Wataalamu wa ardhi, ni sahihi kumiliki ardhi kwa kutumia hati miliki ya kimila kwenye sehemu yenye mchanganyiko wa makabila?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,974
13,614
Kwa mfano, mji kama DSM, ni sahihi kutoa hati miliki ya kimila kumiliki ardhi? Maana kuna makabila karibia yote ya hapa nchini mjini dsm.

Utoaji wa hati miliki unazingatia mambo gani? Mimi nilidhania hati miliki ya ardhi ya kimila hutolewa pale inapoonekana eneo husika lina kabila, tamaduni, na desturi moja.

Mfano mzuri ni mkoa wa Kilimanjaro, haswa eneo linalokaliwa na wachagga. Kwa asilimia kubwa ardhi kubwa inayokaliwa na wachagga inamilikiwa kimila japo wengi hawana hati miliki.

Naomba kujua, ni maeneo gani ambayo yanafaa kumilikiwa kwa kutumia hati miliki ya kimila?
 
Back
Top Bottom