Wataalamu,toeni ushauri kuhusu ujenzi wa nyumba ya ghorofa kwa unafuu

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,959
20,528
Napenda wataalamu watupe ushauri ili kuondoa woga wa watu kuhusu ujenzi wa nyumba ya ghorofa

Moja,gharama kubwa ziko hatua gani,mahitaji muhimu ni nini,na kuna vibali aina gani vinatakiwa,

Na mambo mengine pia,hasa kadirio la chini la gharama
 
Wala usipotezi muda, wewe mtafute Magufuli tu, yeye ndio anajua siri za ujenzi wa maghorofa maana ghorofa la hostel lenye floor nne tena pana sana huku likiwa full Furniture pale UDSM aliweza kulijenga kwa milioni 500 tu. Hii haijawi kutokea popote duniani, maana kwa hiyo bei hata Furniture tu za ndani ya lile ghorofa haiwezi kutosha.
 
Akaongee na TBA watampunguzia kama walivyompunguzia ngosha
 
Gharama hutegemea jinsi kiwanja chako kilivyo.. tambarare au bonde na milima....

Otherwise nondo ni zile zile...kokoto nyeusi ni ile ile....

Cement ni ile ile ...sema hula mifuko mingi zaidi kwenye jamvi na slub

Changamoto ya slub ni gharama ya mbao au marine boards (sijui ndivyo zinavyoitwa)

Na costi ya finishing ni ile ile haijawahi kumuacha mtu salama..... (of course itaongezeka ...)

Vibali vinatakiwa kutoka manispaa na stika toka bodi (sijui ndio wanajiita bodi wenyewe...hakikisha unapata stika /bango zao jamaa wasumbufu wakiona slub tu wanaanza kuzengea zengea...ukikaa vibaya
stop.order inakuhusu)

Anyway mie sio mtaalam...ni kidampa tu nabeba tofali na zege nimekupa uzoefu kutokana na ninavyoona site kwa mabosi
...

Sent from my..... using JamiiForums mobile app
 
Gharama ya kujipanga ni kwenye jamvi (slab) kwa sababu vifaa vingi vya ujenzi huhitajika ambavyo ni saruji, nondo, mbao, mirunda, mchanga, kokoto, maji, misumari, binding wire, conduits za umeme na maji zitahitajika kuwekwa kabla ya kumwaga zege na hela ufundi kwa kila shughuli niliyotaja i.e seremala, kufunga hizo nondo n.k. kwa hiyo inahitaji kujipanga...

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Suala kubwa hapa dont procure services from contractors. Tafuta fundi mzuri msimamie nae kila stegi. Kila kitu ununue mwenyewe.

Ukijiloga ukawema contractor bei itakuja mara 20 zaidi
 
Ili kuokoa muda na kujihakikishia ubora unaweza kununua zege ambayo imeshachanganywa toka kiwandani (ready made concrete )

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Ili kuokoa muda na kujihakikishia ubora unaweza kununua zege ambayo imeshachanganywa toka kiwandani (ready made concrete )

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Mkuu hii inapatikana wapi kwa Dar, na je una idea yoyote kuhusu bei.
 
Tafuta architect akuchoree kulingana na mahitaji yako,tafuta engineer mzuri akufanyie structural design,QS akufanyie estimates ya gharama na akupe schedule ya material(itakusaidia kufanya manunuzi,hakikisha unapata vibali vyote muhimu kutoka mamlaka husika kuepuka usumbufu,ukianza ujenzi tafuta mafundi wazoefu na make sure unafanya follow up ya uhakika.A good design and proper supervision will help you to reduce cost somehow.
 
nondo 300
cement 300
mchanga rol 5
matofal 10000 tofar 1 1000
misumal ya 40000 sh
mafund +wasaidiz mil 10
kokoto mil 3

hata mil 100 haiishi

utan tu jaman ila gharama haiwez kua kubwa sana
 
Back
Top Bottom