Tafsiri halisi ya neno Mswahili

bbtwins

New Member
Sep 1, 2010
3
1
Nilipata kumsikia mtu akisema hangependa aitwe "mswahili". Nikapatwa na maswali mengi kichwani kwani mtu huyu alikua mzawa, mweusi na anaishi DSM.

Kabla sijamtaka undani kwa kauli yake hii, nilidhani uswahili ni title ya mtu mwenye ngozi nyeusi na anayeishi au anayetoka kwenye jamii ya watu wa mwambao. Baada ya kuongea na huyu mtu, niligundua kuwa hata mzungu na watu wa bara wanaweza kuwa waswahili!

Kinachomfanya mtu awe mswahili kumbe ni "hulka" - kubwa mbili zikiwa (1) kuongea zaidi ya matendo na (2) kujifanya kujua kila kitu.

Kwa mtizamo huu, Tanzania tuna waswahili kibao, Tutafika kweli?

========================
Samahani wanaJF, hivi Mswahili ni nani?

Kwa nijuavyo, mswahili ni mtu anaejua kiswahili na anayeongea sana maneno mazuri mazuri yenye ahadi nzuri nzuri ambazo hazitekelezi, yaani ana uongo mwingi kuliko ukweli.

Baadhi ya wabara wakifika pwani hujaribu kuiga uswahili na wengine wanafanikiwa kuwa waswahili wazuri!!

Kwa jumla, waTZ wengi wana uswahili kuliko waKenya na waGanda. Ndiyo maana sisi waTZ tuna maneno mengi kuliko vitendo!! Siasa siasa tu zisizo tafsirika katika vitendo!! Matokeo yake tuko nyuma kimaendeleo licha ya juwa na raslimai nyingi majirani zetu!!

Tuache uswahili ili tuendelee!! Tuache kuongozwa na waswahili!!

SAMAHANI KWA NILIOWAKWAZA!!

Asubuhi njema!!
========================
Wanajf naomba tu share changamoto niliokutana nayo. Leo asubuhi nikiwa kwenye daladala naelekea mjini kati. Baada ya kuwaza na kuwazua, karibu yangu alisimama mtoto wa kike I think she is at 7 or 8 aliyekuwa amevaa sare za shule.

Kwa kuhisi kuwa yuko embarased kutokana na foleni, nikaamua kum keep bize kwa kumpa recognition kwa kumuuliza maswali ya kitoto ya hapa na pale ali mradi tu tufike bila ya uchovu. Unaishi wapi, Unaitwa nani, unasoma shule gani na darasa la ngapi. Nikamuuliza huku nikiwa sina uhakika kama nitajibiwa vizuri swali langu. Nilishtushwa na uwezo mkubwa wa kujieleza baada ya kujibu kwa ufasaha maswali yangu ya mpigo. Du!! Nikajiona Chief mzima napigwa TKO kutokana na jibu la mtoto kwani wahenga walisema kuwa jibu likisadifu swali, ni kama kiu iliyokatwa kwa maji safi ya kisima cha chemchem.

Mtu mzima sikutaka kushindwa kirahisi.nikamuuliza swali lingine ambalo niliamini kuwa litamsumbua kutokana na umri wake. " Umesema unaishi Kimara, Wewe ni kabila gani?" Huku nikitegemea jibu la "Mimi ni Mchaga" kutokana na maeneo mengi ya Kimara kugeuzwa kuwa mashamba ya Migomba kutokana na kukaliwa na Wachaga wengi, nilishangaa kusikia jibu alilolitoa yule mtoto. Kwa kujiamini alijibu "Mimi ni Mswahili" Huku nikiwa siamini masikio yalichosikia, nikamuuliza tena. "Umesema wewe ni kabila gani?" Akijibu kwa msisitizo na kujiamini, alisema "Mimi ni Mswahili" Nikajiona Chief mzima leo ninalo.

Nikajitutumua na kuuliza tena. "Kwa nini unasema wewe ni Mswahili. Kwani baba yako ni kabila gani." Kwa kujiamini akajibu. "Baba yangu ni Mhehe na Mama yangu ni Msukuma. Na kwa kuwa wazazi wangu ni makabila tofauti, mimi ni Mswahili kwa kuwa sifuati mila yoyote wala situmii lugha yoyote ya wazazi wangu zaidi ya Kiswahili".

Ghafla nikasikia sauti ya Konda, "Akiba wa kushuka". Nikajibu "tupo" bila ya kujali kuwa sikutumwa na mtu yeyote kumjibia. Nikashuka zangu huku nikijiuliza MSWAHILI NI NANI?
=============================
Habarini wadau,

Kwa kawaida neno mswahili limekuwa likitumiwa kumaanisha haya

-Mtu wa hali ya chini (kiuchumi) na anayeishi uswahilini

-Pia mara nyingine humaanisha mtu ambaye ana sound nyingi au muongomuongo,utaskia "Acha uswahili wewe"

-Pia watu wengi wa mikoani (especcially wakristo) wanawachukulia waswahili ni waislam wa pwani,Dsm na hata zanzibar

-Lakini pia watoto wa mjini wanawachukulia mswahili ni mjanja mfano utaskia "Mimi ndio mtoto wa kiswahili/kiswazi huwezi niingiza kingi"

SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?
=========================
Nilipata kumsikia mtu akisema hangependa aitwe "mswahili". Nikapatwa na maswali mengi kichwani kwani mtu huyu alikua mzawa, mweusi na anaishi DSM.

Kabla sijamtaka undani kwa kauli yake hii, nilidhani uswahili ni title ya mtu mwenye ngozi nyeusi na anayeishi au anayetoka kwenye jamii ya watu wa mwambao. Baada ya kuongea na huyu mtu, niligundua kuwa hata mzungu na watu wa bara wanaweza kuwa waswahili!

Kinachomfanya mtu awe mswahili kumbe ni "hulka" - kubwa mbili zikiwa (1) kuongea zaidi ya matendo na (2) kujifanya kujua kila kitu.

Kwa mtizamo huu, Tanzania tuna waswahili kibao, Tutafika kweli?
 
Wanajf naomba tu share changamoto niliokutana nayo. Leo asubuhi nikiwa kwenye daladala naelekea mjini kati. Baada ya kuwaza na kuwazua, karibu yangu alisimama mtoto wa kike I think she is at 7 or 8 aliyekuwa amevaa sare za shule.

Kwa kuhisi kuwa yuko embarased kutokana na foleni, nikaamua kum keep bize kwa kumpa recognition kwa kumuuliza maswali ya kitoto ya hapa na pale ali mradi tu tufike bila ya uchovu. Unaishi wapi, Unaitwa nani, unasoma shule gani na darasa la ngapi. Nikamuuliza huku nikiwa sina uhakika kama nitajibiwa vizuri swali langu. Nilishtushwa na uwezo mkubwa wa kujieleza baada ya kujibu kwa ufasaha maswali yangu ya mpigo. Du!! Nikajiona Chief mzima napigwa TKO kutokana na jibu la mtoto kwani wahenga walisema kuwa jibu likisadifu swali, ni kama kiu iliyokatwa kwa maji safi ya kisima cha chemchem.

Mtu mzima sikutaka kushindwa kirahisi.nikamuuliza swali lingine ambalo niliamini kuwa litamsumbua kutokana na umri wake. " Umesema unaishi Kimara, Wewe ni kabila gani?" Huku nikitegemea jibu la "Mimi ni Mchaga" kutokana na maeneo mengi ya Kimara kugeuzwa kuwa mashamba ya Migomba kutokana na kukaliwa na Wachaga wengi, nilishangaa kusikia jibu alilolitoa yule mtoto. Kwa kujiamini alijibu "Mimi ni Mswahili" Huku nikiwa siamini masikio yalichosikia, nikamuuliza tena. "Umesema wewe ni kabila gani?" Akijibu kwa msisitizo na kujiamini, alisema "Mimi ni Mswahili" Nikajiona Chief mzima leo ninalo.

Nikajitutumua na kuuliza tena. "Kwa nini unasema wewe ni Mswahili. Kwani baba yako ni kabila gani." Kwa kujiamini akajibu. "Baba yangu ni Mhehe na Mama yangu ni Msukuma. Na kwa kuwa wazazi wangu ni makabila tofauti, mimi ni Mswahili kwa kuwa sifuati mila yoyote wala situmii lugha yoyote ya wazazi wangu zaidi ya Kiswahili".

Ghafla nikasikia sauti ya Konda, "Akiba wa kushuka". Nikajibu "tupo" bila ya kujali kuwa sikutumwa na mtu yeyote kumjibia. Nikashuka zangu huku nikijiuliza MSWAHILI NI NANI?
 
Kazi kweli kweli, dunia hii sio ile ya miaka ile watoto sasa wamegeuka kuwa wakubwa leo hii mtoto wa chini ya miaka 18 ana uwezo kuliko hata mzee wa zaidi ya miaka 45 na ndio maana akakujibu yeye ni mswahili.
 
Mkuu,

Kwa kusoma thread nyingi hapa JF, mswahili ni mvaa "baragashia".

Kwa kihistoria, kiasili, mswahili ni mtu wa pwani ya Afrika mashariki, mtu wa mwambao na lugha yake ni kiswahili.Kiswahili huwa ndio lugha mama kwake, hana lugha nyengine. *Anaweza kusoma lugha nyengine shule au mitaani.

Kwa tafsiri ya kileo, mswahili ndiyo kama huyo aliyekupa jibu lililokuchangamsha.

Kwa hiyo wapo waswahili wa asili na waswahili wa kujipa na waswahili wa kuja!
 
Mkuu, kwa kusoma thread nyingi hapa JF, mswahili ni mvaa "baragashia". kwa kihistoria, kiasili, mswahili ni mtu wa pwani ya Afrika mashariki, mtu wa mwambao na lugha yake ni kiswahili.Kiswahili huwa ndio lugha mama kwake, hana lugha nyengine. *Anaweza kusoma lugha nyengine shule au mitaani. Kwa tafsiri ya kileo, mswahili ndiyo kama huyo aliyekupa jibu lililokuchangamsha. kwa hiyo wapo waswahili wa asili na waswahili wa kujipa na waswahili wa kuja!
Kwa jibu la yule mtoto, it means tafsiri unayoeleza imeshapitwa na wakati.
 
HAHAHAHHAHA LOL watoto bwana...

You know wewe ni mswahili kama unafanya hizi vitu

1. You talk too much.

2. You sleep at the airport just to wait and catch a glimpse of Drogba with the Ivory coast team.

3. To board a bus in the evening you climb through the window to get a seat even when the bus is just half full.

4. You greet someone in more than 10 different ways before... getting to the point on what you wanted to say.
 
HAHAHAHHAHA LOL watoto bwana... You know wewe ni mswahili kama unafanya hizi vitu 1. You talk too much. 2. You sleep at the airport just to wait and catch a glimpse of Drogba with the Ivory coast team. 3. To board a bus in the evening you climb through the window to get a seat even when the bus is just half full. 4. You greet someone in more than 10 different ways before... getting to the point on what you wanted to say.
No thank u. I disagree with u. Do u mean,also those fisadis are also waswahili?
 
Baba wa Taifa alituasa tusiulizane makabila, wewe kwa nini ulitaka kujua kabila la mtoto?

Anyway, nafikiri jibu sahihi linategemea na mazingira ambayo hilo swali linaulizwa. mfano ukiwa nje ya nchi kama zambia, mswahili atakuwa ni mtu anayeongea kiswahili kama lugha yake ya asili siyo ya kujifunza shule

Ukiwa Tanzania mikoa ya nyanda za juu kusini au kanda ya ziwa, mswahili ataelezewa kuwa ni mtu wa pwani
Ukiwa maeneo ya pwani kama DSM mswahili atatambuliwa kwa tabia zake nafikiri zinafahamika
 
Kwa tafsiri fasaha mswahili ni mtu anayeishi katika utamaduni, lugha ya kiswahili, hapo zamani ilikuwa ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki, sas ni eneo zima la Afrika Mashariki na Kati ikiunganisha na Somalia, Sudan Kusini, Comoro n.k hiyo ndio tafsiri rasmi ya Mswahili
 
Chief kuwa makini hizo ni dalili za ufataki, watoto wa siku hizi hawadanganyiki!
 
Back
Top Bottom