Wataalamu tunao, tunawadharau

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,530
Je Utabiri wa hali ya hewa ulipotamka mwaka 2002 kuwa kutakuwa na uhaba wa mvua, kwa nini Serikali ilipuuzia au ilifanya mambo yanayoonekana kana kwamba walipuuzia ushauri huo?

Wakati tunapata sakata la umeme na Richmond, tulikuwa na njaa na kukimbilia kuomba misaada. Sasa ikiwa Hali ya Hewa waliwasilisha ripoti Serikalini, kwa nini haikufanyiwa kazi?

Wanasema Kinga ni bora kuliko tiba, Mhita alitupa maono ambayo yangetupa kinga na kutuondoa kwenye adha iliyotokea kama tungedamka na kufanya kazi ipaswavyo, kwa nini tunaendelea kukimbilia kutibu na kuweka viraka na si kujijenga na kuweka kinga?

Je ikiwa wataalamu wetu wataendelea kupuuzwa, wakienda Lesotho ni nani wa kulaumiwa?

Je hivi ndivyo serikali yetu ilivyo?

http://www.raiamwema.co.tz/08/03/05/3.php

Richmond yaibukia Uganda

lC.gif
Waandishi Wetu​
Machi 5, 2008
rC.jpg

SAKATA ya kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development LLC, ya Marekani, limevuka mipaka na kujadiliwa nchini Uganda katika mkutano wa wataalamu wa hali ya hewa, ambao wanasema kwamba Serikali ya Tanzania haikuzingatia ushauri wa wataalamu kwa wakati.
Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) amelieleza RAIA MWEMA kwamba, sakata hilo limeibuka baada ya kuwapo taarifa kwamba Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, ilizingatia taarifa za wataalamu wa hali hewa.
“Wataalamu na wadau walioshiriki mkutano uliofanyika Entebbe, Uganda, waligusia suala la Richmond kwa kuwa ni wao waliotoa taarifa za mfululizo kuanzia mwaka 2002 wakitahadharisha kuwapo kwa ukame katika maeneo mbalimbali ikiwamo sehemu kubwa ya Tanzania lakini wakashangaa kusikia suala hilo kwa Tanzania lilionekana kuwa la dharura,” alisema ofisa huyo.
Katika ripoti yake bungeni, Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, iliweka bayana kwamba serikali inapaswa kuzingatia taarifa za wataalamu wakiwamo wa hali ya hewa ili kuepuka kufanya mambo kwa mtindo wa dharura kama ilivyokua kwa suala la Richmond.
Kamati hiyo katika uchunguzi wake, Desemba 5, 2007 ilimhoji Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Mohamed Mhita, ambaye alibainisha wazi kwamba kamati yake imekuwa ikiwasilisha serikalini taarifa zote na baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikinukuliwa vizuri katika vyombo vya habari.
Alipoulizwa wanakopeleka taarifa zao, Dk. Mhita alieleza kamati hiyo kwamba wanapeleka katika idara zote serikalini ikiwa ni pamoja na Ikulu (kupitia Idara ya Usalama wa Taifa), Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo na pia kupeleka moja kwa moja kwa watumiaji wengine na wananchi kupitia vyombo vya habari.
Dk. Mhita alibainisha pia kwamba mbali ya kuwasilisha taarifa hiyo, wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja katika hatua zote na wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu ambao imefahamika kwamba wamekuwa wadau wakubwa wa TMA wakati wote.
Maelezo hayo ndiyo yaliyozingatiwa pia na washiriki wa mkutano wa kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Machi hadi Mei mwaka huuu, wakisikitishwa na jinsi Serikali ya Tanzania ilivyopatwa na mtikisiko katika jambo ambalo halikupaswa kuwa la dharura.
Ofisa mmoja wa TMA aliliambia RAIA MWEMA jana Jumanne kwamba taarifa iliyotolewa na wataalamu Machi 2005 na ile ya Septemba mwaka huo, iliikuta Serikali nzima ikiwa katika joto la Uchaguzi Mkuu huku baadhi ya wataalamu nao wakiwa washiriki wakuu wa harakati hizo kwa namna moja au nyingine ambao walikuwa wametelekeza ofisi zao.
“Taarifa tulizozitoa Machi 2005 na ile ya Septemba 2005 zilizoelezea bayana kuwapo kwa upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi, ziliwakuta viongozi na watendaji wetu wakiwa busy (katika harakati) za uchaguzi na walipokuja kuzinduka ilikua Februari 2006 wakati mambo yamekwisha kuharibika na hakuna mtu aliyekumbuka taarifa,” alisema.
Ofisa huyo ambaye amewahi kushiriki mikutano mingi ya hali ya hewa, aliliambia RAIA MWEMA kwamba pamoja na udhaifu wao mwingi wa kiutendaji na kimaadili, rais mstaafu, Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu wake, Frederick Sumaye, walizingatia taarifa za utaribiri za mwaka 2003 na 2004 kwa kutenga fedha na mikakati ya kukabiliana na ukame ulioikumba nchi mwaka 2004.
“Mwaka 2004 hata Bwawa la Mtera lilifungwa kwa muda lakini hakukua na mgawo wa umeme na wananchi hawakupata shida ya chakula baada ya Serikali kuwasilisha bungeni maombi ya fedha za ziada ambazo zilitumika kuisaidia Tanesco na Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR) kwa hiyo Serikali mpya ilijikuta haijajipanga ilipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2005 na mwanzoni mwa 2006. Nadhani hili ni fundisho kubwa kwetu,” anasema.
Katika Mkutano wa Entebbe, pamoja na kutabiriwa kuwapo mvua za wastani katika maeneo mengi ya nchi, bado kuna hatari ya kuwapo uhaba mkubwa wa mvua kutokana na kuwapo kwa mabadiliko makubwa ya joto katika Bahari ya Pacific inayoashiria kuwapo kwa hali ya La Niña, ambayo husababisha upungufu mkubwa wa mvua katika maeneo mengi ya Pembe ya Afrika, Tanzania ikiwamo.
Sakata la Richmond lilisababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili, waliowahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini iliyoshiriki katika mchakato wa zabuni ya mradi wa Richmond. Mawaziri hao, Dk. Ibrahim Msabaha, ambaye alikwisha kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na aliyechukua nafasi yake, Nazir Karamagi.
Katika utetezi wao, wote watatu walielezea hali ya udharura kama sababu ya msingi ya kuharakisha bila umakini kuingia mkataba wenye utata na kampuni ya Richmond Development LLC, ambayo haikuwa na uhalali wa kisheria kuwapo nchini, na ambayo ilibainika kutoa taarifa za uongo kwa Serikali na umma kupitia nyaraka na tovuti.
Pamoja na kujiuzulu kwa wanasiasa hao, Serikali imekuwa katika shinikizo kubwa la kutakiwa kuwachukulia hatua watendaji wake walioshiriki kuibeba Richmond na mrithi wake Dowans ya Falme za Kiarabu na hatimaye kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika wakiwamo wanasiasa waliojiuzulu.
 
Serikali (viongozi) wetu ni reflection yetu sisi wenyewe. Kwa hiyo kama serikali (viongozi) ndivyo ilivyo basi na sisi ndivyo tulivyo except Mwanakijiji.
 
Serikali (viongozi) wetu ni reflection yetu sisi wenyewe. Kwa hiyo kama serikali (viongozi) ndivyo ilivyo basi na sisi ndivyo tulivyo except Mwanakijiji.

Sio kweli, sio kwamba kwa sababu viongozi watatoka kwetu basi ndo kiwe kigezo cha kujaji, kuwa ni reflection yetu, Hapana

Na likataa hilo kabisa, viongozi wengi wamekuwa wakipata uongozi wanakimbilia kuangalia maslahi binafsi badala ya kuwaangalia wananchi, wanakuwa na tamaa za kutaka kuwa matajiri wakisahau, heshima sio pesa zako bali ni utu wako kwa jamii

Kumbuka kikwete alivyokuwa akiongea kwenye Kampeni zake za 2005, Nanukuu kampeni zake za mwisho pale jangwani, "Nitapigana kwa hali na mali na kuhakikisha kila mtanzania anapata maisha bora, na mungu anisaidie" je haya kikwete ndo mapigano haliyowambia wananchi, na je sio kwamba halikuwa kajivalisha ngozi ya kondoo kumbe naye ni fisi??
Maswali ni mengi kwa mtu kama kikwete aliyeaminiwa na watanzania, lakini leo hii anaishia kuunda kamati tu za kinafiki na zisizo kuwa na ukweli wowowte, Kama mwenye kumbukumbu za kutosha kamati nyingi sana zimeundwa, na zilizowasilisha repot ni chache sana zingine zinaishia hewani tu

Kikwete ndo anatumalizia kabisa, Mkapa alitudidimisha, tukawa na matumaini kwa kikwete, lakini the Guy in non sense kwa watanzania, yupo kwa ajili ya kutafuta pesa za familia yake badae
 
Kwa hiyo kulingana na uliyoyasema nategemea Kikwete na genge lake watakataliwa kabisa na wananchi ambao hawana mchezo ifikapo 2010 kwenye uchaguzi mkuu vinginevyo bado nitaamini sisi ndivyo tulivyo na viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe.
 
Nyani, kwanini unasahau kwamba CCM kwa kutumia vyombo vya dola, polisi, jeshi n.k. wanaweza kabisa kuiba uchaguzi pamoja na kuwa hawakushinda katika uchaguzi huo? Wameshawahi kuiba chaguzi mara nyingi tu, je ni kipi kitakachowazuia kufanya hivyo tena hapo 2010?
 
Sasa kama wana uwezo wa kuiba ndio basi hatuna jinsi zaidi ya kuwapigia kura? We huoni tukifanya hivyo ndio tunazidi kudhihirisha kuwa ndivyo tulivyo?
 
Kwa hiyo kulingana na uliyoyasema nategemea Kikwete na genge lake watakataliwa kabisa na wananchi ambao hawana mchezo ifikapo 2010 kwenye uchaguzi mkuu vinginevyo bado nitaamini sisi ndivyo tulivyo na viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe.

Nyani, wewe binafsi unafanya juhudi gani za kuhakikisha kuwa haitachaguliwa tena 2010 au kwa vile "ndivyo ulivyo" umeamua kukubali tu yaishe?
 
Nyani, wewe binafsi unafanya juhudi gani za kuhakikisha kuwa haitachaguliwa tena 2010 au kwa vile "ndivyo ulivyo" umeamua kukubali tu yaishe?

Nitapiga kura na CCM haitapata kura yangu iwe kwenye uraisi au ubunge. Na ninachofanya hapa jamboforums ni kuinua awareness ya uchafu unaofanywa na CCM kwa kuchokoza conscience na kuchokonoa akili zenu kwamba tukiendelea kuwachagua hawa watu basi sisi tutakuwa wajinga wa mwisho ktk list ya wajinga na hatustahili kulalamika!!

Ndivyo Tulivyo goes far beyond your perception that I've given up and there is nothing I can do to change the status quo, mindset, habits, etc. etc. I am a firm believer in proving people wrong and so far in my life I've done just that. If I can do it, then you can do it, he can do it, she can do it, they can do it, and most importantly we can and we will do it!
 
Kwa mara ya kwanza,viogozi wa Tz walipoanza kuzomewa na wananchi wpiga kura barabarani.....walianza kujua nini maana ya "NGUVU YA WATU". Kulikuwa na mtindo viogozi walikuwa wanajiaminisha kuwa wananchi..."WATU" ni nguvu uchwara tu!! Sioni namna nyingine ya kuwawajisha viongozi wetu...nje ya "NGUVU YA WATU"...hawa viogozi wanawaona Wataalamu kama uchafu fulani...hawathamini..lolote toka wao..Nafikiri wananchi wakaze uzi..waamke na kufanya kila kinachofaakufanywa..kuwatingish madarakani!!! Hata wakasafishana ..wanachi wakakataa ...hawa viongozi watanyoka... Kama hufuati utaalamu wa watu hsika ufanyweje..zaidi ya kuziomewa?
 
Je Utabiri wa hali ya hewa ulipotamka mwaka 2002 kuwa kutakuwa na uhaba wa mvua, kwa nini Serikali ilipuuzia au ilifanya mambo yanayoonekana kana kwamba walipuuzia ushauri huo?

Wakati tunapata sakata la umeme na Richmond, tulikuwa na njaa na kukimbilia kuomba misaada. Sasa ikiwa Hali ya Hewa waliwasilisha ripoti Serikalini, kwa nini haikufanyiwa kazi?

Wanasema Kinga ni bora kuliko tiba, Mhita alitupa maono ambayo yangetupa kinga na kutuondoa kwenye adha iliyotokea kama tungedamka na kufanya kazi ipaswavyo, kwa nini tunaendelea kukimbilia kutibu na kuweka viraka na si kujijenga na kuweka kinga?

Je ikiwa wataalamu wetu wataendelea kupuuzwa, wakienda Lesotho ni nani wa kulaumiwa?

Je hivi ndivyo serikali yetu ilivyo?

http://www.raiamwema.co.tz/08/03/05/3.php

Wataalamu wenyewe kama ndo akina Chenge,Mnyika, Ndulu na hao waliokuwepo kwenye kamati ya kujadili mambo ya RDL basi lazima niwadharau.Sioni utaalamu wao uko wapi!!
 
How about "mtaalam" huyu according to Michuzi Blog? Ukiweza soma mpaka kwenye comments..

link: http://issamichuzi.blogspot.com/2008/03/mashaka-ni-mfano-wa-kuigwa.html#comments
mashaka ni mfano wa kuigwa
Mashaka akila pozi
Mashaka akihutubia mamilionea kwenye hafla ya Rotary
John Mashaka na milionea Joan CooperHoya Wadau,Nyuzi hiyo hapo nimeipigani kwa udi na uvumbi kuipata. I am proud of this guy. He is a Tanzania na story yake ilitokea kwenye gazeti la Charlotte Observer.
Bwana Michuzi, lazima tuwape watu hongera wanazostahili, hiyo dola 200 niliyolipia kuipata hii story ni kidogo sana kulinganisha na kazi anayoifanya jamaa kwa ajili ya nchi yetu. Hata na wewe siku moja nitakutumia kizawadi kwa maana unaifanyia kazi nzuri sana Tanzania.
Nadhani wengi sasa inabidi watambue mchango wako kwa Nchi yetu. Huyu kijana ni mdogo sana, miaka 30 tu! Huku anawika kwenye ma business week magazine.Kadhalika anafanya kazi Wall-Steet, sehemu hata wazungu wengi wanaiotea ndoto.
Wazungu na vituo vyao vya redio na televisheni wanamhoji kila mara, anapanda sana chati, lakini kikubwa ni moyo na bidii aliyo nao, ni kijana wa ajabu sana. Mimi sijamuona huso kwa uso, lakini namsikia kila mara.

Wabongo tunapanda Chati, vijana wetu wanaamka sana sasa hivi.Mdau Jumanne Kavishe

JOHN MASHAKA, A PEACE- MAKER IN THE MAKING

By our Staff Writers
04 March 2008
The Charlotte Observer

He sat quietly in a business, navy blue suit, amidst prominent, well known corporate heads in the Cozy and exclusive, South Park Manzetti Restaurant Board Room. Until he rose to speak, everyone, all members of the prestigious Rotary Club International, wondered what this quite, humble young man was up to.

As the say goes, that, do not judge a book by its cover, well, he proved those who judged him by his quietness wrong; he had more for his listeners than the expensive suit he wore. His heart spoke louder than his voice

His soft tone did not stay soft for a long time; his eloquence rented the room and pierced through many hearts; John Mashaka, delivered a well thought concise and poignant speech that touched different aspects of human suffering.

"Why must we kill each other? Why must we hate each other? And how for how long are we going to stand while seeing the world burn in ashes? I am not a philosopher or a politician; I am only a concerned private citizen who wants to see the best out of men.

I only want to see human living by each other happiness not by each other's misery. I want to see a world where humans are not being treated as charity cases but as humans" These were Mashaka's concluding sentences.

Not a stranger to the podiums or headlines, John Mashaka, is becoming a household name by his emotional and inspiring speeches across the state.

Joan Cooper, Cooper & Company's, CEO, a well known millionaire, could not help herself, but break in tears to hear Mr. Mashaka narrate his horrific stories of suffering while visiting Tanzania, last August.

He is indeed God sent servant. The world needs more of Mr. Mashaka, I was particularly touched by his humility and love towards humanity, recounted Ms. Cooper.

Wachovia's Investment Banker, Mashaka, balances his busy, fast paced Wall-Street work by donating his time to charitable organizations across the country, and takes three weeks annually without pay, to help people in his native country of Tanzania with his own funds
Mashaka narrated seeing 20 children at Safina-Orphanage in the middle of the slams go without food, and the most touching story was about a two year old boy, suffering from Meningitis at Shirati-Hopsital who could not receive treatment, due to lack of $12

John Mashaka, a native of Tanzania, grabbed headlines in 2005; after he sold his car and returned to his homeland to help his village during famine, with food and clean water. His latest trip to Tanzania was featured in Business Week Magazine's, December edition.

He is currently planning to establish his own foundation that will cater for his village's social needs such as a secondary school, a clinic and a fund to sponsor bright kids into higher learning institutions

A 2004 UNC graduate, Mr. Mashaka is not your typical young man; he is a man with a mission, he is well respected, and stands tall in his peer group, and could not have come at a perfect time, when the world need millions of generous and passionate people like him
 
Wataalamu wenyewe kama ndo akina Chenge,Mnyika, Ndulu na hao waliokuwepo kwenye kamati ya kujadili mambo ya RDL basi lazima niwadharau.Sioni utaalamu wao uko wapi!!

Nyangumi,

Nafahamu fika una hasira na Serikali, lakini wataalamu tunaoongelea ni wale wa hali ya hewa ambao mwaka 2002 walitoa tahadhari kwa Serikali kuhusu ukame uliokuwa unakuja kwa miaka 3-4 ya mbeleni.

Mimi nimeleta hoja si kuwazungumzia kina Chenge, Mwanyika au Ndulu, bali ni wale wataalamu wanaofanya kazi zao na kupuuzwa na kama si kupuuzwa basi viongozi wetu ni wazembe.

Kumbuka sakata la mvua si kuwa lilisababisha uhaba wa umeme pekee, hata chakula kilikuwa shida na kama nakumbuka vizuri kuna watu walikufa njaa!

Swali ni kwa nini Serikali yetu si pro-active? why are they so passive on issues that matter? May be I should ask why is CCM so passive on issues that matters but extremly pro-active on issues that do not matter?
 
Back
Top Bottom