Wataalamu wa hesabu, ninaombeni ufafanuzi wa hivi vipimo vya shamba

Arnold Ndosi

Member
Aug 14, 2012
65
3

Wadau wa jamvi hili, habari zenu?


Ninaomba msaada wa ufafanuzi wa hili tatizo langu la kimahesabu--mwenzenu sipo vizuri sana kwenye hesabu ila nina imani kuwa hapa kuna wadau wanaoweza kunipa ufafanuzi:


Kuna rafiki yangu anataka kununua shamba heka nne na kaniomba nimsaidie kusimamia mchakato wa vipimo ili viwe sahihi kabisa.


Shamba linalouzwa lina umbo la herufi "L". kwenye mstatili wa kwanza, ambao ndio mrefu zaidi umepimwa lakini ukapela kidogo kutimia hizo heka nne zinazohitajika. Hapo sasa ndipo mahesabu yanapohitajika.


-Kilichopimwa kina urefu upatao mita 130 na upana mita 107


-Huwa heka moja ina urefu wa mita 70 na upana mita 70


-Kwa maana hiyo, heka nne zinahitaji urefu wa mita 140 kwa upana wa mita 140.


-hata hivyo, tunafahamu fika kuwa eneo lilipelea ni mita 10 x 140 +mita 33 x 140 (kama sijakosea)


- kipande cha pili cha shamba hilo hakijapimwa lakini ni kikubwa sana hivyo tunaamini kinaweza kutoa eneo kubwa zaidi ya hilo lililopelea.


-Vibaya ni kwamba eneo la kipande ambacho hakijapimwa hakina urefu wala upana utakaofikia mita 140 kwa hiyo kupima kunaleta ugiligili na ukakasi wa hali ya juu.


-Ninaomba mnisaidie kukokotoa kutafuta square meter za eneo lililopelea na kuzitafutia urefu na upana wake (lakini hizo mita za urefu na upana zibalansiwe zisiwe ndefu ama pana sana, angalau ziwe katika misingi ya vipimo vya mita around 70, yaani urefu na upana ili tuweze kupima hilo eneo ambalo siyo refu wala pana sana.



NB.

-Kama kuna jinsi nyingine ambayo mtaona ndio sahihi zaidi kulipima hilo eneo, ninaomba ufafanuzi wenu.


-Wauzaji wako shalo kwenye masuala ya vipimo na mahesabu hata kuliko mimi kwa hiyo ninaomba ufafanuzi mwepesi sana



Asanteni sana,

Ndosi.
 

Attachments

  • shamba.jpg
    shamba.jpg
    31.6 KB · Views: 257
Si kweli kwamba ekari moja ni Mita 70×70

Ekari moja ni approximately mita 63.2×63.2.
Hii ni approximately hatua za miguu 70 kwa 70.
Ekari moja ni mita za mraba 4000.
Eneo ulilopewa la mita 107 kwa mita 130 lenye umbo la mstatili, linatoa mita za mraba 13910 ambazo ni kama ekari tatu unusu (13910÷4000=3.47).

Unachohitaji kupimiwa zaidi ni eneo la mraba la mita 45.7 kwa 45.72 ili kupata eneo lililopwelea la mita za mraba 2090, ili ufikishe jumla ya mita za mraba 16,000 ambazo zitakupa ekari nne kamili.

Natumaini kwenye maelezo yako ulipoandika heka ulimaanisha ekari (acre) na sio hekta (hectare). Fahamu kuwa: 2.5 acres = 1 hactare = mita za mraba 10,000.
 
Back
Top Bottom