Watafiti: Uendeshaji bodaboda na baiskeli ni hatari kwa uzazi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
Vijana wengi Afrika Mashariki wamekuwa wakitumia baiskeli kufanya biashara ya uchukuzi wa abiria, maarufu kama boda boda.
Ni kazi inayohitaji mhudumu atumie nguvu nyingi za mwili wake.

Sasa, watafiti nchini Kenya wanasema kunaweza kuwa na changamoto nyingine - kwamba wahudumu wa bodaboda wanakabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wao wa uzazi.
Baada ya kufanya utafiti, waligundua kwamba waendeshaji boda boda walikuwa katika hatari ya kutoweza kutanua mishipa ya damu kwenye uume wakati wa kushiriki tendo la ngono.

Mmoja wa watafiti hao Isaac Wamalwa ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta aliambia BBC kwamba suluhu huenda likawa ni kutumiwa kwa kiti maalum ya waendesha baiskeli ambayo hakitadhuru uume wa waendeshaji.

Bw Wamalwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi alifanya utafiti miongoni mwa vijana eneo la Bungoma, magharibi mwa Kenya. Walichunguza wahudumu 115 wa boda boda wa umri wa chini ya miaka 40 eneo hilo, wakishirikiana na wataalamu wa afya ya uzazi kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Chuo Kikuu cha Nairobi.

"Tuliwachunguza vijana waendeshaji wa bodaboda Bungoma na matokeo yalikuwa ya kushangaza. Kwa jumla, tuligundua kwamba zaidi ya theluthi moja ya waendeshaji bodaboda, asilimia 35.9, ya washiriki walikuwa na matatizo ya kuweza kusimika," aliambia gazeti la Standard la Kenya.

Anasema tatizo lilitokana na kuendesha baiskeli hizo kwa muda mrefu.
Bw Wamalwa anasema wote walioendesha baiskeli kwa zaidi ya saa 60 kwa wiki, walikuwa na matatizo ya kiafya. Anatahadharisha pia kwamba maelfu ya vijana wanaofanya mazoezi kwenye vituo vya mazoezi mijini, kwa Kiingereza gym, ambapo huendesha baiskeli zisizosonga, wanakabiliwa na hatari sawa na hiyo.

"Ujumbe wetu ni muhimu kwao pia, kwamba wanafaa kuwa wanapumzika kwa muda kutoka kwa kazi yao. Anasema wanapojikakamua kutafuta posho, wanafaa pia kujali uwezo wao kitandani."
Wataalamu wengine sita kutoka Chuo Kikuu cha Moi walifanya utafiti mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya, na kupata matokeo yanayokaribiana na ya Bw Wamalwa.

Waliwachunguza wahudumu wa dbodaboda 131 wa umri wa kati ya miaka 18 na 65, umri wa kadiri ukiwa miaka 40. Waligundua kwamba asilimia 76 kati yao walikuwa na matatizo kitandani. Watafiti hao pia walidokeza kwamba tatizo hilo huenda linatokana na kuendesha baiskeli kwa muda mrefu.

BBC SWAHILI
 
Maneno tu haya, hao wanaoendesha baskeli nenda Tanga kashangae mtu ana watoto hadi 6
 
Kichwa cha Uzi wako kina bodaboda na baiskeli. au mtu anaposema baiskeli ana include na pikipiki? Ufafanuzi kwangu please.
 
Waliwafanyia uchunguzi wa uwezo wa kusimamisha dushe?
Vitendea kazi vyao vilikuwa ni nini?
 
Stori za vijiweni, huko vijijini baiskeli ndio usafiri mkubwa na watu wana watoto zaidi ya kumi.
 
Wangefanya utafiti kwa wawndesha pikipiki maarufu kama bodaboda huku bongoland,mimi huwa nahisi kua lile joto la tanki la pikipiki,kukaliwa muda mrefu na waendeshaji huwa linawaathiri.
 
Wengine tumeendesha mpaka baiskeli iinaexpire.... bado tuko fiti na uzazi tumemaliza, na bado mwili unadai.
 
Back
Top Bottom