.
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
3,101
2,000
Acha uongo ,pasi ya Dick Job ilikuwa murua kabisa,kosa Ni la Kapombe aliyesimama akisubiri mpira umfuate badala ya kuufuata yeye.
Huwezi kupiga pasi kitoto haina nguvu ya kuishia njiani halafu wapinzani wako ni wenye uwezo wa hali ya juu,kama wewe na mchezaji wako mlifikiri pasi huwa zinapigwa hivyo, poleni na kama hujawahi gusa gusa soka basi huwezi kuelewa,makocha huwa wana train wachezaji kupiga pasi zenye kufika mahali panapo kusudiwa na sio kuishia njiani na kutegemea uliyempigia ndio aifuate kijana.....wale sio Ruvu shooting au coastal mzee wale ni professional players wanatuzidi kila kitu.
 

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
4,313
2,000
Tz kila mtu mpenda soka ninkocha wa leseni D ya TFF, nimecheka pale TBC 1 kuna jamaa ni mposhi ktknile studio yao mle ktk kipindi cha jambo Tz, eti yule mpishi akaanza kuichambua Starz 😆😆😆😆
 

Bukali

JF-Expert Member
May 7, 2018
1,124
2,000
Nielewe mara ngapi hakuna goli la kipa hata moja yote ni uzembe wa mabeki hawakufanya majukumu yao ipasavyo....Job alipiga pasi isiyokuwa na nguvu lakini lengo lake halikuwa baya maana alikuwa anaanzisha mashambulizi kwenda mbele bahati mbaya mpira haukufika ukawahiwa na mchezaji wa Congo...hakuna lawama tena Manula kajitahidi sana....yaani wewe ndio ungekuwa golikipa ungefanyaje ili kuzuia goli?
Kudaka,sasa utafanya nini zaidi ya hapo mkuu.
 

Nyonzo bin mvule

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
1,063
2,000
Manula apumzishwe,,
Kapombe apumzishwe,,
Ila mwamnyeto na job wapewe maelekezo 🤣
Mleta uzi una vichembechembe vya utopolo sio bure
 

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
6,326
2,000
Tanzania kila mtu ni mtaalamu wa kila kitu kulingana na mazingira aliyopo.....
yaan huko kwe professional zao ni failure ila kazi ni kujadili kukosoa watu wa mpira na kuwaona hamna kitu, tupo nyuma kwe kila kitu ila tunaamini tunastahili kufanikiwa kwe mpira sema tu wahusika wanazingua, mtangazaji busy kulaumu wachezaji wetu hawajitumi ili waonwe na timu za ulaya wakati ye mwenyew yupo redio matonya hajajitahidi aende BBC
 

Msudu

JF-Expert Member
Aug 19, 2021
428
1,000
Kabla ya yote nianze kwa Kusema kuwa Mimi ni Shabiki Kindakindaki wa Simba SC ila katka Uzi huu naweka Ushabiki wangu huo pembeni na nasema Ukweli mtupu ambao najua utawaumiza baadhi au hata wengi hapa

Goli la Kwanza

Aliyechomesha ni Kipa Aishi Manula

Maoni yangu ni kwamba kwa sasa apumzishwe na Wadake wengine kama Metacha Mnata kwa Taifa Stars na kule Simba SC awe anadaka Beno Kakolanya.

Goli la Pili

Aliyechomesha ni Beki Shomary Kapombe

Maoni yangu sasa ifike muda kuanzia Taifa Stars hadi Simba SC huyu Beki apumzishwe au aachwe na awe anaanza ama Israeli Mwenda au Kibwana Shomary.

Goli la Tatu

Waliochomesha ni Mabeki Dickson Job na Bakari Mwamnyeto

Maoni yangu ni kwamba ikiwwzekana Dickson Job awe anacheza namba za pembeni kwani Ufupi wake unatoa Faida Kubwa kwa Washambuliaji Warefu na Mahiri.

Beki Bakari Mwamnyeto afundishwe kutokupenda kutumia sana Nguvu bila Akili mara kwa mara kwani Mapungufu yake haya huwa yanamgharimu na Kuzigharimu pia Timu zake anazozichezea.

Tafadhali Maoni yangu yaheshimiwe!!
Nakubaliana na wewe japo sikubaliani na wewe Hahahaha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom