Wataalamu wa ac (AIR CONDITION)mje huku

laii

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
834
1,058
Habari wadau,nataka kufunga ac kwa ajili ya matumizi ya ofisi, kuwashwa ni kila siku kuanzia saa1 kamili mpaka saa 4 usiku.

Nilikuwa naomba kujua faida na hasara ya ac used na mpya.Kuanzia kudumu, matumizi ya umeme, maintanance. Nawakilisha.
 
hakuna hasara kwa AC zaidi ya kupata raha na mazingira mazuri ya kufanya kazi hasa kwa nchi zetu za joto hizi
 
Huwezi linganisha mpya na iliyotumika labda uwe na mtindio wa ubongo!

Kabla ya kuwa Used ilikuwa mpya!

Hivyo mpya hairinganishwi na kukuu!

Kwasababu ubora wa kuukuu hutegemea matunzo ya mtumiajji wa kwanza toka upya!
Uchakavu wa coil, pipes na compressor vyote hupelekea ubovu wa AC!

Miongoni mwa ubovu ni pamoja na kuvuja kwa gesi inayopelekea kushindwa kutoa ubaridi unaotakiwa!

Changamoto nyingine ni kukosa usawa wa indoor unit na out door unit!
AC za mitumba nyingi zimefanyiwa matengezo kwa kuwekwa Vifaa vyenye uwezo tofauti na capacity ya AC husika!

Changamoto ya tatu AC za zamani nyingi hazikuwa na mfumo wa energy saving kama zinazotoka sasa hivyo wengi wanaondoa za zaman ili kubana umeme
Changamoto ingine AC za zamani ni air pollutants zina makelele kuliko mpya

Changamoto nyingine, ni aina ya gesi ya sasa ni mpya, hivyo kuendelea kutumia AC la kizaman hasara yake likivuja gesi, itakugharimu sana kuitafta gesi ya zamani itakayokuwa imeondolewa sokoni!
Kwa mawasiliano na huduma nione!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom