Wataalamu wasema Askofu Gwajima amepotosha ukweli kuhusu chanjo ya corona

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,635
2,000
Dar es Salaam/Dodoma. Wakati Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikihitimisha mjadala wa bajeti yake jana, baadhi ya wataalamu wamemkosoa Askofu Josephat Gwajima kwa msimamo wake kuhusu chanjo ya corona.

Gwajima, ambaye ni mbunge wa Kawe (CCM) alitoa angalizo hilo Mei 11, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya na kuzitaja aina tatu za chanjo ya ugonjwa huo alizosema hazijafanyiwa utafiti wa kina.

Pia, alisema chanjo hizo hazijapitishwa na taasisi zinazohusika na udhibiti wa magonjwa ambazo ni CDC (Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa) na FDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa) kwa Marekani na EMA (Wakala ya Dawa) kwa Ulaya.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Daniel Maeda alisema Askofu Gwajima anapotosha anaposema taasisi ya CDC inahusika na kuruhusu kutumika kwa chanjo au ubora wake.

“CDC haihusiki na upitishaji wa chanjo, bali inahusika na magonjwa ya binadamu kama ilivyo NIMR (Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu). FDA ndiyo inayoruhusu chanjo na ndiyo imeunda mfumo wa kuruhusu chanjo za dharura, siyo shirika jingine kama anavyosema Gwajima,” alisema Dk Maeda alipozungumza kwa simu.

Akifafanua zaidi, alisema chanjo hizo za corona zimeruhusiwa kwa dharura baada ya utafiti wa awali kuonyesha zina faida zaidi kuliko madhara katika kukabiliana na virusi hivyo vinavyoitesa dunia kiasi cha kuyumbisha uchumi.

“Wametoa ruhusa huku wakiendelea na utafiti mwingine kuona kama faida walizoziona zinaendelea kuwepo au kutaibuka madhara ambayo hawakuyaona awali,” alisema.

Kuhusu madhara ya kijenetiki, Dk Maeda alisema si kweli kwamba chanjo hizo zinaweza kuleta madhara.
“Chanjo hizi zinapoingia kwenye seli hazipenyi kwenye kiini (nucleus) bali zinaishia kwenye ganda la juu (cytoplasm). Kwanza hata virusi vya corona haviwezi kuingia kwenye kiini hicho. Kinachoweza kuingia ni virusi vya Ukimwi na ndiyo maana mpaka sasa hakuna chanjo yake,” alisema.

Kwa upande wake, mhadhiri wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dk Emmanuel Malya alisema hakuna haja ya kuwa na hofu kwa kuwa chanjo zote zimethibitishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) linalosimamia tiba na afya za watu wote duniani.

“Ni chanjo zinazotumika duniani kote, hata China wametengeneza chanjo kwa njia hiyo. Kama ni madhara, kila dawa inayo. Hata ukitumia panadol kuna madhara yake,” alisema Dk Malya.

Aliongeza kuwa matumizi ya chanjo duniani yamepunguza maambukizo nchi za Ulaya na Marekani.

Hoja za wabunge
Akihitimisha mjadala wa hotuba yake ya bajeti jana, Waziri wa Afya, Dk Doroth Gwajima alisema yeye na timu yake wamejipanga kushughulikia hoja hizo kwa masilahi ya Watanzania.

Akijibu hoja kuhusu janga la corona iliyoibuliwa na Askofu Gwajima juzi, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel alisema hadi sasa Serikali bado inatembea na kauli ya Hayati John Magufuli aliyoitoa mkoani Kagera aliposisitiza kuwa Tanzania haiwezi kupokea kila kitu kutoka nje bila kukifanyia uchunguzi wa kujiridhisha.

Alisema ndiyo maana Rais Samia Suluhu Hassan ameunda tume ambayo imejaa wasomi na maprofesa.

“Tanzania haipingani na WHO (Shirika la Afya Duniani) wala siyo kisiwa cha kujifungia, hoja ya Mheshimiwa Gwajima tumeichukua na kumwambia kuwa Serikali inalitambua hilo na iko makini hivyo mtupe muda kamati aliyoiunda mheshimiwa Rais itakuja na majibu yote,” alisema Dk Mollel.
Alisema Serikali inajua kuhusu uchunguzi wa chanjo na hadi sasa kamati hiyo iliyojaa maprofesa imejichimbia kutafiti na itakuja na majibu ya moja kwa moja kumshauri Rais cha kufanya.

Kuhusu mtambo wa kuzalisha barakoa unaodaiwa kuzalisha chini ya matarajio, Waziri Gwajima alikiri kuwa ulianza kwa kusuasua, lakini baadaye walinunua na na kuboresha vifaa hivyo ukaanza kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa ambacho ni barakoa 48,000 kwa siku.

Akijibu hoja za jumla zilizotolewa na wabunge, Waziri Gwajima alisema suala la uhaba wa dawa bado lipo, ila linachangiwa na kupatikana kwa fedha.

Waziri alikiri kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kununua dawa, vifaa na vitenganishi hazikutolewa kama ilivyotakiwa, lakini akaahidi kuwa Sh200 bilioni zilizopangwa mwaka wa fedha 2020/21 zitatolewa hadi mwishoni mwa Juni unapohitimishwa mwaka wa fedha.

Alisema kumekuwa na mwongozo ambao utawezesha kuwa na mzunguko mzuri wa upatikanaji wa dawa kutokana na mchango wa watu wanaochangia katika huduma ya afya kwenye dawa ambako alisema usimamizi wake utakuwa mkubwa zaidi.
Waziri pia alizungumzia bima ya afya kwa wote na aliwataka wabunge kuwa wavumilivu, kwani muswada uko mbioni kupelekwa mjengoni humo kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii wanayoiwakilisha.

Na kuhusu madeni yaliyopo ndani ya wizara hiyo na taasisi zake, alisema hadi Aprili 2021, Serikali ilishalipa Sh16.3 bilioni, lakini bado inadaiwa Sh260.7 bilioni na Bohari ya Dawa (MSD) ambazo zinajumuisha madeni ya vituo vya afya.
 
Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,479
2,000
Gwaji tangu afumaniwe akili zilimruka, anadandia hoja bila kuwa na chembe ya utaalam, wamemnywesha matango pori naye anayamwaga kama yalivyo bila hata kujiridhisa kwa wataalam wa afya.

Angalizo, Kitu kama huna utaalam nacho, usijitie kimbelembele aibu itakuwa yako. Hivi kweli huyu alikuwa mchunga kondoo wa Mungu?

Tangu nimfahamu huyu anayejiita Askofu kwamba anafufua wafu, sijawahi kumuona aliyefufuliwa, najua siku moja hicho kijiwe chake kilichopo ubungo kitatoweka kwasababu ya kutokidhi vigezo vya kiimani.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,623
2,000
Wataalamu dhidi ya mamburula (pedestrians). Hii inaweza kutokea Tanzania tu.

Madhara ya dhahiri ya kupuuzwa mno kwa taaluma na wataalamu katika awamu ile yenye kiza kinene.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
24,763
2,000
Hao wataalam mbona sasa wamemuunga mkono kwamba hiyo dawa ni ya majaribio, sijaona sehemu wamekanusha hilo, sasa sijajua kukosoa maana yake nini?

Na pia huyo anyejiita mtaalam kusema kwamba MRNA haiingii kwenye nucleus hivyo madhara tajwa hayapo nadhani hajielewi, hiyo ni sawa na kusema nikiingia ndani kwako kukuletea ujumbe ndio ujumbe unafika, bali nikiishia dirishani kwako na kukufikishia ujumbe kwa sauti kubwa kupitia dirishani basi ujumbe unakuwa haufiki.

Madalali wa chanjo wanahangaika sana ili wapige 10%
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
24,763
2,000
Gwaji tangu afumaniwe akili zilimruka, anadandia hoja bila kuwa na chembe ya utaalam, wamemnywesha matango pori naye anayamwaga kama yalivyo bila hata kujiridhisa kwa wataalam wa afya.
Angalizo, Kitu kama huna utaalam nacho, usijitie kimbelembele aibu itakuwa yako. Hivi kweli huyu alikuwa mchunga kondoo wa Mungu? Tangu nimfahamu huyu anayejiita Askofu kwamba anafufua wafu, sijawahi kumuona aliyefufuliwa, najua siku moja hicho kijiwe chake kilichopo ubungo kitatoweka kwasababu ya kutokidhi vigezo vya kiimani.
Sawa alifumaniwa, hilo hatukatai, ila mbona hoja yake ya kuwa chanjo ni ya majaribio nao wameiunga mkono?
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,623
2,000
Hao wataalam mbona sasa wamemuunga mkono kwamba hiyo dawa ni ya majaribio, sijaona sehemu wamekanusha hilo, sasa sijajua kukosoa maana yake nini?

na pia huyo anyejiita mtaalam kusema kwamba MRNA haiingii kwenye nucleus hivyo madhara tajwa hayapo nadhani hajielewi, hiyo ni sawa na kusema nikiingia ndani kwako kukuletea ujumbe ndio ujumbe unafika, bali nikiishia dirishani kwako na kukufikishia ujumbe kwa sauti kubwa kupitia dirishani basi ujumbe unakuwa haufiki.
Madalali wa chanjo wanahangaika sana ili wapige 10%

Staha ilitumika. Wako hapa:

Nisiache kugongelea na nyundo. Ujinga ni adui mbaya sana kuliko hata Corona yenyewe.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
24,763
2,000
Staha ilitumika. Wako hapa:

Nisiache kugongelea na nyundo. Ujinga ni adui mbaya sana kuliko hata Corona yenyewe.
“Staha ilitumika wako hapa” ; atakae elewa hii sentensi anishtue.

Ila kwa sasa jibu hoja yangu.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,623
2,000
“Staha ilitumika wako hapa” ; atakae elewa hii sentensi anishtue.

Ila kwa sasa jibu hoja yangu.

Hahaahaaa haa! Ukimnukuu mtu, kumbuka kumnukuu sahihi kabisa bila kuacha nukta wala koma. Vinginevyo kwa kiswahili, itakuwa ni "kujitia hamnazo."

Kwenye red uliandika hukuona walipomkosoa Askofu Gwajima.

IMG_20210513_184908_171.jpg

Kwenye blue nikakutaarifu kama hauoni basi itakuwa ni "staha tu" ya mleta mada na kukupa source ya habari nzima kwenye green ukipenda kujiridhisha mwenyewe.

NB: Kiswahili ni bahari. Kushindwa kuelewa andiko ni jambo la kawaida mno. Kwa kushindwa kuelewa kwako hakukufanyi binafsi kuwa na lolote la zaidi.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,095
2,000
Gwaji tangu afumaniwe akili zilimruka, anadandia hoja bila kuwa na chembe ya utaalam, wamemnywesha matango pori naye anayamwaga kama yalivyo bila hata kujiridhisa kwa wataalam wa afya.

Angalizo, Kitu kama huna utaalam nacho, usijitie kimbelembele aibu itakuwa yako. Hivi kweli huyu alikuwa mchunga kondoo wa Mungu?

Tangu nimfahamu huyu anayejiita Askofu kwamba anafufua wafu, sijawahi kumuona aliyefufuliwa, najua siku moja hicho kijiwe chake kilichopo ubungo kitatoweka kwasababu ya kutokidhi vigezo vya kiimani.
tukiachana na uzinzi wake,wewe unaweza kumshinda gwajima kwa uelewa wa mambo,
au kujenga hoja??
 
Afande Tanzania

JF-Expert Member
May 3, 2020
460
1,000
Dar es Salaam/Dodoma. Wakati Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikihitimisha mjadala wa bajeti yake jana, baadhi ya wataalamu wamemkosoa Askofu Josephat Gwajima kwa msimamo wake kuhusu chanjo ya corona.

Gwajima, ambaye ni mbunge wa Kawe (CCM) alitoa angalizo hilo Mei 11, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya na kuzitaja aina tatu za chanjo ya ugonjwa huo alizosema hazijafanyiwa utafiti wa kina.

Pia, alisema chanjo hizo hazijapitishwa na taasisi zinazohusika na udhibiti wa magonjwa ambazo ni CDC (Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa) na FDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa) kwa Marekani na EMA (Wakala ya Dawa) kwa Ulaya.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Daniel Maeda alisema Askofu Gwajima anapotosha anaposema taasisi ya CDC inahusika na kuruhusu kutumika kwa chanjo au ubora wake.

“CDC haihusiki na upitishaji wa chanjo, bali inahusika na magonjwa ya binadamu kama ilivyo NIMR (Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu). FDA ndiyo inayoruhusu chanjo na ndiyo imeunda mfumo wa kuruhusu chanjo za dharura, siyo shirika jingine kama anavyosema Gwajima,” alisema Dk Maeda alipozungumza kwa simu.

Akifafanua zaidi, alisema chanjo hizo za corona zimeruhusiwa kwa dharura baada ya utafiti wa awali kuonyesha zina faida zaidi kuliko madhara katika kukabiliana na virusi hivyo vinavyoitesa dunia kiasi cha kuyumbisha uchumi.

“Wametoa ruhusa huku wakiendelea na utafiti mwingine kuona kama faida walizoziona zinaendelea kuwepo au kutaibuka madhara ambayo hawakuyaona awali,” alisema.

Kuhusu madhara ya kijenetiki, Dk Maeda alisema si kweli kwamba chanjo hizo zinaweza kuleta madhara.
“Chanjo hizi zinapoingia kwenye seli hazipenyi kwenye kiini (nucleus) bali zinaishia kwenye ganda la juu (cytoplasm). Kwanza hata virusi vya corona haviwezi kuingia kwenye kiini hicho. Kinachoweza kuingia ni virusi vya Ukimwi na ndiyo maana mpaka sasa hakuna chanjo yake,” alisema.

Kwa upande wake, mhadhiri wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dk Emmanuel Malya alisema hakuna haja ya kuwa na hofu kwa kuwa chanjo zote zimethibitishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) linalosimamia tiba na afya za watu wote duniani.

“Ni chanjo zinazotumika duniani kote, hata China wametengeneza chanjo kwa njia hiyo. Kama ni madhara, kila dawa inayo. Hata ukitumia panadol kuna madhara yake,” alisema Dk Malya.

Aliongeza kuwa matumizi ya chanjo duniani yamepunguza maambukizo nchi za Ulaya na Marekani.

Hoja za wabunge
Akihitimisha mjadala wa hotuba yake ya bajeti jana, Waziri wa Afya, Dk Doroth Gwajima alisema yeye na timu yake wamejipanga kushughulikia hoja hizo kwa masilahi ya Watanzania.

Akijibu hoja kuhusu janga la corona iliyoibuliwa na Askofu Gwajima juzi, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel alisema hadi sasa Serikali bado inatembea na kauli ya Hayati John Magufuli aliyoitoa mkoani Kagera aliposisitiza kuwa Tanzania haiwezi kupokea kila kitu kutoka nje bila kukifanyia uchunguzi wa kujiridhisha.

Alisema ndiyo maana Rais Samia Suluhu Hassan ameunda tume ambayo imejaa wasomi na maprofesa.

“Tanzania haipingani na WHO (Shirika la Afya Duniani) wala siyo kisiwa cha kujifungia, hoja ya Mheshimiwa Gwajima tumeichukua na kumwambia kuwa Serikali inalitambua hilo na iko makini hivyo mtupe muda kamati aliyoiunda mheshimiwa Rais itakuja na majibu yote,” alisema Dk Mollel.
Alisema Serikali inajua kuhusu uchunguzi wa chanjo na hadi sasa kamati hiyo iliyojaa maprofesa imejichimbia kutafiti na itakuja na majibu ya moja kwa moja kumshauri Rais cha kufanya.

Kuhusu mtambo wa kuzalisha barakoa unaodaiwa kuzalisha chini ya matarajio, Waziri Gwajima alikiri kuwa ulianza kwa kusuasua, lakini baadaye walinunua na na kuboresha vifaa hivyo ukaanza kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa ambacho ni barakoa 48,000 kwa siku.

Akijibu hoja za jumla zilizotolewa na wabunge, Waziri Gwajima alisema suala la uhaba wa dawa bado lipo, ila linachangiwa na kupatikana kwa fedha.

Waziri alikiri kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kununua dawa, vifaa na vitenganishi hazikutolewa kama ilivyotakiwa, lakini akaahidi kuwa Sh200 bilioni zilizopangwa mwaka wa fedha 2020/21 zitatolewa hadi mwishoni mwa Juni unapohitimishwa mwaka wa fedha.

Alisema kumekuwa na mwongozo ambao utawezesha kuwa na mzunguko mzuri wa upatikanaji wa dawa kutokana na mchango wa watu wanaochangia katika huduma ya afya kwenye dawa ambako alisema usimamizi wake utakuwa mkubwa zaidi.
Waziri pia alizungumzia bima ya afya kwa wote na aliwataka wabunge kuwa wavumilivu, kwani muswada uko mbioni kupelekwa mjengoni humo kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii wanayoiwakilisha.

Na kuhusu madeni yaliyopo ndani ya wizara hiyo na taasisi zake, alisema hadi Aprili 2021, Serikali ilishalipa Sh16.3 bilioni, lakini bado inadaiwa Sh260.7 bilioni na Bohari ya Dawa (MSD) ambazo zinajumuisha madeni ya vituo vya afya.
Mchango pekee wa Gwajima unaokubalika katika jamii Ni video za ngono, nje ya hapo Ni debe tupu Hana kitu kwenye lile bichwa.
 
chapangombe

Senior Member
Sep 28, 2014
142
225

Hahahaha mkuu hapo napingana na wewe kanisa anamchango mkubwa sema Hana kwako tu kumbuka kupitia nafasi ya uaskofu anawasaidia wangapi? Lkn haitoshi umeshawahi kufika kqnisani kwake jpili ? Wote unaowaona yeye ndiye anayewaongoza

Lakini pili kwa nafasi yke ya ubunge anawatetea watu wake hasa Jimbo lake kwani nawewe ni mbunge wako?
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,085

Mimi nashangaa watu kumjibu Lumpen kama Gwajima! This is a typical Lumpen proletariat, why bother with him!
 
Afande Tanzania

JF-Expert Member
May 3, 2020
460
1,000
Hahahaha mkuu hapo napingana na wewe kanisa anamchango mkubwa sema Hana kwako tu kumbuka kupitia nafasi ya uaskofu anawasaidia wangapi? Lkn haitoshi umeshawahi kufika kqnisani kwake jpili ? Wote unaowaona yeye ndiye anayewaongoza

Lakini pili kwa nafasi yke ya ubunge anawatetea watu wake hasa Jimbo lake kwani nawewe ni mbunge wako?
Sina mbunge mwizi wa kura.

Sikatai Gwajima kanisaidia Sana, nilikuwa operasheni nje ya nchi wakati ile video yake inatoka, kwa kweli niseme tu ukwelii huwa napenda kondoo nyeupe Kama ile aliyokuwa anakula Gwajima., hivyo ile video ilitusaidia Sana kwenye puchu puchu puchu soldiers wote tuliokuwa kwenye ile operation.

Tunaamini hatatuangusha this time maana Kuna hao covid-19 hachelewi kutembea na mkee wa Mdee, sema atutupie tena kavideo tupo Africa ya kati tupate ya kupigia puchu puchu tena, mademu adimu huku
 
Hhhhh ok mkuu
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,772
2,000
tukiachana na uzinzi wake,wewe unaweza kumshinda gwajima kwa uelewa wa mambo,
au kujenga hoja??
Gwajima huwa ana kopi mitandaoni anaenda ku paste bungeni na kanisani kwake.
Elimu ya genes kaisomea wapi mkuu ?
Wachungaji wengi walikosa elimu kwa njia rasm wakaenda za uinjilist, hawana kitu.
Uchungaji ni ujanja ujanja na ukanjanja.
Gwaji aliwahi sema Korona ni 5G.Hana lolote, waumini wake ndio humuona kichwa.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,095
2,000
Gwajima huwa ana kopi mitandaoni anaenda ku paste bungeni na kanisani kwake.
Elimu ya genes kaisomea wapi mkuu ?
Wachungaji wengi walikosa elimu kwa njia rasm wakaenda za uinjilist, hawana kitu.
Uchungaji ni ujanja ujanja na ukanjanja.
Gwaji aliwahi sema Korona ni 5G.Hana lolote, waumini wake ndio humuona kichwa.
mimi nimeuliza tu,unaweza kupambana na gwajima katika kujenga hoja,tuliachana na uzinzi maana huko inawezekana unampiga 5:0.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,772
2,000
Sauti yako imesikika mkuu.
VETA unafundishwa na akina nani, wamesoma wapi? VETA huandaa walimu ?
Mara nyingi sana VETA ni ngazi ya elimu ya wasio na uwezo mkubwa na ndio maana hadi la7 wanasajiliwa.
Elimu ya VETA ni ya vitendo hivyo mwenye IQ ndogo hawezi shindwa kuelewa, hakuna abstract knowldegde.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom