mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 535
- 1,746
Kama kuna kipindi ambacho wataalamu wa ulozi , magwiji wa ushirikina na uchawi na waganga wote wa kienyeji toka kigoma, ufipa, sumbawanga, rukwa na tanga wangejizolea umaarufu na kupiga pesa za maana ni wakati huu wa covid 19
Lakini cha kushangaza tangu covid itie timu wajuba wote wa ulozi wametokomea pasikojulikana na Yale mabango yao ya kutibu magonjwa yote sugu hayaonekani.
Hadi wale wa zile meseji za "mjukuu wangu majaliwa utajiri niliokupa naona umekupa kiburi nlikuomba unipe kilo moja ya nyama Tu, ila Kwa jeuri Leo umeniletea ng'ombe wazima 9 na ndama wawili" na wao hawatumi meseji.
Sasa sijui wamekwama wapi wajuba wetu hawa katika kada ya ulozi.