Wataalamu wa China wamethibitisha kuwa dawa ya Malaria aina ya Chloroquine Phosphate ina ufanisi wa kutibu ugonjwa wa COVID-19

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,757
4,305
Clor Ph.jpg

Wataalamu wa China wamethibitisha kuwa dawa ya Malaria aina ya Chloroquine Phosphate ina ufanisi wa kutibu ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na virusi vya Corona COVID-19.

Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Maendeleo ya Teknolojia ya Viumbe kilicho chini ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China Bibi Sun Yanrong, amesema wataalamu wamependekeza kuiweka dawa hiyo kwenye mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa huo na kufanya majaribio zaidi ya dawa hiyo kwa binadamu haraka iwezekanavyo.

Dawa ya Chloroquine Phosphate ambayo imetumiwa kwa zaidi ya miaka 70 kutibu ugonjwa wa Malaria, imechaguliwa miongoni mwa mamia ya maelfu ya dawa zilizopo baada ya kufanyiwa majaribio.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, dawa imeanza kufanyiwa majaribio kwa wagonjwa katika hospitali zaidi ya kumi mjini Beijing na katika mikoa ya Guangdong na Hunan, na imeonesha ufanisi dhidi ya virusi vya korona. Amesema wagonjwa zaidi ya mia moja waliotumia dawa hiyo wamepona haraka zaidi na mpaka sasa hakuna madhara au athari hasi zilizoripotiwa kutokana na matumizi ya dawa hiyo.

Chanzo: CRI Swahili
 
FEBRUARI 20 2020

Beijing, China. Dawa ya malaria aina ya chloroquine imedhibitisha kutibu virusi vya corona (covid-19)

Dawa hiyo iliyokuwa ikitumika zaidi kutibu ugonjwa wa malaria katika miaka ya 1980 na 1980 imeonyesha kutibu virusi hivyo baada ya kufanyiwa utafiti na wataalam wa afya wa nchi hiyo.

Wizara ya Afya sayansi na teknolojia ya China, ilisema “chloroquine imethibitisha inaweza kutibu corona lakini pia ikakinga ugonjwa wa maralia kwa miongo kadhaa sasa.”

Shirika la habari la Xinhua limeripoti kuwa chloroquine imekuwa ikitumika kwa zaidi ya hospitali 10 ikiwamo moja iliyopo katika mji mkuu wa Beijing na mbili katika majimbo mengine.

Kwa mujibu wa Xinhua dawa hizo zimeonyesha ufanisi mzuri.
 
Dawa ya malaria aina ya chloroquine imedhibitisha kutibu virusi vya corona (covid-19)

Dawa hiyo iliyokuwa ikitumika zaidi kutibu ugonjwa wa malaria katika miaka ya 1980 na 1980 imeonyesha kutibu virusi hivyo baada ya kufanyiwa utafiti na wataalam wa afya wa nchi hiyo.

Wizara ya Afya sayansi na teknolojia ya China, ilisema “chloroquine imethibitisha inaweza kutibu corona lakini pia ikakinga ugonjwa wa maralia kwa miongo kadhaa sasa.”

Shirika la habari la Xinhua limeripoti kuwa chloroquine imekuwa ikitumika kwa zaidi ya hospitali 10 ikiwamo moja iliyopo katika mji mkuu wa Beijing na mbili katika majimbo mengine.

Kwa mujibu wa Xinhua dawa hizo zimeonyesha ufanisi mzuri.

Credits: Mwananchi Newspaper

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom