Wataalamu kutoka Sumbawanga, Rukwa na Ufipa wameishia wapi?

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
535
1,746
Kama kuna kipindi ambacho wataalamu wa ulozi , magwiji wa ushirikina na uchawi na waganga wote wa kienyeji toka kigoma, ufipa, sumbawanga, rukwa na tanga wangejizolea umaarufu na kupiga pesa za maana ni wakati huu wa covid 19

Lakini cha kushangaza tangu covid itie timu wajuba wote wa ulozi wametokomea pasikojulikana na Yale mabango yao ya kutibu magonjwa yote sugu hayaonekani.

Hadi wale wa zile meseji za "mjukuu wangu majaliwa utajiri niliokupa naona umekupa kiburi nlikuomba unipe kilo moja ya nyama Tu, ila Kwa jeuri Leo umeniletea ng'ombe wazima 9 na ndama wawili" na wao hawatumi meseji.

Sasa sijui wamekwama wapi wajuba wetu hawa katika kada ya ulozi.
 
Wamehamishia matangazo yao kule instagram. Huko wana sema wanatoa Kisomo na Dua kwa matatizo sugu.

Sasa sina hakika na uhusiano na dini.wote dini moja
 
Wapo kama kawaida, unataka wafanye nini? Tangu lini Serikali ikakubali wazi wazi mambo ya uganga wa jadi? Waulizeni jamaa zenu mnaowapa kipaumbele kuwa wamefikia wapi huko maabara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna kipindi ambacho wataalamu wa ulozi , magwiji wa ushirikina na uchawi na waganga wote wa kienyeji toka kigoma, ufipa, sumbawanga, rukwa na tanga wangejizolea umaarufu na kupiga pesa za maana ni wakati huu wa covid 19

Lakini cha kushangaza tangu covid itie timu wajuba wote wa ulozi wametokomea pasikojulikana na Yale mabango yao ya kutibu magonjwa yote sugu hayaonekani.

Hadi wale wa zile meseji za "mjukuu wangu majaliwa utajiri niliokupa naona umekupa kiburi nlikuomba unipe kilo moja ya nyama Tu, ila Kwa jeuri Leo umeniletea ng'ombe wazima 9 na ndama wawili" na wao hawatumi meseji.

Sasa sijui wamekwama wapi wajuba wetu hawa katika kada ya ulozi.
Wanaokoa maisha yao dhidi ya corona.
 
Uchawi hauvuki bahari kitu kimetoa ma mbele huko,wenyewe wanabakia kuwabaini wezi wa kuku.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom