Tanzania ya pili duniani kwa vivutio asilia vya utalii, tulikwama wapi?

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,983
4,080

Kila mwaka duniani kuna wastani wa watalii 1.5 bilioni wanatafuta ni wapi waende kutali au kula bata ||​

||Sisi Tanzania ni nchi ya Pili kwa vivutio vingi vya asili duniani lakini tunaambulia watalii chini ya 2m kwa mwaka hapa kunajuhudi zinahitajika Sehemu,​

===
Niseme kidogo kuhusu Rais Samia na " Royal Tour. " Tanzania ni nchi ya Pili kwa Vivutio vya asili duniani baada ya Brazili.

Tofauti na nchi zingine 80% ya Watali wote wanaozuru Vivutio vya Brazili ni Wabrazili,Ni watali 6.5m tu ndio wanatoka nje ya Brazili kwa mwaka.

Mwaka 2018|19 Brazili ilijikusanyia kiasi cha US$97.11BL karibu TZS 215 trilioni kama mapato yatokanayo na Utalii.

Kwamsiofahamu fedha hii inaweza gharamia bajeti ya Serikali ya JMT kwa miaka 5 mfululizo bila Mtanzania yeyote kutozwa kodi|tozo hapa namaanisha hadi Vyoo vya kulipia viwe bure.

Je, tumewahi kujiuliza kwanini hawa Brazili wakusanye Tshs 215trilioni kwa mwaka na Sisi tukusanye Tshs 5.3trilioni kwa mwaka sawa na tofauti ya Tshs 210trilioni ili hali Sisi ni Wapili baada ya wao kwa kuwa na Vivutio vingi vya asili duniani, Yaani Kwanini Wao!!?

Rais Samia Suluhu amekuja na jibu ambalo ni "Royal Tour Film " na hapa lazima tutambue Tanzania Kiutali haifahamiki kabisa duniani huenda heri ya Bongo Zozo.

Leo kwa mwaka Tanzania inapokea watali chini ya 2m pamoja na utitiri wa Vivutio ilivyonavyo, Chaajabu Ufaransa inayoongoza kwa Utali duniani haina twiga wala Simba inamagofu na Minara ( all are man-made ) lakini inaingiza zaidi ya watali 89m na €56.2BL kwa mwaka sawa na Tshs 154trilioni,

Tujiulize, kwa vivutio tulivyonavyo nikweli tumeshindwa kuinyanga'nya hata Watali 5m tu kwa mwaka waje Tanzania!? Lazima tufahamu duniani kwa Sasa Utali ni biashara kipaumbele na msitegemee nchi yeyote duniani kutangaza vivutio vyenu zaidi ya Sisi wenyewe kwa Platform hizi za " Royal Tour Film. "

Tatizo la Uhaba wa watali Tanzania sio tu Corona hata "Ushawishi " pia uko chini, Kwaakili ya kawaida ni ngumu zaidi kwa Mtali anayefahamu "Nini Kipo Tanzania " aache kuja kumtazama nyumbu|tembo "Live " pale Serengeti aende kumtazama tembo wa kwenye michoro kule Versailles Ufaransa,

Siku Mungu akitupa walau watali 5m tu kwa mwaka nchi yetu itaingiza zaidi Tshs 10trilioni kama mapato yatokanayo na Utali,

Pesa hii itakwenda moja kwa moja kwa wanachi kwa njia ya kuwahudumia Watali na serikali itapata kiasi kama tozo ya Utali,

Nchi hii inaweza kuendeshwa kwa Utali tu kama tu dunia itafahamu "Nini Kipo Tanzania. " Zaidi ya 50% ya watali wanaofika Kenya kwa Utali kwa mwaka wamevutiwa na Vivutio vilivyopo Tanzania, inauma Sana na lazima tumshukuru Rais Samia kwaajili ya "Royal Tour Film "

Mfano, Mwaka 2017|18 mapato yetu yatokanayo na Utali yalifikia $2.4BL sawa na Tshs 5.5trilioni wakati rekodi ya Watali ikiwa 2m,

Lakini tunafahamu duniani kila mwaka kuna zaidi ya Watali 1.5bl wanatafuta wapi waende kula bata, Sisi Tanzania pamoja na kuwa Wapili kwa Vivutio tena vya asili duniani tunaambulia watali 2m tu,

Nadhani kunasehemu tulikwama na ndio Sababu ya Mungu kumleta Rais Samia na yeye kutuletea "Royal Tour Film. "Mnaolalamikia gharama za Tour rudieni kusoma andiko hili kwa makini,

IMG-20210919-WA0025.jpg
VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA
 
Wanasiasa wa Tanzania siwaamini kabisa.

Baada ya gas kugundulika huko kusini, Kikwete alituambia mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gas ikikamilika umeme ungeshuka bei..mpaka leo tunasubiri.

Huyu mama naye ni wale wale tu.
 
Huduma zetu ni mbovu...

Wakaribishaji wetu (Port of Entry) ni wabovu, wana lugha chafu, hawajali, wapenda kitu kidogo

Polisi wetu huwasumbua sana Tour Operators....
Are your sure watu wanavifahamu vivutio vilivyopo Tanzania?

Polisi kumsumbua Tour Operator kuna mzuiaje mtali kurudi tena,

Kuhusu fukwe yes but sio wote wanakuja kuogelea,

Tatizo knowledge haipo huko Duniani,
Anachokifanya Rais Samia ndio hasa kinahitaji kwa dunia ya leo,

Tumuunge mkono mama,
 
Are your sure watu wanavifahamu vivutio vilivyopo Tanzania?

Polisi kumsumbua Tour Operator kuna mzuiaje mtali kurudi tena...
Hivi unadhani Watalii wanapenda kila baada ya km 10 polisi wanawasimamisha na kuomba rushwa?

Hivi nani asiyeijua Serengeti dunia hii?

Au unadhani huko duniani hakuna mawakala wanaotafuta watalii kuja huku tz?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba tu inatushinda hadi tunatiana jela, hili la kuvutia watalii ndio tutaliweza?

Nchi watu hatupendani tumekuwa kama kijii cha wachawi.

Mungu wa bariki Tanzania.
Tanzania inahitaji toba ili kurudisha upendo na mshikamano aliutuachia Mwalimu.
 
Katiba tu inatushinda hadi tunatiana jela, hili la kuvutia watalii ndio tutaliweza?

Nchi watu hatupendani tumekuwa kama kijii cha wachawi.

Mungu wa bariki Tanzania.
Tanzania inahitaji toba ili kurudisha upendo na mshikamano aliutuachia Mwalimu.
Katiba inahusiana nini na Utali?
 
Shida Tanzania ni bei ghali ya kutalii.

Nilienda Zanzibar juzi kati hapa kihoteli cha ajabu kabisa gharama 100k.

Tanzania gharama za utalii ziko juu sana.
Kweli kabisa gharama ni kubwa sana ukilinganisha na ubora wa huduma zitolewazo kwenye mahoteli, migahawa na vyombo vya usafiri. Vile vile miundo mbinu ya kufikia hivyo kivutio ni chemsha bongo. Kwa mfano, kutoka ngorongoro na kupitia serengeti hadi musoma barabara ya changarawe na vumbi siyo kivutio kwa mtalii. Na kutoka Dar utafikaje Selous.

Siyo kila mtalii anaweza kukodi ndege ndogo. Hiyo ni baadhi ya mifano. Pamoja na royal tour hakuna njia ya mkato zaidi ya kuboresha miundombinu yetu, huduma za mahoteli, wafanyakazi wa huduma hizo wenye juzi na weledi mkubwa. Tumeona njia na tumuunge mkono Rais wetu. Isipopatikana tija ni mama Tanzania atakayekwama siyo Rais.
 
Mtoa mada umejitahidi sana kuandika, 😁.
Ila unasahau siasa zetu za Afrika jinsi zinavyoharibu utendaji wa serikali moja kwa moja.

Hata ukijipiga picha ukiwa na kisima cha mafuta hapa Tanzania angalia jinsi wanasiasa watakavyokugasi kuomba kupiga picha na wewe, get answer!.

As citizens hatuna morals kuitangaza nchi yetu kifua mbele sababu hutu uliotakiwa kuanzia juu (leaders) haupo.
Hii ndiyo chanzo mtu anaona 'bora twende tu' sababu wanaofaidi tunu ya taifa wanahesabika kuliko wanaotakiwa kupambania tunu ipatikane.

Fikilia mzee makamba ameshastasfu, how and for what purpose kijana wake lazima awe kiongozi?.
☝🏾
Is one of foolish inayovunja watu mioyo.
 
Daaah

kwa Uchambuzi huu nimemwelewa Mama,

Kumbe Watali wapo wengi sana shida nani wa kuwaita waje ndio shida,

Naendelea kusema huyu mama ataipaisha hii nchi kiuchumi kirahisi sana,
 
Utali ni zaidi ya madini aise, Tanzania tunakila kitu,
Royal Tour naamini itaifungua nchi kiutali, Watali waje tupige pesa
 
Na sasa hivi wanatuambia bwawa la mwl. Nyerere likiisha..umeme utashuka bei..

Believe me brothernakwambia.. Bwawa hilo likiisha.. Umeme ndio utapanda bei..

Watakwambia nchi imeingia hasara kubwa.. Kwa hyo inabidi tulipe ili tufidie ...
Wanasiasa wa Tanzania siwaamini kabisa.

Baada ya gas kugundulika huko kusini, Kikwete alituambia mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gas ikikamilika umeme ungeshuka bei..mpaka leo tunasubiri.

Huyu mama naye ni wale wale tu.
 
Rekebisha hapo,

Tanzania ni nchi ya pili kwa vivutio vya asili duniani,

Hii ni somo la uraia darasa la Tatu,
Alie kuambia watalii wanataka kuangakia tu vivutio vya asili ni nani? Hispania ni moja kati ya nchi zinazo pokea watalii wengi mno Duniani nazani ni Million 30+ ila je kuna vivutip ya asili huko Hispania? France kote huko, Malaysia, Singapole na kwingineko
 
Back
Top Bottom