Wataalamu yaha maneno tafsiri yake kwa kiswahili ni ipi?

Hiyo ni misemo sio maneno kwahiyo inakua ngumu kupata tafsiri ya moja kwa moja ila nadhani kwa hii Walk the talk= Tenda unachonena( msemo wa kiswahili)
 
Talk a Talk and Walk a talk

Hizi ni misemo au kwa kiswahili kizuli nahau,ni sentensi inakuwa na maana tofauti na maana ya kawaida ya maneno yaliyotumika.
mfano: ana mkono wa birika,kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa.
tukirudi kwenye swali lako kwa jinsi ya ufahamu wangu kama nikipotea ruksa kunisahihisha

Talk a talk- inamaanisha kuongea tu bila kufanya kile kitendo unachokiongea
walk the talk-inamaanisha unasema kitu then unakitenda kama ulivyosema.It means to do as you say you would do, to be consistent with your words and actions.Ni kama unavyosikia watu wanasema "practise what you preach" yanafanana.
Mtu anaweza kukwambia,can you walk the talk?Hapa kuna issue mmejadili sasa anataka ajue kama unaweza make that issue to happen(unaweza kutekeleza kwa vitendo).
Mtu anaye talk the talk ni dhaifu hana uwezo wa kufanya jambo litokee ila mtu anaye walk the talk huyu ni safi.
So kama utaambiwa wewe ni mtuwa ku talk the talk it means unaongea tu na hujawahi kufanya yale unayoyasema.
The way I see it
 
Wow!!!!!!!!!! Aqua you are so good................ you got it.
 
Back
Top Bottom