Wataalamu tupeni ujuzi kuhusu specifications za Simu na TV

chilali

Member
Feb 25, 2019
51
19
Kama kichwa kinavyoo jieleza hapo juu wengi wetu hutoka kapa na kujikuta tunaishia kubambikwa tu, ukishatumiwa bidhaa unakuta kinyume na mategemeo yako.

Mfano: Resolution 1080p, battery 1000ahm,gps,inch 9.5,Ram 5,6mega pixel,Android 7.1 na vingine vingi.Mnisamehe kwa hizo specification maana duuuuh nahisi kuboronga mno.
 
hiyo ndio tunaita sifa za simu.

resolution=hiyo uwezo wa kioo kuonyesha picha kubwa na bora zaidi jinsi namba zinavyokuwa ndio kioo ni bora zaidi.

Display inch=huo ni upana na urefu wa kioo,namba inavyozidi kuwa kubwa maana yake simu ni pana zaidi.

Megapixel=hiyo baba ni ukubwa wa picha itakayopigwa,pixel zinavyokuwa nyingi picha linazidi kuwa kubwa.mfano mp 64 za tecno zinazalisha picha la mb kama 15 hivi,ila wingi wa pixel hauhusiani na ubora wa picha.

Android vasion=hiyo nikama suti ambayo inatumika kila mwaka una ya kwake,ikiwa na lengo la kuviongezea vifaa ulinzi,wepesi na hata muonekano mzuri,kuna IOS pia nayo ni nyingine katika namna hii hii.

Mah 1000=huo ni ukubwa wa betry.linavyozidi kuwa kubwa kwa namba maana yake ni kubwa zaidi,linakaa zaidi na charge ila si mara zote.

RAM=hiyo ni kama ubongo wa mbele wa simu,unahusika na shughuli zote za simu,ni kama jikoni,inavyozidi kuwa kubwa ndio nafasi ya simu kuwa nyepesi na nguvu inawezekan.

Storage=hii ndio ghala sasa ya kutunzia mazaga zaga yote,utatunza mapicha video nk,linavyozidi kuwa kubwa ndio nafasi ya kuweka vitu vingi zaidi inapatikana.

Prosessor=hiyo ni kama kichwa cha simu akina ram,storage na utumbo mwingine unaofanya simu kuwa na akili unapatikana hapo ndani.zinapishana ubora pia zinasabisha simu kupishana bei.
 
Nakusaidia kwenye TV

Resolution
Hii ni Urefu na upana wa kioo chako kwa kuzingatia Pixel na sio Dimension yaani Urefu na upana in metrics.

Video inavyorekodiwa/ kutengenezwa, kamera husetiwa kwa kuzingatia resolution
Mf. Unataka video ya Full HD. Hii ina 1080i

Kwa hiyo wakati wa kununua TV lazima ujue unahitaji ubora wa picha kiasi gani ili uweze kupata.

Sasahivi kuna 4K resolution au Utra High definition yaani UHD. Ambapo upana wa video unafikia 3500+ pixels ambayo ni picha nzuri sana na very clear.

Ila hapo cha kuzingatia ni kwamba lazima content yako iwe sawa na TV yako.

Mf. Kama una TV ya 4k basi hakikisha una Video ya 4K otherwise uwe na Video upsacaler ndio unaweza tumia kutazama content za resolution ya Chini.

Au mnasemaje mods wa JF
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom