Wataka sheria iruhusu kujamiiana na wanyama

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,015
114,360
Walalamishi wawili wameshindwa katika jaribio lao la kuishinikiza mahakama ya kikatiba nchini Ujerumani kuangazia madai yao dhidi ya sheria inayopiga marufuku kujamiiana na wanyama. Watu hao ambao majina yao hayakutajwa wanasema kwamba wana uchu na wanyama.

Walitaka kuishinikiza mahakama hiyo iliopo Karlsruhe kufikiria iwapo sheria hiyo ni kinyume na katiba.

Hatahivyo mahakama hiyo ilitupilia mbali madai yao ikisema kuwa ni haki kwa sheria hiyo kuendelea kufuatwa. Mahakama ilisema kuwa kuwalinda wanyama dhidi ya unyanyasaji wa kingono ni jukumu la sheria ,ambayo haikubadilishwa kufuatia uamuzi wa mahakama hiyo.

Sheria za kuwalinda wanyama nchini Ujerumani zimeweka faini ya $27,700 kwa wale watakaowalazimisha wanyama kushiriki katika tabia mbaya.
 
Dah hakika tamaa zimewaka kwetu binadamu hadi zimepitiliza..Na wafanye uchunguzi wa hawa dada zetu wanaojifanya kuwapenda sana mbwa unakuta anatembea na mbwa kila mahala nasikia ukibahatika kuona anachofanya na huyo mbwa usiku...Utaanguka ufe kwa presha..
 
Sheria za kuwalinda wanyama nchini Ujerumani zimeweka faini ya $27,700 kwa wale watakaowalazimisha wanyama kushiriki katika tabia mbaya.

Kwa nini hiyo faini iwe ni kwa "watakaowalazimisha" wanyama badala ya kuwa tu kwa "watakaothibitishwa" kujamiiana na hao wanyama? Hakuna mazungumzo yoyote kati ya mtu na huyo mnyama yanayopelekea huyo mnyama kukubali kwa hiyari yake kujamiiana na mtu. Vinginevyo kama kuna vyombo vya sheria kuangalia uwepo wa kulazimisha au utayari wa mnyama mwenyewe maana yake ni kwamba kitendo cha mtu kujamiiana na mnyama kinakubalika mradi tu haujamlazimisha huyo mnyama.
 
Back
Top Bottom