Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Hivi karibuni tumesikia serikali imeamua kuvirudisha viwanda vilivyokuwa vimeuzwa halafu vikashindwa kuendelea kuzalisha au kushindwa kufufuliwa.
Kwa kuanzia tumeambiwa serikali itatoa au imetoa shilingi bilioni 60 ili kianze uzalishaji wa matairi. Pesa hiyo pamoja na kulipia gharama za ufufuaji, pia italipia hisa za mwekezaji aliyeshindwa kuzalisha matairi.
Kila mmoja anatamani kuona Tanzania ikiwa na viwanda vya aina mbalimbali kwa sababu hakuna asiyejua faida ya viwanda. Na kwa kiwanda cha matairi kama hicho cha Arusha ni muhimu sana hasa kwa sababu soko la matairi lipo ndani ya nchi yetu na linaendelea kukua kila siku.
Ninachojiuliza ni kwamba hivi viwanda vilikuwa chini ya serikali, tukashindwa kuviendesha, tukaamini kuviuza ndiyo uamuzi mzuri. Kama tulishindwa kuviendesha hapo awali, ni nini kitakachotufanya tuweze kuviendesha sasa? Ni watu gani tutakaowatumia kuvisimamia viwanda hivi? Tumeambiwa NDC ndiyo itakayokuwa msimamizi mkuu. Hiyo NDC ina watu wapya, wenye fikra mpya, uwezo mpya au ni watu wale wale walioua viwanda na mashirika ndiyo sasa wanaiendesha NDC?
Viwanda ni biashara. Uendeshaji wake unahitaji Sayansi ya biashara na uchumi, wala siyo ukada wa chama na ukaribu na wakuu wa serikali. Ili viwanda viweze kubuniwa, kuanzishwa na kuendelezwa ni lazima visimamiwe kibiashara. Kama msimamizi mkuu wa viwanda atakuwa ni NDC, je hii NDC kuanzia muundo wake na watendaji wake wamekaa kibiashara au wamekaa kiserikali/kisiasa? Kama NDC imekaa kiserikali/kisiasa, ni lazima hata muundo wa utendaji na usimamizi wa viwanda utakaa kiserikali/kisiasa.
SERIKALI HAINA UWEZO WA KUFANYA BIASHARA
Nimetumia muda mwingi kufanya kazi katika taasisi binafsi za kibiashara ndani nan je ya nchi kwa faida. Nikifanya ulinganifu wa taasisi binafsi za kibiashara na utendaji wa taasisi zile zinazofanya biashara zilizo chini ya serikali kuna tofauti kubwa. Utendaji wa taasisi za kibiashara zilizo chini ya serikali zimekaa kiserikali au kisiasa.
Maofisa wa serikali, japo kuna mabadiliko katika miaka ya karibuni, wengi wao wanataka kunyenyekewa au kuabudiwa. Maofisa wengi wa serikali, ni vigumu hata kumsimamisha kwenye corridor na kumweleza shida yako. Ni vigumu kumsimamisha barabarani ukataka asaini karatasi yako ambayo haihitaji hata kumbukumbu ya mafaili yaliyopo ofisini mwake. Ni vigumu sana kumpigia simu ofisa wa serikali saa 6 usiku akutatulie tatizo lako. Ni taasisi chache kama vile Polisi, JWTZ, Hospitali, Zimamoto, ambazo maofisa wake wapo kazini masaa yote 24, japo utendaji wao huwa ni hafifu na uliokosa usimamizi kamili muda baada ya masaa ya kawaida ya kazi
Niliowaongelea hapo juu ni watumishi/maofisa wa serikali. Kosa kubwa linalofanyika na serikali, ni kuwachukua watumishi hao hao waliokuwa maofisa wa serikali, ambao wamezoea kunyenyekewa, kuabudiwa kwenda kusimamia taasisi za kibiashara zilizo chini ya serikali. Kwa hiyo wanatoka na utendaji wao wa kiserikali kwenda kwenye taasisi za kibiashara. Huko wanaenda kuendesha taasisi za kibiashara kwa utaratibu wa kiserikali. Bahati mbaya biashara ina kanuni zake, haitaionea Huruma biashara yako eti kwa sababu biashara hiyo ni ya serikali.
Ukichunguza mara nyingi ni wale wale waliokuwa maofisa wa serikali muda fulani, ndiyo walipelekwa kuwa wakurugenzi wa TANESCO, TTCL, POSTA, BANDARI, AIR TANZANIA, NBC, na viwanda mbalimbali vya umma. Ni wale wale waliokuwa wanaua shirika/kiwanda kimoja wanapelekwa kuua shirika/kiwanda cha pili, cha nne, cha tano, wengine mpaka 10. Ukiangalia walivyokuwa wakiteuliwa na kuhamishwa unadhani serikali inatafuta mtu mwenye uzoefu mkubwa wa kuua mashirika/viwanda.
USHAURI
Ifahamike kuwa viwanda vyote vitakavyofufuliwa havitafanikiwa kama kwanza hautaangaliwa muundo wa msimamizi mkuu, yaani NDC. Je, hiyo NDC inasimamiwa na watu gani? Ni watu wenye sifa na historia ya kuanzisha au kuendesha taasisi za kibiashara kwa faida? Au uteuzi wao ulitegemea mlengo wao wa kisiasa, uzoefu wa miaka mingi ndani ya serikali na ukaribu wa viongozi wa serikali? Biashara ina kanuni zake. Huwezi kutaka kunyenyekewa au kuabudiwa halafu ukafanya biashara kwa mafanikio.
Kwenye makampuni makubwa binafsi kazi hufanyika masaa 24, na maamuzi pia maamuzi yanafanyika masaa 24. Ukiritimba wa kusema muda wa kazi umeisha, hatuwezi kufanya maamuzi, tusubiri kikao cha bodi kilichopangwa kufanyika mwezi ujao, n.k., haupo.
Kwenye sekta binafsi za kibiashara, mfanyakazi huweza kumwona boss wake mahali popote, wakati wowote na kwa namna yoyote. Anaweza hata kumfuata boss akiwa nje ya ofisi, anaweza kumsimamisha boss wake barabarani, anaweza kumfuata boss nyumbani kwake wakati wowote ili boss wake afanye uamuzi kwa lengo la kuhakikisha uzalishaji hausimami hata dakika 1. Hawa watu tulio nao watakaokabidhiwa kuviendesha na kuvisimamia hivyo viwanda, NDC na serikali yenyewe yenye mali kwa niaba ya wananchi, wamejiandaa kwa uendeshaji wa namna hiyo? Au watawazuia mameneja wa makampuni kufanya maamuzi ya operations mpaka vikao vya bodi? Au mameneja wataishia kutumbuliwa kwa kufanya maamuzi hata ya mambo ya uendeshaji bila ya idhini ya bodi?
NANI ATASIMAMIA KIWANDA CHA MATAIRI ARUSHA
Kiwanda hicho kinapofufuliwa, ni nani watakaokisimamia? Ni wale walioshindwa kukiendesha kiwanda kibiashara au tunatafuta watu wapya? Tutawachukua humu humu ndani ya nchi au tunawaleta kutoka nje? Tanzania tulikuwa na kiwanda kimoja tu cha matairi. Kama waliokuwa kwenye kiwanda hiki walishindwa kukiendesha kiushindani, tutawapata wapi wenye uzoefu na uwezo?
Litakuwa ni kosa kubwa kuwarudisha wasimamizi wale wa mwanzo waliokifanya kiwanda kishindwe kushindana, halafu tuamini safari hii wataweza. Uwezo wa kuendesha biashara ni pamoja na uwezo wa kuhimili ushindani. Inawezekani uwezo wa kuhimili ushindani kwa kiwanda hicho kulichangiwa na sababu nyingi kama vile upungufu na ughali wa nishati ya umeme lakini ni ukweli pia kuwa taasisi mbalimbali za kibiashara zilizo chini ya serikali daima zinakuwa nyuma sana kiteknolojia bila ya kutambua kuwa katika ulimwengu wa sasa tekinolojia ni ‘dynamic’, ndiyo maana makampuni mengi wakati wote yana mafunzo mbalimbali ya muda mfupi ili kuwawezesha wafanyakazi wake na wafanya maamuzi kuendani na kasi ya tekinolojia ambayo au huboresha ubora wa bidhaa au hupunguza gharama za uzalishaji.
Serikali au NDC isione shida kuwapata watu hata wa kutoka nje wenye uzoefu na uwezo wa kukiendesha kiwanda hicho kibiashara wakaungana na Watanzania, hasa katika hatua za awali. Watanzania wengi ni wazuri wa kujikweza kuwa wanaweza hata kwenye mambo ambayo hatuna uwezo nayo kiufanisi. Uendeshaji wa kiwanda hauhitaji tu vyeti vya shule bali record nzuri ya kiutendaji na uzoefu katika sekta hiyo ya uzalishaji matairi. Wengi watasema tunaweza kukiendesha wenyewe halafu matokeo yake kiwanda kitaishia kuomba ruzuku tena serikalini. Mfano mzuri ni TANESCO. Hili ni shirika ambalo limeendeshwa na wazalendo kwa miaka mingi lakini nadhani ndiyo taasisi ambayo ufanisi wake ni duni sana. Kama tusingekubali kuingiza kampuni binafsi za simu, chini ya TTCL iliyo chini ya serikali, sijui huduma za simu zingekuwaje nchini Tanzania!
Kama ilivyo kwenye miradi ya barabara, hata hivi viwanda, tunahitaji kuwa na wataalam washauri wakati wa kuvifufua na wakati wote wa kuviendesha.
Msambichaka Bart Mkinga