Watalaamu wa masuala ya kifedha kupitia kwa mawakala naomba mawazo yenu katika hili

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
2,968
9,226
Wakubwa kwa wadogo natanguliza salamu zangu kwenu nyote .

Moja kwa moja niende kwenye mada husika .

Ipo hivi hapa ofisi ninayofanyia kazi(sehemu ya biashara) dodoma area d kuna huduma za mawakala wa fedha zinafanyika hususan za simu na za kibenki.sasa leo kuna mtu kutoka singida kapiga simu kwa wakala hapa na kutaka kujua imekuwaje muamala alioufanya mwezi wa tano haukukamilika. Kwa maana hela aliyokuja ku deposit kupitia crdb wakala sicho kiwango stahiki.

Kwa maana ya kwamba kiwango kilichostahili kuwekewa ni milioni tano na sio tatu. basi kwenye simu akaulizwa huyo mhusika wewe imekuwaje hujadhibitisha kiasi hicho kama ni tano au tatu. Akasema yeye ni mfanyabiashara na yupo singida kwahiyo hapo dodoma alimwagiza mtu akamwekee milion tano kwa makubaliano yao ya kibiashara ambayo hatuwezi yajua kwenye akaunti lakini alipofuatilia benki statement imewekwa milioni tatu kwenye hiyo tarehe aliyosema kwamba ilistahili iwekwe tano.

Na ni kweli hata wakala mwenyewe akichapisha statement kwenye hiyo tarehe ni mil 3 iliwekwa nasio tano. Jamaa akaulizwa haukupata ujumbe wowote kwenye simu yako kwamba kuna kiasi fulani kimewekwa kwenye akaunti yako? Akasema alipata ila ni ile ya ku foward ila inasoma milioni tano na sio tatu. Kwamba jamaa alimfowadia tu mesj ma sio ile ya kutoka benki moja kwa moja .

Hapo labda ali edit kwenye figure amount.akulizwa je huyo aliyekuja ku deposit hiyo hela hakukutumia risiti ya muamala uliofanywa ,akasema hakupata risiti. Na mpaka kuja kuuliza kwa wakala ni kwamba jamaa aliyemtuma hapatikani tena kwa mujibu wa huyu ndugu.

Kwa mawazo yangu ni kwamba hiyu bwana huenda baada ya kupiga hesabu hazikai ikabidi akachukue bank statement benki na kuona hakuwekewa tano kama walivyokubaliana.. kwa maana yake kapigwa.

Lakini pia inakuaje mtu unaagiza kuwekewa fedha kwenye akaunti yako hata kama mnaaminiana .unakaa muda hivyo pasipo kufuatailia kama hela imeingia au la.

Hapa uzembe sijui utakuwepo kwa nani .

Nimeleta kwenu wadau tujadili
 
Nimejifunza kitu,

Kumbe hawa wenye kampuni hizi za kifedha wahakikishe ile sms ya mhamala huwezi ku-edit.Naomba makampuni mlifanyie kazi kama hii option haipo!

Katika tatizo hili acha waje wajuzi zaidi
 
Mimi navyojua hizi sms zinaingia automatically unapofanya transaction ya kutoa au kuweka.
 
Nimejifunza kitu,

Kumbe hawa wenye kampuni hizi za kifedha wahakikishe ile sms ya mhamala huwezi ku-edit.Naomba makampuni mlifanyie kazi kama hii option haipo!

Katika tatizo hili acha waje wajuzi zaidi
Kama unaiweza ukaicopy basi unaweza ukaedit.....chakufanya ni confirmation hapo tena ya pdf .ile risiti

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Nimejifunza kitu,

Kumbe hawa wenye kampuni hizi za kifedha wahakikishe ile sms ya mhamala huwezi ku-edit.Naomba makampuni mlifanyie kazi kama hii option haipo!

Katika tatizo hili acha waje wajuzi zaidi
Hapana, sms ziko sahihi sema Iko hivi Unapomwagiza mtu akuwekee fedha kwa Hawa mawakala hasa upande wa bank mwambie ajaze namba yako muwekewaji Ili Either CRDB au hao NMB wakutumie hiyo text ya muamala moja kwa moja na so vingine
 
Back
Top Bottom