Watalii 450 wa Israel watembelea Tanzania

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1577350619381.png


WATALII zaidi ya 450 kutoka Israel, wamewasili nchini mwezi huu kwa ajili ya kutembelea vivutio vya kitalii vilivyoko Kaskazini mwa Tanzania.

Watalii hao wamekuja nchini kwa kutumia ndege binafsi na za kawaida. Kundi la kwanza la watalii 150 liliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Desemba 21, na kupokelewa na Bodi ya Utalii (TTB) na baadaye kuelekea katika vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kundi la pili na la tatu lililokuwa na watalii 305 limewasili nchini kupitia KIA, juzi Desemba 24, mwaka huu.

Watalii hao wako nchini kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, na wanatembelea Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire, Ziwa Manyara, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la Eyasi.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Israel, umetoa viza zaidi ya 500 kwa Waisraeli ambao wamepanga kuwasili nchini kwa kutumia mashirika ya ndege ya Ethiopia, Uturuki na Uswisi katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka huku.

Ubalozi huo unaendelea kuratibu ziara nyingine ya watalii zaidi ya 800, ambao mchakato wa safari yao upo katika hatua za mwisho.

“Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuvutia watalii zinazofanywa na Ofisi ya Ubalozi nchini Israel kwa kushirikiana na makampuni ya wakala wa utalii ya ndani na nje ya nchi ili kuunga mkono harakati za serikali za kukuza Pato la Taifa kupitia utalii na hivyo kuiletea nchi maendeleo,” ilisema taarifa hiyo ya wizara
 
Back
Top Bottom