Watalaam, nini suluhisho la hili tatizo la uvimbe shingoni na homa?

Ahsante sana kwa ushauri wako mzuri, MUNGU akubariki sana ndugu angalau nimepata matumaini flani.
Pole sana mkuu TB inatibika vizuri tu wala msipate shida...!! Tena mwili wa jamaa inaonekana kinga yange bado ipo vizuri unaweza kupambana hasa.. Apige dawa kama alivyoandikiwa yani asichoke kabisa na Matunda ya kutosha kuimarisha kinga yake zaidi.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Ahsante mkuu, ngoja arudi tena hospital
 
Wadau msaada wenu tafadhali.

Cha kwanza ni kufanya vipimo ili kujilizisha kama TB imepona. Hii ikiwa ni kuangalia na dalili nyingine zilizoandamana na ugonjwa husika.

Lakini pia kuna haja ya kufanya screening kujilidhisha kuwa hivi vivimbe nj zao la TB pekee na hakuna kitu kingine.

Pili ni vizuri kufahamu kwa lympnodes huchukua muda mrefu kurudi sawa. Tunaona haya kwa watoto ambao hupata virusi vikali na kupata lympnodes, huwachukua muda mrefu kidogo vivumbe kuondoka. Hii inatokana na kiasi ambacho pia mfumo wa mwili ulichukua ukiwa unapambana na TB.

Hivyo fika hospitali ya karibu, mweleze daktari kuhusu suala lako. Atakueleza kama hayo yanaweza kufanyika na kwa kiasi kipi au atakupa rufaa.
 
Ushauri huu pia, apime na HIV pia kama awali hakupima

Ni kweli hii iko ndani ya screening. Wakati mwingine ukiandika kinagaubaga anaweza mtu asiende tena hospitali kwa kuona ndo nimekwisha au hakuna namna tena. Kumbe hiu ni mtizamo baada ya kuwa umesikiliza issue husika.

Maneno mengine huitaji kutoholewa ili baada ya counselling ndiyo twende mbele.
 
Back
Top Bottom