Watalii wa kizungu wanazurura hivyo hovyo Kariakoo, kuna vivutio gani hapo?

Jumapili ni siku tulivu sana kwa Kariakoo, lakini nimepita mitaa kadha wa kadha katika mizunguko yangu hapo Kariakoo na kukuta makundi kwa makundi ya wazungu wanao onekana kuwa ni watalii wakizurura hovyo hovyo bila guide wala utaratibu maalum, twiga wamehamia huko nn? Whats going on?
Its a very important observation mkuu. You are making a point very few people would understand

I hope TISS wanafuatilia hili kwa umakini. Binafsi siwaamini hawa jamaa hata kidogo. Sehemu nyingi zenye matatizo ya kiusalama hutanguliwa kwanza na uwepo wa wazungu wakiwa kama watalii wasio kua na mipaka wala uratibu
 
Nasikitikika sana kwa mada uliyoileta
Lakini si kosa lako. Maana utalii ni Taaluma. Lakini wewe upo kwenye box kwamba utalii ni kuangalia wanyama na natural features

Utalii unaenda Far sana. Hata ukigoogle types/ Forms of tourism

Utaona kuna utalii wa Biashara, utalii wa matibabu, utalii wa elimu, utalii wa Michezo, utalii wa utamaduni, utalii wa wanyama Nk.

Kama umewaona kko ishia kuwaona tuu. Maana utalii una Motives zake. So ww hujui huyo mtalii amekuja kuangalia nini.

Hata wewe ukiumwa ukienda Apolo india kutibiwa wewe ni mtalii wa matibabu. Kama ukienda Uk kucheki game ya Man U, wewe ni mtalii wa Michezo.

Asante kama umenielewa.....!
 
Its very important observation mkuu. You are making a point very few people would understand

I hope TISS wanafuatilia hili kwa umakini. Binafsi siwaamini hawa jamaa hata kidogo. Sehemu nyingi zenye matatizo ya kiusalama hutanguliwa kwanza na uwepo wa wazungu wakiwa kama watalii wasio kua na mipaka wala uratibu
mkuu ukiwakuta utawatimua au
 
Hiyo ni aina ya utalii maarufu Amerika kusini hasa Brazil kwenye "Favela" ambayo ni makazi yanayofanana na Manzese uwanja wa fisi, Katika eneo letu la Africa Mashariki watalii wa aina hiyo wako zaidi Mombasa na kidogo Zanzibar. Dar es salaam haijatangazwa sana, huwa wanapita tu kwenda Zanzibar... Inawezekana mambo yamebadilika.
 
Jumapili ni siku tulivu sana kwa Kariakoo, lakini nimepita mitaa kadha wa kadha katika mizunguko yangu hapo Kariakoo na kukuta makundi kwa makundi ya wazungu wanao onekana kuwa ni watalii wakizurura hovyo hovyo bila guide wala utaratibu maalum, twiga wamehamia huko nn? Whats going on?
kariakoo Business Centre ambayo pia Ni kivutio kwa mgeni yeyote yule kuona jinsi solo kubwa kuliko yote mashariki na Kusini mwa Africa linavyofanya kazi

Kuna utalii wa aina nyingi Sana
1.Utalii wa Wanyama Pori
2.Utalii wa Milima
3.Utalii wa Uoto wa asili
4.Utalii wa ngono
5.Utalii wa Biashara
6.Utalii wa Kilimo
7.Utalii wa Viwanda
8....
9....
10....

Kwa kifupi Kila kinachovutia Ni utalii.Kitu Cha maana n kuingiza pesa kwa watu kuja kuon kinachowavutia
 
mkuu ukiwakuta utawatimua au
Hapana mkuu huwezi kuwatimua bila ushahidi. Ninachosemea ni muhimu kuchukua tahadhar za kiusalama hasa kwa vyombo vyetu vyenye dhamana hiyo

Maranyingi nchi zetu za kiafrika tunajisahau sana na kuwaamini watalii wote wa kizungu tukidhani wote wamekuja kutalii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom