Wataalamu wa Saikolojia tusaidieni: Nini chanzo cha matatizo ya viongozi wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wataalamu wa Saikolojia tusaidieni: Nini chanzo cha matatizo ya viongozi wetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyamahodzo, Jul 23, 2011.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa nikitafakari sana lakini nafika mahali nagota, ila badi sijahitimisha(not concluded). Mtaani nako wamekuwa wakisema-sema na hata JF kuandika-andika kuwa kiongozi fulani ni mgonjwa au anamatatizo katika akili zake. Si hivyo tu hata wale wanaomtetea muhusika katika jambo ambalo liko wazo kuwa ni la aibu kufanywa katika jamii ya wastaarabu, nao huambiwa wana matatizo katika akili zao.

  Wanasaikolojia naomba mtusaidie kufahamu ni kwanini wahusika wako hivyo, chanzo chake na ikibidi tufanye nini ili kuiokoa jamii yetu kiujumla isikumbwe na tatizo hilo kwa ujumla wake, ama kupata marudio ama ongezeko la tatizo hilo.

  Ukiwasakiliza viongozi wetu wa serikali na kisiasa, kuanzia kwa mkuu wa kaya hadi mawaziri, makatibu wa wizara, wakurugenzi, na kadhalika utagundua kuwa wengi wao wanatoa kauli zilizojaa uongo na karaha katika jamii inayotaka kushibishwa na ukweli. Kauli hizo zinaumiza jamii ama moja kwa moja au kwa namna nyingine.

  Hebu tafakari kauli zinazotolewa na mkuu wa kaya na mwaziri wake, pia zile zinazotolewa na DPP ama Mkurugenzi wa TAKUKURU, ama baadhi ya wabunge hadi spika. Zinafanya hadi wanajamii wanatukana ikiwa ni matokeo ya kuchukizwa kwao na kauli hizo.

  Ili tupate ufafanuzi mzuri, wanasaikolojia tusaidie, nini tatizo la kiongozi wetu wa kaya na mawaziri wake?
  Vile akiwa ni mtu wa kuheshimiwa, anapotoa kauli za uongo wa wazi na kusahahau siku chache nyuma alisema nini bila ya woga ni matokeo ya malezi ya utoto? Msongo wa mawazo katika utu uzima? Mlevi wa madaraka? Ulevi pombe, madawa, n.k.? Woga? Unafiki? ni kufuata mkumbo?
  (Mf, wanasaikolojia wanasema kuwa ukatili aliokuwa nao Adolf Hitler ni matokea ya kukatishwa kunyonya maziwa toka kwa mama yake kabla ya wakati, maana alikatishwa kunyonya mapema. Tafiti zao zinaonyesha watoto wengi wanaokatishwa kunyonya maziwa ya mama zao huwa wanakuwa na tabia ya ukatili). Nini chanzo cha umbumbumbu huu wa viongozi wetu hata kwa wale ambao katika ujana wao walikiuwa ni bora (bright)?

  Wanasaikolojia ndio ninyi mnaosema kila kiburi kina chanzo na kinamahali pa kushikilia.

  Ikiwa kama yana msingi wa utotoni tushaurini tuiponyaje jamii ya watanzania ili wasije wakawa na watawala/viongozi wabovu kama hawa tunaowaona leo.

  Ninawaalika wanasaikolojia wote, kuanzia wale wa saikolojia ya watoto, saikolojia ya jamii katika ujumla wake(mass psychologist), saikolojia ya tiba (psychopathologist) na tanzu nyingine za saikolojia.

  Sikuiweka kule kwenye jukwa la elimu wala JF doctor kwa wanaohusika ni wanasiasa, watawala na viongozi. Naukiliangalia vizuri utaona hoja hii ni mtambuka.

  Nwasilisha.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Ukifocus kwenye viongozi tu utakosea, viongozi wanatoka miongoni mwa jamii yetu. Kama unataka utafiti wa kina angalia jamii nzima ya Tanzania.
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  <P>
  </P>
  <P><BR>Mkuu, naomba nielewe vizuri. Najua viongozi wametoka katika jamii, katika familia. Ili tupate kulijadili vizuri lazima tuwe na mahali pa kuanzia. Kwa ufahamu wangu, mahali hapo ni kwa viongozi wetu kwani udhihirisho (manifestation) wa matatizo ya kisaikolojia unaweza yaona/kuonekana na wengi kuliko jamii yenyewe. Kwa kupata maarifa jumla hapa basi ni rahisi kuifikiria jamii na hata familia. Na malengo yawe kuiponya jamii ya watanzania ijayo msingi ukiwekwa sasa. <BR>Nisome vizuri. If you dont want my approach go with that of yours.</P>
   
 4. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  I think is due to ''mihemko'' intensity for wealth accummulation.Otherwise hawana shida kwani huwa tunawachagua wakiwa timamu.
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, mihemko (emotions) ni passive issue. Kwanini kwao inakuwa kama kitu cha kudumu? Kma jambo linaloendelea?
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Utajuaje kwamba tatizo si la jamii nzima, na kwamba tunaliona kwa viongozi tu kwa kuwa wao ndio walio visible kutokana na madaraka yao?

  Kwa maoni yangu, uki focus kwenye jamii nzima unapata sample space kubwa itakayokupa matokeo yaliyo accurate zaidi.

  Kuwa treat viongozi kama a special breed of people ni makosa.

  Swali zuri zaidi ni, matatizo ja jamii ya Kitanzania ni nini? Mbona tunatoa viongozi wa ajabu?
   
 7. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  nadhani inatokana na upungufu wa busara mwilini/UBUMWI/. Tatizo hili ni la kurithishana na huchukua miaka 5,000 tatizo liondoke kwenye chembechembe za DNA za jamii husika. Njia nyingine ya kuondoa tatizo hili ni kuua angalau theluthi ya jamii iliyopo, hasa watu wenye umri wa miaka ya 50 na kuendelea. Tafiti mbalimbali zinaonyesha uwiano/proportionality/ wa tatizo na watu waishio kando ya bahari/pwani/. Taarifa nyingine nyingi zipo psychiatric.com
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwenye red, nafikiri ni watu wenye matatizo makubwa ya kiakili a.k.a. wendawazimu wanaweza kukubali.
   
 9. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ulichoandika ndio tatizo nilalolizungumzia na kinathibitisha uwepo wa tatizo.
   
 10. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  tatizo lao wana nyumba ndogo nyingi mno
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo, mtu akiwa na nyumba ndogo anakuwa hana akili. Hana akili ya kufanya maamuzi sahihi. Pia hutoa kauli za dharau kwa jamii anayoiongoza.
   
 12. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubinafsi, uelewa mdogo wa mambo! mfano kiongozi anaulizwa kuhusu tatizo sugu la umeme, majibu yake ni kuwa serikali haina uwezo wa kuleta mvua na kujaza maji mabwa ya kuzalisha umeme, huu ni ufinyu wa mawazo, kiburi, jisahau n,k tena anatoa majibu kwa jazba.
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Tatizo mama ni malezi,kwenye malezi ndo unatengeneza mtazamo wa kila jambo!Ndivyo utaishi ukubwani!
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Naona ni ulimbukeni wa madaraka mtu anaona kwavile yupo chama flani kuwajibishwa si rahisi kwahiyo wanajisahau kwa mfano TZ tungeweza kubadili chama tawala kila wakati wa uchaguzi changamoto zingekuwepo na pindi wakiwa madarakani watakua waangalifu sana ili wabaki madarakani hilo lingetusaidia sana
   
 15. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  tatizo la viongozi na watumishi wetu ni kwamba wanaongoza na kutumikia nchi wasiyoijua, wasiyoipenda na wasiyoithamini. Haya mengine yote ni matokeo tu ya huo upungufu.
   
 16. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naam ni kweli tunatatizo la uongozi ,lakini sidhani ni tatizo la kisaikolojia bali ni tatizo la kimfumo [System].Mwalimu alijenga mfumo ambao waliokuwa think tank walikuwa ni viongozi wa Chama na vilevile ni Viongozi wa Serikali.

  Mfumo huu umefanya kazi kwa baadhi ya Mataifa lakini kwa yaliyo mengi mfumo huu umesababisha vifo kwa mataifa husika kufikia mpasuko na kupata Nchi zilizo vipande vipande kama iliyokuwa USSR sasa Russia.

  Kwa kuwa mfumo huu ulikuwa uwe sahihi kama watu wote wangekuwa wanafikilia kwa namna moja.Lakini kwa kuwa watu wote hawafili kwa namna moja basi kwa mfumo huu umekosa nguvu kuiaminisha dunia kuwa ni mfumo bora wa kuleta ustawi wa maisha ya watu wote.Na kama kuna jamii zimefanikiwa kuendelea na mfumo huo basi zile haki za mtu mmoja mmoja ambazo dunia imezitanabaisha kuwa na haki za msingi za kila mwanadamu sehemu ambako mfumo huu unafanya kazi basi Haki hizo zimekandamizwa na kuonekana raia wake wanaendeshwa kidikteta na kunyimwa haki zao za msingi.

  Sio kuwa mfumo huu ulikuwa haufai bali kwa muda na nyakati kulingana na matakwa ya jamii na muda mfumo huu ulikuwa sahihi kwa namna ambayo waliotutangulia waliona inafaa kulingana na kuwa Taifa lenyewe lilikuwa ndio kwanza linazaliwa.

  Mwalimu kupitia mfumo huo alifanikiwa kutuunganisha makabila mia na ushee wote kuwa kabila moja kupitia lugha ya kiswahili.Lakini kupitia Mfumo huo kwa kuwa ni mfumo uliokuwa ukiwajenga wachache waliokuwa kama think tank kwa niaba ya Chama na Serikali.Hivyo majukumu hayo ya kufikilia juu ya Chama na kufikilia juu ya Serikali yakawafanya wale wote waliokuwa ndani ya chama kujiona wana jukumu sahihi ya kuwa wao ndio wenye Dhamana ya Nchi na watu wake.

  Japo kwa muasisi wa mfumo huo,wa ujamaa wa kiafrika yeye binafsi hakuonyesha kuhodhi kofia hizo mbili kwa niaba ya kuwamilki Watanzania na Maliasili zao.Kwa kuwa mamlaka ya JUU ya kuamua mambo ya msingi ya TAIFA yaliwekwa chini ya MAMLAKA YA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

  Kupitia kamati kuu hiyo mambo mengi ya Taifa hili yamaekuwa yakiamuliwa huko.
  Na hapo ndio mwanzo wa mfumo hodhi tatizo lilipoanzia na kulala.

  Kwa kuwa Mwalimu aliamini kuna Wanafunzi [Viongozi wa Sasa] wanalielewa somo ,hakika haikuwa hivyo zama na nyakati ziliwachanganya wakashindwa kutumia formula kupata majibu kwa njia tofauti na mbalimbali.

  Kuja kwa vyama vingi na ujio wa dunia kijiji [Globalizationa] ikiwemo kung'atuka kwa Mwalimu Mkuu kuliwashinda wanafunzi kuchuja mapungufu au makosa na kuyalekebisha kulingana na nyakati na kuwa wabunifu [Creative] wa utawala wa Taifa ndani ya vyama vingi huku wakitengeneza nao viongozi wapya wengine kuja kulithi uongozi.

  Kwa kuwa wafikiliaji wakuu [Think Tank] walikuwa ni wafuasi wa chama,ujio wa vyama vingi ulizalisha chimbuko la waliokuwa vijana ndani ya chama na viongozi watalajiwa wa Chama na Serikali,kuona kuwa wana hati hati ya kupoteza nguvu zao [mamlaka ] ambazo walitayarishwa kuja kutumikia Chama na Serikali.

  Kwa kuwa kimfumo Watanzania walikuwa wamefundishwa kuishi na kuutambua mfumo mmoja wao,na kiimani walishaamini mfumo huo,lakini Mwalimu Mkuu kwa kuona mtaala [Syllabus] huo umepitwa na wakati akaona si vyema kuwalazimisha wanafunzi [Watanzania] wake waendelee kuutumia japo Wanafunzi waliupenda.Kwa kuwa Mwalimu Mkuu alikuwa na uamkini na ubora wa kujua uzuri wa kilicho chema kwa Wanafunzi wake hivyo akasisitiza Wanafunzi waachane na mfumo wa kizamani.

  Walimu [viongozi] walioambiwa kusimamia ubadilishaji wa mitaala kwa kuwa na uchovu na kukosa uwezo wa kujielimisha na kujifunza mitaala ya kisasa na kujua mbinu za Wanafunzi [Watanzania ] wao kuelewa masomo na kuwa na ufahamu wa kuyakabili maisha yao kupitia masomo yaliyotolewa na mitaala mipya, huku wakipaswa kufundisha Wanafunzi [Watanzania] wakitumia silabasi mpya zenye muongozo na kanuni walizo achiwa na Mwalimu Mkuu.

  Yalliyo ya ajabu Walimu walikubali kufundisha silabasi mpya kwa kuigiza huku wakiwa na uchu na dhamila ya kuwadanganya Wanafunzi kuwa wako kwenye silabsi mpya [vyama vingi].Ukosefu wa Ubunifu na Welevu wa kujua umuhimu wa dhamana ya ujenzi wa TAIFA.Walimu ambao ndio viongozi wetu wakamilki hatima ya Ujenzi wa TAIFA kwa kutumia CHAMA.

  Kwa kuwa KOFIA HIZI MBILI ziliendeshwa pamoja viongozi waliokuwa Ndani ya CHAMA wakaendeleza umilki wa DOLA na hivyo kunyima haki TAIFA la kutofautisha CHAMA NA SERIKALI.Kwa kukataa kuvua KOFIA HIZO chama kimeendelea kuwa ndio mzalishaji wa VIONGOZI WA TAIFA.Kwa kuwa CHAMA kinamlengo na itikadi yake hivyo hata wazalishwaji wake wanaendana na itikadi yao ya chama.

  Kwa kutokutoka kwao ndani ya Serikali wamendelea kudumisha,itikadi yao ndani ya Serikali vivyo kutoa tabia ya mazoea ya kichama ndani ya Serikali, kitu hichi ndio zao la viongozi wetu wa sasa.  n
   
 17. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  DSN nakubaliana na wewe ukilielezea tatizo lilipo kwa jicho la kisiasa ambapo unakuta lipo tatizo la mfumo wa siasa (la kimfumo) au tatizo la mfumo wa utawala. Lakini hiyo ni namna moja ya kuliangalia tatizo. Watakuja watu dini watalitazama tatizo kwa jicho la imani zao, nako watakuwa wako sahihi kwa upande/mtazamo wao.

  Turudi kwenye mada. Kwa kutumia elimu ya masuala ya saikolojia, watu waliobobea ktk elimu hiyo wanaweza kutuelezea nini kiini cha haya tunayoyashudia? Kwani sisi tunaona udhihirisho tu, mbegu iko mahala fulani. Watatusaidia kuchimbuachimbua hadi twaweza kupata mizizi kama si kiini.
   
 18. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Je! Ni kwasababu nataka kujua kiini ndiyo maana nashindwa kutulia na kuendelea kuuliza-uliza?Je! Ni kwasababu najua kuwa kuwa babu na babu na mababu zangu walizaliwa na kufa katika nchi ambayo baadaye iliiitwa Tanzania na wengine kufa wakati inaitwa Tanzania; naamini kuwa mimi na watoto, wajukuu na vitukuu vyangu tutajazikwa katika nchi ambayo huko nyuma iliwahi kuitwa Tanzania au itaendelea kuitwa hivyo?Maana sitegemei kuomba uraia wa nchi nyingine ati.
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mwanzoni kabisa, nguvu nyingi zilielekezwa katika azimio la arusha. Sasa walipolitupa, hawakuangalia policy mbalimbali kwa makini. hata Nyerere alitoa mfano wa miiko ya uongozi, na kwamba huwezi kuwa naviongo bora bila vigezo. Mmomonyoko wa maadili unatokana na kukosa refernce za kupima dhana ya uongozi. Sasa hata mwizi wa umma anaweza tu kuwa kiongozi. Mikataba mibovu ya madini ni matokeo tu. Hebu angalia hata suala la katiba lilivyotaka kuchakachuliwa. Ila naamini mambo yote yataanzia katika kurekebisha katiba. Yapo mengi ya kuangaliwa. Hebu jiulize, suala lisilo la muungano linajadiliwa bungeni. Mbunge wa zanzibari anachangia nini katika mjadala huo. Anatakiwa atoke nje. Vivyo hivyo kwanye baraza la mawiziri. Kwanini Tanganyika iuliwe hafu zanzibari ibaki. Hili ni Bomu tu. Katibaaaaaa! Kupewa kazi ya nchi lazima ujiheshimu, serikali korupt mtawaabudu wanye mali, mtaibiwa madini na hata nchi yenu (The mighty Tanganyika). Tanganyika itarudi tu.
   
 20. F

  Fblukuwi Senior Member

  #20
  Aug 13, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo la viongozi wetu linaanzia kwa sisi wananchi. Mathalani kiongozi mwizi kaiba VIJISENTI anapopigiwa kelele hapa Dar anaamua kurudi kijijini kwake na anafanyiwa sherehe kubwa kama SHUJAA na wananchi wanampongeza!!!! Lakini kiongozi huyo angetengwa na jamii nzima ingemdiscourage kuibia wananchi.
  wananchi pia wanachangia kiongozi awe mbaguzi apendelee eneo analotoka na asipofanya hivyo anaonekana hafai Mfano KAWAWA na kusini, Daudi Mwakawago na Iringa na pia jamii inategemea kupata misaada kutoka kwa kiongozi wao mfano ampe kila mtu mwenye shida mbalimbali msaada na hilo linasababisha kiongozi kuwa mwivi kukidhi mahitaji ya wananchi wanaomzunguka.
  Kiongozi anakuwa mwizi pia ili atajirike kuepuka matatizo anapokuwa mzee kwani hakuna mfumo madhubuti wa kusaidia wastaafu wetu hilo linasababisha wazee waliokuwa waaminifu ktk nyadhifa zao WACHEKWE na jamii kuwa walishindwa kujitajirisha walipokuwa viongozi
   
Loading...