Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Wataalam wa Umoja wa Mataifa wamesema kwenye ripoti yao kwamba Korea ya Kaskazini inaendelea kuiba mamilioni ya dola kutoka katika taasisi za kifedha na makampuni yanayojihusisha na sarafu za mitandao na ubadilishanaji fedha.
Wataalamu hao waliowanukuu wataalamu wa masuala ya mitandao kwenye ripoti yao, wamesema fedha hizo za wizi zimekuwa muhimu kwa Pyongyang kufadhili miradi yake ya nyuklia na makombora.
Jopo la wataalam la Umoja wa Mataifa limesema kulingana na duru ambazo hazikutajwa serikalini, wadukuzi wa mitandao wa Korea Kaskazini waliiba zaidi ya dola milioni 50 kati ya mwaka 2020 na katikati ya mwaka 2021.
Fedha hizo ziliibwa kutoka mashirika yasiyopungua matatu ya ubadilishanaji fedha yaliyoko Amerika ya kaskazini, Ulaya na Asia, kitendo ambacho huenda kinaakisi njama ya Korea Kaskazini kujumuisha uhalifu wa mitandao kwenye operesheni zake.
Wataalamu hao wamesema kwenye ripoti yao kuhusu uhalifu wa mitandao, kwamba kampuni moja ya usalama wa mitandao ambayo haikutajwa jina iliripoti kwamba mnamo mwaka 2021, wadukuzi wa mitandao wa Korea Kaskazini waliiba jumla ya dola milioni 400 za sarafu za kidijitali.