Watalam wa umeme msaada katika hili

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
408
1,032
Naomba kuuliza: Unaweza kutumia mfumo wa sora ya wat 100 kwenye nyumba ambayo imekonekitiwa na njia zilezile za umeme? Maana sehemu nilipo umeme bado hauja fika nimenunua solar.

Naomba kufahamu hilo nilihitaji njia za umeme ndio nzitumie kama zilivyo kwa kutumia umeme huu wa solar.

Kama una majibu nisaidie kunipa uelewa na elimu kuhusu masuala haya kwa ujumla.
 
Nadhani si vizuri kuchanganya mifumo; kwa uzoefu wangu ambao pia nimeutekeleza kwangu, mfumo wa sola unajitegemea na mfumo wa umeme pia unajitegemea; ni vizuri mbuzi wakawa kwenye zizi lao, na ng'ombe pia wawe kwenye zizi lao, kuwachanganya ng'ombe na mbuzi kwenye zizi moja ni kusababisha maafa kama yatatokea.
 
Naomba kuuliza: Unaweza kutumia mfumo wa sora ya wat 100 kwenye nyumba ambayo imekonekitiwa na njia zilezile za umeme? Maana sehemu nilipo umeme bado hauja fika nimenunua solar.

Naomba kufahamu hilo nilihitaji njia za umeme ndio nzitumie kama zilivyo kwa kutumia umeme huu wa solar.

Kama una majibu nisaidie kunipa uelewa na elimu kuhusu masuala haya kwa ujumla.
Kama unatumia kifaa cha kubadili mkondo (DC to AC) ni sawa lakini kama unatumia DC only ni vizuri kuwa na mfumo wake.
 
Njia hii apa Samahani sio muandishi mzuri ila muhimu kuelewa Tuanze na muongozo

Kwanza unaweza ukatumia umeme wa Solar kama unakifaa ( inverter) cha kubadilisha uwo umeme wa DC kwnda AC na ukakonect na Waya za umeme wa kawaida ata siku ikitokea umewekewa umeme aitakuwa shidah mbk kubadilisha tena system
Ila km umeme uwo wa Solar auna kifaa cha kubadilisha kupeleka AC ni vizuri ukatengenezea system yake Mpya ya wiringi
 
Nenda kwenye distribution board (mafundi wanapenda kuita main panel). kisha chomoa waya zinazoingiza power kutoka tanesco. Kisha chomeka waya za bettry, positive kwnye red/brown na negative kwnye blue, green usiitumie (funga tape kabisa).

Alafu chomoa taa zako zote kisha weka taa za DC (ambazo mara nyingi huwaga 1watt).
mpaka hapo mfumo umekamilika.

LAMUHIMU: Hizo socket usizitumie wala usije ukajichanganya kwa hilo.

tanesco wakiweka umeme unarudi kwnye main panel tena unachomoa za bettry tena unachomeka za tanesco. Sasa unaweza ukaendelea na matumizi ya kawaida.
 
Naomba kuuliza: Unaweza kutumia mfumo wa sora ya wat 100 kwenye nyumba ambayo imekonekitiwa na njia zilezile za umeme? Maana sehemu nilipo umeme bado hauja fika nimenunua solar.

Naomba kufahamu hilo nilihitaji njia za umeme ndio nzitumie kama zilivyo kwa kutumia umeme huu wa solar.

Kama una majibu nisaidie kunipa uelewa na elimu kuhusu masuala haya kwa ujumla.
Mimi nimefunga solar na umeme katika njia moja japo kwenye tv peke yake kwa kuwa solar yangu ni ndogo ku supply nyumba nzima. Unakiwa kuwa na vitu vifuatavyo:-
1. Inverter- kubadili DC to AC
2. Exchange switch- hiki ni kifaa cha kutenganisha umeme wa tanesco na wa kutoka kwenye inverter, unaweza nunua dukani au ukatengeneza kutoka "two way- two gang switch ikafanya kazi sawa na exchange switch
Namna ya kufunga:
1.Funga exchange switch kwenye 6mm just before main board
2.Common peleka kwenye main board
3. Funga Line 1 let's say tanesco kisha Line 2 from inverter (solar)
4. Ukitaka badili kwenda solar, washa inverter kisha switch line 2. Leta mrejesho ukikwama niulize

Nikipata muda nitaelezea kwa picha na clip na namna ya kubadili two way two gang kuwa exchange switch
 
Back
Top Bottom