Watalaamu tupieni maoni basi! Neno sahihi kati ya "hicho" na "hiko"

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
2,275
1,698
Mambo vipi wakuu!

Siku za hivi karibuni nilimsikia mtangazaji mmoja wa radio flani akizungumzia chuo flani huko mkoani Kilimanjaro. Neno alilokuwa akitumia ni "hiko" (tofauti na wengine niliozoea kuwasikia wakitamka "hicho").

Mtangazaji huyo alikuwa akitamka " Mkuu wa chuo hiko amesema kwamba..."
Vile vile mtangazi huyo aliendelea kutamka "aidha chuo hiko kinatoa nafasi..."

Swali langu ni kwamba je mtangazaji huyo yuko sahihi katika kutumia neno "hiko" badala ya neno "hicho"?

Maoni tafadhari.
 
Nadhani yupo sahihi zaidi.
Chuo kimefungwa vs Chuo chimefungwa

Wazee wa Ngeli watatusaidia zaidi hapo
 
Mambo vipi wakuu!

Siku za hivi karibuni nilimsikia mtangazaji mmoja wa radio flani akizungumzia chuo flani huko mkoani Kilimanjaro. Neno alilokuwa akitumia ni "hiko" (tofauti na wengine niliozoea kuwasikia wakitamka "hicho").

Mtangazaji huyo alikuwa akitamka " Mkuu wa chuo hiko amesema kwamba..."
Vile vile mtangazi huyo aliendelea kutamka "aidha chuo hiko kinatoa nafasi..."

Swali langu ni kwamba je mtangazaji huyo yuko sahihi katika kutumia neno "hiko" badala ya neno "hicho"?

Maoni tafadhari.
Ngoja kwanza nikuweke sawa wewe mwenyewe,

Sio tafadhari bali ni tafadhali
 
Back
Top Bottom