Watafutaji Mafuta Hawalipwi Na Serikali.

Domo Kaya

JF-Expert Member
May 29, 2007
531
59
Na Tanzania daima 06.11.07

Imeelezwa kwamba makampuni inayoingia mkataba na Tanzania kuhusu utafutaji wa mafuta hujigharamia yenyewe pasipo kulipwa fedha yoyote kutoka serikalini.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini , Willium Ngeleja, amaliambia Bunge kuwa athari na gharama zote za utafutaji mafuta - kifedha na kiufundi hebebwa na kampuni husika. Endapo mafuta yatapatikana kampuni hiyo hutakiwa kufidia gharama zake kutoka katika mafuta yatayozalishwa.

alisema baada ya kuondo gharama hizo za utafutaji, faida inayopatikana hugawanywa kati ya kampuni husika na serikali na kimkataba ya mafuta kama hayatagunduliwa gharama za uwekezaji hazitarudishwa.

Alisema mikataba hiyo huiwezesha serikali kudhibiti shughuli za ufafutaji na uzalishaji wa mafuta ambako hadi sasa zipo kampuni 11 zinazoshughulika na utafutaji wa mafuta katika maendo mbalimbali.

Alisema utafutaji wa mafuta unahitaji fedha nyingi na utaalamu wa hali ya juu hivyo athari za utafutaji ni kubwa sana, ndiyo maana nchi nying zinazoendelea hazina uwezo wa kugharamia shughuli hizo.

Alisema kutokana na sababu hizo mikataba ya uzalishaji na kugawana mapata ndiyo bora zaidi kwa nchi zinazoendelea ili kuepuka hasara zinazoweza kujitokeza.

Alisema Tanzania haijaingia kwenye biashara ya mafuta kwa maana kuchimba, kusafirisha na kuuza. Hivyo ili kulinda shughuli za utafutaji sheria inayotumika ni sheria ya utafutaji na uzalishaji ya mwaka 1980.

Alisema kutokana na utafiti uliokwishafanyika Tanzania imeweza kugundua gesi asilia ya Songosongo kwa mita za ujazo bilioni 30, mnazi bay (Mita za ujazo bilion 15) na Mkuranga uchunguzi unakoendelea ili kubaini kiasi cha gesi kilichobo.

Alisema ingawa bado mafuta hayajagunduliwa, takwimu zilizopo na taarifa za kujeographia katika maeneo mbalimbali ikiwamo katika vilindi bya bahari na miambayenye tabaka katika nchi kavu zinazoashiria kuwako kwa mfumo hai wa mafuta nchini.
 
jamani ni ya kweli haya kwamba mafuta hayapatikani, na je hao watafuta mafuta mbona wanazidi kuja????? au ndio wanaendelea kula hasara kwa kutafuta kitu ambacho miaka na miaka hakipatikani??????
 
jamani ni ya kweli haya kwamba mafuta hayapatikani, na je hao watafuta mafuta mbona wanazidi kuja????? au ndio wanaendelea kula hasara kwa kutafuta kitu ambacho miaka na miaka hakipatikani??????

Labda ni utafutaji wa mafuta usio na kikomo/mwisho...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom