Uchaguzi 2020 Watakaopitishwa kura za maoni ndani ya CCM ni wenye pesa

Ruwamangi

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
944
1,669
Na Tade ole Mushi kada wa CCM.

FACT:- ATAKAYESHINDA KURA ZA MAONI NI MWENYE FEDHA.

Na Thadei Ole Mushi.

Vijana wengi wa CCM wametia nia kwenye maeneo mbalimbali ya kugombea Ubunge. Ni Jambo zuri Sana Ila issue ya kushinda Ni Kudra za mwenyezi Mungu.

Twende sawa.

Wanaopiga Kura kwenye majimbo yetu ni Viongozi wa matawi yetu, Viongozi Hawa Wana Hali ngumu kimaisha kwa maana ya wengi wanatokea kwenye familia za kipato Cha chini, Mpiga Kura Kama huyu akipelekewa baiskeli kama zile Kigwangala alizotoa anachaje kumpigia Kura HK?

Majimbo yetu mengi Wapiga Kura wanaanzia wajumbe 300 Hadi 500 kwa mtu aliyehudumu kwenye Ubunge kwa miaka hata mitano tu akiamua kuhonga watu Mia tatu kwa kuwapa kila mtu shilingi 20,000 atatumia shilingi milioni sita tu, akiamua kuwapa 40,000 elfu atatumia shilingi milioni 12 tu.

Kijana ambaye Hana fedha anawezaje kupambana na jitu lenye mamilioni ya shilingi aliyovuna kwenye Ubunge na kwa Sasa Wana Kiinua Mgongo?

Kijana ambaye Hana fedha anawezaje kupambana na Mbunge mwenye network kubwa ya watu wenye fedha wanaoweza kumfadhili akashinda?

Narudia Tena hakuna mahali ambapo mpiga Kura toka kwenye matawi anaweza akaacha elfu 40,000 halafu aje asikilize blah blah zinazoitwa sera na mipango ya vijana Tena sera zenyewe unapewa dakika tatu kuzielezea. Wajumbe Hawa siwalaumu Ila maisha yao yanawalazimu kuchukua rushwa hata Kama Ni kidogo.

Ni vigumu Sana katika Hali Kama hii mtu ambaye hana financial Muscles kushinda. Any way kamati kuu imeahidi kuwakata wote ambao watatumia hila kushinda lakini watawakata wangapi?.

Tuna nafasi bado ya kurekebisha utaratibu wetu wa kupata Viongozi. Hili nimeliongea Sana Sana ipo siku tutafika huko.

Ole Mushi
0712702602
 
Ccm Haiikubatii Rushwa Wakati Huu
Ng'ombe Aliyekatwa Mkia Machungani Akirudi Zizini Wenzake Watajua Hana Mkia!!
😀😁😂😅😃😃😃
 
Unajua kuna vitu kwenye maisha sio muhimu ila ni vya lazima
Sio vitu vyote vyenye umuhimu ni vya lazima
Sasa ngoja uone kazi wataparuliwa na 'chair' hawatoaminia
Ila kindakindaki kiukweli kiama kimewajia
 
Sijawahi kumwelewa kiumbe anayepokea/kataa rushwa ili kupiga kura, hivi hongo inawezaje kubadili maamuzi yako ambayo utayafanya sirini!

Tafuna takrima, kura ni siri yako.
 
Sijawahi kumwelewa kiumbe anayepokea/kataa rushwa ili kupiga kura, hivi hongo inawezaje kubadili maamuzi yako ambayo utayafanya sirini!

Tafuna takrima, kura ni siri yako.
Rushwa inasuta nafsi, amini usiamini ni ngumu sana ule pesa ya mtu halafu umtose
 
Ulivyoandika nikajua huyu anatokea kikimanjaro kumbe kweli Ni Mushi kada wa chadema anayejifanya CCM
Ndomaana mmefika huku. Kila anayewaambia ukweli mnaona ni CHADEMA. Lakini napata faraja kuona kuwa wanaosema ukweli ni CHADEMA (Wapinzani). Iko siku na wewe utasema ukweli ila sijui kama utabahatika kuitwa CHADEMA. Tuendelee.
 
Wewe uko Dunia ya wapi? Majina ya wagombea wote yanaanzia Dodoma.. Wabunge ambao hawakukisaidia chama wala serikali wote watakatwa fasta (huenda Ndugai akashiriki kwenye 'ukataji wa mwendokasi')... Ila wabunge waliokuwa na msaada (ikiwa ni pamoja na wale waliotoka upinzani) wataingizwa kwenye tatu bora ya kwenda kushindana jimboni kwenye kura za maoni .. Kikubwa, ombea jina lirudi jimboni.
 
Ni jambo la kushangaza, Sekretariat walibadilisha utaratibu wa kura za maoni uliozoeleka kwamba watia nia wachukue fomu halafu kati ya watia nia wote, majina 3 ndio yatarudishwa kupigiwa kura za maoni..utaratibu huu ungezuia kwa kias kikubwa matumiz ya pesa kuhonga wapiga kura vile hawez mgombea kutoa pesa kuhonga wakati hana uhakika kama jina lake litakuwa kati ya yale 3 yatakayorudishwa, inasemekana wenyeviti walipoitwa dodoma kwa mafunzo wakasema utaratibu huo utaleta lawama..hivi kweli kiongozi ukiogopa lawama utaongoza?

Rais angeogopa lawama za ndani na nje alizokuwa anapewa wakati korona imeingia leo tungekuwa hivi??? Sekretariat wametishwa kwa hoja dhaifu kabisa ili wabadilishe utaratibu mzuri walioweka na kukubali kurudia utaratibu mbovu wa zamani..kumbe CCM bado haijapona maradhi yake, wenyeviti wa CCM ni wanufaikaji wakubwa wa mfumo mbovu wa kura za maoni..kwa mfano unapitishaje watu 60 kupigiwa kura za maoni, suppose yule mtu wa 27 kati ya hao 60 ndiye potential, ni kweli hizo dakika 3 zitatosha kushawishi wajumbe wamchague wakati tayari walishawasikiliza wengine 26 mbele yake?

Si rahisi, hivyo tutarajie kupata watu wale wale ambao uwezo wao ni dhaifu na hivyo kumpa wakati mgumu Rais kuona watu wazuri wenye sifa na mambo mapya kumsaidia bungeni..kwa hili CCM wameteleza kwa kurudisha utaratibu mbovu wa zamani kwenye kura za maoni..lakini kiongozi shupavu haogopi lawama wakati akitenda haki inayoleta faida kwa wengi!!!
 
Fomu yenyewe ni laki 1 + kuchangia chama laki 5, kijana gani anayo hiyo hela? umeongea ukweli sana
Huna wanao kuunga mkono wakuchangie? utagombeaje wakati huna waunga mkono? wewe ni mgombea binafsi na ubinafsi hauna nafasi ndani ya CCM.KUGOMBEA INA MAANA UNA WATU NYUMA WALIO TAYARI KUKUUNGA MKONO KAMA HUNA ACHA KUGOMBEA

Wagombea kibao wanaokubalika maeneo yao mbona wengi wanachangiwa fomu ya kugombea

Wewe unatafuta pa kuponea!!!! Huna watu
 
.....jaribu kutofautisha zama, hizi ni zama za Magufuli. Mwenyekiti ameshatoa onyo kuwa atakayetumia rushwa kushinda hawezi kushinda... hivyo unaweza pata hizo kura lakini kama zimetokana na rushwa HUPITISHWI KUGOMBEA UBUNGE. Tunamwamini Mwenyekiti atalisimamia hilo bila tabu

Viva Magufuli.
 
Acha utapeli, kwanini wewe usigombee na wakati umejaa shida? kuchangiwa ni dalili ya rushwa
Huna wanao kuunga mkono wakuchangie? utagombeaje wakati huna waunga mkono? wewe ni mgombea binafsi na ubinafsi hauna nafasi ndani ya CCM.KUGOMBEA INA MAANA UNA WATU NYUMA WALIO TAYARI KUKUUNGA MKONO KAMA HUNA ACHA KUGOMBEA

Wagombea kibao wanaokubalika maeneo yao mbona wengi wanachangiwa fomu ya kugombea

Wewe unatafuta pa kuponea!!!! Huna watu
 
.....jaribu kutofautisha zama, hizi ni zama za Magufuli. Mwenyekiti ameshatoa onyo kuwa atakayetumia rushwa kushinda hawezi kushinda... hivyo unaweza pata hizo kura lakini kama zimetokana na rushwa HUPITISHWI KUGOMBEA UBUNGE. Tunamwamini Mwenyekiti atalisimamia hilo bila tabu

Viva Magufuli.
Na vp kamati nzima ya siasa yenye kutoa maoni ngazi za juu ikajazwa manoti,je,watamsaliti mtoa rushwa?
 
Acha utapeli, kwanini wewe usigombee na wakati umejaa shida? kuchangiwa ni dalili ya rushwa
Kwa hiyo mama yako,baba yako,kaka zako na dada zako wakikuchangia uchukue fomu ni rushwa? wewe huna ushirikiano hata na ndugu zako mwenyewe .Wangekuchangia kama ndugu usingekuja kupiga miyowe humu
 
Back
Top Bottom