Watafiti kujifungia "gesti" kupata data | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watafiti kujifungia "gesti" kupata data

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Edo, Dec 24, 2008.

 1. E

  Edo JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mtanzania jtano:

  RAS Lindi kapasua jipu-kumbe watafiti wetu wanapokwenda mikoani kutafuta data wanajifungia gesti wanajaza madodoso wao wenyewe halafu wanavunga kuwa wamekusanya data hizo toka kwa walengwa. Nadhani hili ni moja ya tatizo kubwa karibu katika kila jambo tunalopanga sababu hatuna takwimu sahihi. Sijui sasa ina maana kila kitu hewa, watumishi hewa!!!
   
 2. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  habari ndio hiyo. Kwani walikuwa hajui wanachokifanya
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  unajifungia ndani unatoa data za kiwango cha mavuno cha Mkoa. Ikitokea njaa inaonekana kuwa chakula kingi kiliuzwa badala ya kutunzwa na wakulima (ndio wanaposema kimevushwa kwenda nchi jirani). Kumbe hata data zenyewe hazikuwa sahihi. Ila kama China, tutaanza taratibu na tutafika, MINYORORO inawasubiri wahujumu.....
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kuna mtu hapa hafanyi kazi yake. Analipwa vizuri, anaenda kazini kwa gari la Serikali , ofisi nzuri tu yenye kiyoyozi.
  Halafu mtu anatuambia kitu ambacho alitakiwa akichukulie hatua.Hivi kwa nini RAS -Lindi hakuchukua hatua zaidi, au anangojea tume.Na huko ndiyo kushindwa kazi.
   
Loading...