Wataalamu wa ndege wanatoa tahadhari kwamba ndege za ATR 72 haziko salama tena kusafiria; Precision Airways bado wanazitumia?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,649
2,000
Katika pitapita yangu ya kupata habari za dunia, nimekutana na habari ambayo imenishitua sana ikisema ndege za ATR ambazo hapa kwetu zinatimiwa na Precision Airways si salama tena kusafiria, na hata sasa zinaingizwa katika orodha ya ndege mbaya duniani zilizowahi kutengenezwa (the worst planes that have been made). Na hata inasemwa kwamba mashirika mengine yameachana na ndege hizi.

Juzi hapa nimeona katika maeneo ya Njombe na Makete kulikuwa na theruji, na inasemekana kwamba ndege za ATR 72 ni hatari sana kukiwa na hali ya theruji ambayo ni rahisi kutokea anga za juu za maeneo yenye baridi kama nyanda za kusini hapa nchini (icing on the wings).

Nadhani hili ni suala linalohitaji majibu kutoka serikali yetu na Precision Airways wenyewe. Habari niliyokutana nayo ni hii hapa chini

The ATR 72

Before American Eagle retired the ATR 72, Alex Murel warned people not to fly on this plane. “Its massively outdated, and the existing fleet is really starting to fall apart,” he explained. “I understand that turboprops can be more cost-efficient for some flights, but these are old and feel like they’re shaking the plane apart. 11 of the 508 built have been destroyed in crashes that resulted in the deaths of over 190 people.”

The ATR 72

Source: The Worst Planes That Have Been Made | Page 34 of 48 | DailySportX

Comment nyingine:

The safety record is very good for a plane of the type - of course now the design is getting aged ( the ATR 72 entered service in 1989). The plane's safety record was excellent until 2009, with only three notable accidents, however between 2009 and 2013 there have been 9 notable accidents.
 

Kitanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
276
250
In maana mamala ya Tanzania zinahusika na usafri wa anga/ dnege hazina taarifa hii au hadi litokee janga ndiyo hatua zichukuliwe?!
 

rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,780
2,000
Acha hizo ATR72 Precision wanazo pia ATR 42 na jeshi letu bado tuna ndege za Kirusi MIG21 ambazo ni toleo LA mwaka 1959 na bado zinafanya kazi na hizo ndo zilimtoa Amin
 

Jamiix

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
839
500
Tatizo nnalo liona hapa kwenye uzi huu ni "LUGHA",kilichoandikwa kwa lugha ngeni na kilicho tafsiriwa kua lugha ya kiswahili havishahabiani kabisa,
96% ya wa TZ wanashindwa tofautisha kati ya "OPINION,REALITY and FACTS".
97% yetu tunasoma ku "REPLY" na sio ku "UNDERSTAND".
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom