kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,010
Mara nyingi naona baadhi ya watu wakilalamika kuhusiana na suala la kuvunjwa kwa katiba katika maamuzi mbali mbali.Kuvunjwa huku kumekuwa kunafanywa na wale walioapa kuilinda na kuitetea katiba.Sasa nina maswali yafuatayo;
1.Kwa nini watu huapa kwa dini ama imani yao wanapopewa madaraka na kuahidi kuilinda katiba?Nini madhara ya kutotimiza kiapo?
2.Iwapo mtu atavunja katiba makusudi ama kwa kutojua,nini kitatokea?Hiki kitakachotokea mbona watu hawakiogopi kama kweli kipo?
3.Je utaratibu wa kuapa kwa wakristo,hawaoni kuwa ni kinyume na biblia yenyewe mtu anayotumia kuapa kwani imeandikwa "msiape"?
4.Je ni lazima kuwepo kwa katiba ambayo wala haitekelezwi au inapuuzwa?