Wataalamu Hawa Wachunguzwe! Je, Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!"

"Carbon dioxide produced during smelting of Copper Concentrate can result into acid rain, which is harmful to plants".

Naunga mkono hoja. Hao walioandika mambo haya watafutwe wafunguliwe kesi ya kuhujumu uchumi.

Lakini kama watu wamehongwa kuruhusu wizi wa mahela yote hayo, basi kuna watu wana hela sana jamani. Au huwa wanahongwa bila kujua thamani ya kile wanachoruhusu, hivyo kushindwa kukadiria kiasi cha mlungula wanachostahili? Maanake unaweza kukuta Waziri aliahidiwa ufadhili wa kumsomesha bintiye ughaibuni, akadondoka signature. Nina mashaka makubwa na uwezo wa watendaji wetu. Pia elimu yetu.
Nyerere alipata kusema ''mzungu anakupa kipande cha chupa na wewe unampa almasi kisha unakimbia kama zuzu''...pili, wabongo wengu humuamini mtu anayezungumza kiingereza.
 
Mkuu hazina ya madini tuliyonayo thamani yake ni zaidi ya dola milioni 300, pia tukiwanayo hiyo hata DRC na majirani wengine wataleta michanga yao kwetu.
Paskali umeandika hoja kali za kinabii, hii nchi ina kakikundi ka wapotoshaji, ni very smart na ni wasomi wazuri sana. Wanapopewa kazi wao ni kujihalalishia upigaji tu.
Kiukweli wewe Mkuu Wakudadavua, uko vizuri sana, na amini usiamini, mimi ninakukubali sana tuu, tatizo lako ni moja tuu na ni dogo sana!, nikikuambia kisababishi cha madudu yote haya kiko mtaa wa Lumumba, utanibishia na tutatofautiana kabisa!.

Naomba nikukumbushe hoja hizi?,
Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision ...
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye ...
Umechoshwa na Ujinga, Umasikini, Maradhi, Rushwa na Ufisadi?!, 25 ...
Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya ...


unakumbuka nilisema nini kuhusu Tanzania sio masikini, kuna mtu ni responsible kwa umasikini wetu huu ila tuu mnajitia upofu, hamtaki kukubali!.
Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari na tumeamua ...

Kiukweli Magufuli ameletwa na Mungu ili kulikomboa hili taifa japo...

Paskali.
 
"Carbon dioxide produced during smelting of Copper Concentrate can result into acid rain, which is harmful to plants".

Naunga mkono hoja. Hao walioandika mambo haya watafutwe wafunguliwe kesi ya kuhujumu uchumi.

Lakini kama watu wamehongwa kuruhusu wizi wa mahela yote hayo, basi kuna watu wana hela sana jamani. Au huwa wanahongwa bila kujua thamani ya kile wanachoruhusu, hivyo kushindwa kukadiria kiasi cha mlungula wanachostahili? Maanake unaweza kukuta Waziri aliahidiwa ufadhili wa kumsomesha bintiye ughaibuni, akadondoka signature. Nina mashaka makubwa na uwezo wa watendaji wetu. Pia elimu yetu.
Mkuu Zungu Pule, karibu mitaa ya Masaki, Osterbay, Mbezi Beach na Mbweni, utembelee ma apartments ya waserekali hawa, ndipo utaelewa!.

Hujabahatikaga kuona makontena ya vitabu vikigawiwa majimbo yote ya ule mkoa fulani kule Kanda ya Ziwa?, kwa taarifa vitabu hivyo huletwa na marafiki zake walioko Canada!, tunachoonyeshwa ni makontena tuu ya vitabu, ila yale makontena ya ma vogue na ma escallades, hatuonyeshwi, bali tunapishana nato tuu mabarabani, sisi tukiwa kwenye bajaj na boda boda, huku wake zao, watoto wao na vimada wao, wakiyaburuza mitaani!.

Tanzania ni zaidi hii uijuayo!.

Paskali
 
Mkuu Zungu Pule, karibu mitaa ya Masaki, Osterbay, Mbezi Beach na Mbweni, utembelee ma apartments ya waserekali hawa, ndipo utaelewa!.

Hujabahatikaga kuona makontena ya vitabu vikigawiwa majimbo yote ya ule mkoa fulani kule Kanda ya Ziwa?, kwa taarifa vitabu hivyo huletwa na marafiki zake walioko Canada!, tunachoonyeshwa ni makontena tuu ya vitabu, ila yale makontena ya ma vogue na ma escallades, hatuonyeshwi, bali tunapishana nato tuu mabarabani, sisi tukiwa kwenye bajaj na boda boda, huku wake zao, watoto wao na vimada wao, wakiyaburuza mitaani!.

Tanzania ni zaidi hii uijuayo!.

Paskali
Nakukubali Paskali,
Kwani waasisi na wapaliliaji wizi huu si ndio 'huteua' nani awe rais?
 
Kutoka ndani ya Roho yangu kwa dhati kabisa

Ningelikuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Pascal Mayalla angekuwa mmoja wa washauri wangu wandani kwa masuala mbalimbali.

Somebody who dares to talk with vision, focua and accuracy.
 
What if kama hawa waliotoa report leo 24/05/2017 nao walihongwa na waliowatuma ili kujustify jambo fulani wanalolitaka, then wakawaambia waseme tunaweza kujenga kinyume na wale wa mwanzo.
 
Wanabodi,
Hii ndio Ripoti ya kitaalamu iliyotoa go ahead mchanga wa dhahabu uendelee kusafirishwa nje kwa hoja kuwa Tanzania hatuwezi!. Kwa vile hii ni ripoti ya kitaalamu, na mimi sio mtaalamu, naomba kuwauliza wenye mwanga na mambo haya, Jee kunauwezekano wataalamu wetu hawa walihongwa na makampuni ya madini ili kutoa ripoti hii, hivyo wachunguzwe na ikukutikana ni kweli, sheria ichukue mkondo wake?. Kwa Ripoti hii kuwa Tanzania Hutuwezi kujenga smelter ya mchanga wa makanikani ya dhahabu, Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!".

Ripoti yenyewe ni hii kwa hisani ya Mkuu Chige.

Mkuu Chige, thanks kwa Ripoti hii.

Natoa wito kwa Wataalam waliyo tayarisha, Ripoti hii, watafutwe, wachunguzwe, watakuwa walihongwa na makampuni ya madini, ili watoe Ripoti kuonyesha Tanzania hatuwezi, hivyo washitakiwe, hawa ndio waliosababisha Tanzania tuendelee kuibiwa dhahabu yetu kwa kudanganywa kuwa ni mchanga!.

Japo mimi sio mtaalamu wa madini, lakini ni Mtanzania wa kawaida kabisa ninaejua kusoma na kuandika tuu, kwa kuisoma ripoti tuu Ripoti hii, utaona wazi wazi kabisa, wataalamu hawa walihongwa, wakatafuna fedha za umma kufanya ziara za China na Japan kisha kutujia na ripoti hii ambayo ni wizi mtupu!.

Hao makampuni ya madini kwa vyovyote vile watakuwa waliwahonga wataalamu hawa kutoa ripoti hii, ili waendelee kuiba dhahabu yetu kwa kutudanganya ni mchanga!, hivyo sasa Magufuli, leta ule mtambo mdogo, tuuchenjue wenyewe huu mchanga wote ulikamatwa, kisha kiasi cha dhahabu kitakacho patikana, kitazidishwa mara idadi ya makontena yote ya mchanga, waliowahi kusafirisha nje!, tangu waanze kuchimba, kisha watulipe kila senti ya dhahabu waliotuibia, wezi wakubwa hawa!.
Observation yangu.
1.Conclusion yao imesema hivi "The study concludes that it is currently not feasible for a Copper Concentrate smelter to be constructed in the country to smelt and refine Copper Concentrate produced by BGM and BZGM. However, investors are encouraged to explore more on possibilities of discovering copper deposits which will warrant for installation of a Copper Concentrate smelter in the Country."
Hii ndio iliyohalalisha huu wizi!.

2. Kwenye ripoti yao wameonyesha wametembelea China na Japani zenye smelter kubwa zinazohitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka ambazo zinagharimu dola USD 500 million hadi USD 800 millioni ili tushindwe, kwa sababu hatuna mchanga mwingi kihivyo, na pesa hiyo ni pesa ndefu ili tuu wezi hawa waendelee kutuibia, ila ukweli ni kuwa kuna smelter ndogo za hadi ya tani 30 tuu kama ile ya Stillwater Mining ya nchini Marekani inayogharimu dola milioni 300 tuu!. Kwanini hawakwenda huko?!.

3. Ripoti hiyo imeonyesha taarifa ya kupika kuonyesha mchanga huo una kiwango kidogo cha cha shaba na dhahabu kiduchu tuu ili tusijue tunaibiwa!, kwa kuonyesha copper (average assay 15%), gold(average assay 0.02%) and silver (average assay 0.02%), copper being in higher concentration than the rest, hence the product named Copper Concentrate hivyo kuonyesha hakuna faida yoyote ya maana, wakati ripoti za kijilojia zinaonyesha viwango tofauti vya shaba, dhahabu,na fedha ndio kiduchu, lakini kuna madini mengine mengi ambayo yana thamani, lakini hayatajwi!. Hivyo kiukweli hapa tunaibiwa!.
  • The Bulyanhulu Gold Mine located in Kahama District has a copper deposit with high gold values averaging 0.0015% gold, 0.52% copper and 0.00114% silver. It has a mineable resource of 13.64 million tonnes. It commenced production in 2001 with an average annual production of Copper Concentrate of 50,000 tonnes (source: Opportunities for Mineral Resource Development, 2005).

  • The Buzwagi Gold Mine located in Kahama District has a copper deposit with high gold values averaging at 2.10 grams per tonne, 0.14% copper and 0.00115% silver. It has a mineable resource of 41 million tonnes. It commenced production in 2009 with an average annual production of Copper Concentrate of 10,000 tonnes.
4. Mwisho ripoti hiyo ikatoa vitisho kibao kuhusu athari za kimazingira ili kutukatisha kabisa tamaa tusithubutu hata kujaribu, kwa kuorodhesha haya masumu kibao, tukijaribu tuu, tutaua watu wetu..
  • Depending on the composition of the Copper Concentrate, a number of heavy metals such as copper, mercury, cadmium, nickel, cobalt, zinc and so forth may be concentrated through processing and be deposited to the environment. These metals may enter into the human blood system by inhalation or by being ingested from heavy metal contaminated species (animals, fish, plants, etc).

    Heavy metal toxicity can result in damaged or reduced mental and central nervous function, lower energy levels, and damage to blood composition, lungs, kidneys, liver, and other vital organs. Long-term exposure may result in slowly progressing physical, muscular, and neurological degenerative processes that mimic Alzheimer's disease, Parkinson's disease, muscular dystrophy, and multiple sclerosis.

  • Crystalline silica, when inhaled can cause silicosis of the lung both to humans and animals;

  • Carbon dioxide produced during smelting of Copper Concentrate can result into acid rain, which is harmful to plants;

  • Chemicals/reagents used in smelting process can be harmful to humans especially to staff exposed to them.

  • Waste products from Copper Concentrate may amount to billions of tonnes. The tailings from the concentrating operation and the slag from the smelting operation do pose a potential health hazard and may require huge expenses to protect and manage the affected areas.
Swali ni jee kwani huko wanakosafisha, wanafanya nini kukabiliana na athari hizi?, na sisi tukianzisha si tutakabiliana nazo?. Au hii migodi iliyopo inatoa sumu hizo hizo, kwani wanafanyaje?, hilo smelter tukalijenge kule kwenye visiwa visivyo na watu, au maporini kabisa!.

Haiwezekani watu wahangaike hivyo kusafirisha makontena milioni toka Tanzania hadi Japan for nothing kama tunavyoelezwa na ripoti hii!, msikute rais wetu hili alioteshwa na Mungu mwenyewe, na kama issue ni Tanzania hatuna umeme wa kutosha, tnaweza kukubaliana kila siku umeme nchi nchi nzima ni hadi saa 6 usiku, hadi 12:00 asubuhi, isipokuwa taasisi muhimu, kisha umeme wote wa gridi uende kwenye smelter just 6 hours daily.

Mnaonaje wajameni hawa wataalamu wachunguzwe, au wenye utaalam, tusaidieni hii kitu iko sawa?!. Na hata kama hawa wataalamu walihongwa, hadi mimi tuu ni layman kabisa, nimewashutukia, how about wabunge wetu?, vipi kama yetu ya Bunge ya Nishati na Madini?, vipi watendaji wetu wa Wizara ya Nishati na Madini, kweli hili hawajaliona?. Haya hao wote ni watu wa mshahara tuachane nao, waachwe wajipigie tuu mishahara yao, jee vipi kuhusu wateule wa rais?, waziri, naibu waziri na katibu mkuu?. Waziri si ni profesa wa geolojia, nae kadanganywa kama mtoto mdogo na kakubali?. Siku ukweli ukibainika kuwa tunapigwa, atasubiri kutumbuliwa, au ni bora awatumbue wahuni hawa kabla, vingenevyo watamponza, atatumbuliwa yeye!.

Kama iko sawa jee rais wetu ataimeza amri yake na huo mchanga utachunguzwa tuu kisha kuendelea kusafirishwa?!.

Paskali
Update 1.
Kumejitokeza Mtaalam mwenye insight kuhusu mambo haya na amejitokeza hapa
Kwenye Sakata la Mchanga wa Dhahabu - NAFAHAMU Ukweli wa ndani
Mayalla, ripoti hii na uzi huu ulinipita. Nani aliyetoa ripoti hii? yaani waliokuwa kwenye timu hiyo ni akina nani? Nin hamu sana ya kuchangia hapo kwenye vitisho maana naona walitumia taaluma yangu kuwatisha wasiojua.
 
Nyerere alipata kusema ''mzungu anakupa kipande cha chupa na wewe unampa almasi kisha unakimbia kama zuzu''...pili, wabongo wengu humuamini mtu anayezungumza kiingereza.
Ujinga wa watanzania walio wengi ni kumuamini mtu anayeongea kiingereza vizuri kuliko mtu mwenye akili. Kujua lugha fulani kwa ufasaha na kuwa akili na uwezo wa kufikiri ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Yaani hapa sijui tukusaidieje? Maana watanzania tumeisha amua, na dunia ituelewe hivyo. Hatutaki kuibiwa tena. Katafute kilinge kingine cha kupora. Hivi Kenya hawana madini kweli? Au nao walikuwa wanachimba ya nchi za nje wakati yakwao wanayaacha kama US afanyavyo kwenye nishati ya mafuta!
What if kama hawa waliotoa report leo 24/05/2017 nao walihongwa na waliowatuma ili kujustify jambo fulani wanalolitaka, then wakawaambia waseme tunaweza kujenga kinyume na wale wa mwanzo.
 
....
....Upinzani walipiga sana kelele kuhusu mikataba ya uchimbaji wa madini kuwekwa Hadharani...Leo tusingefika huko...Muda ni fedha
Mkuu tatizo la udanganyifu kwenye mchanga wa dhahabu sio la mkataba, kimsingi ni watanzania wabinafsi wala rushwa.
 
Baba wataifa alisema tusichimbe rasilimali zetu yaani madini kama hatujawa tayari. Baada ya mzee wetu kuondoka sasa walafi wanakomba hata mchanga wenye rasilimali mbali mbali. Raisi watumbue wote toka enzi ya mzee kipara maana katuingiza mkenge kwenye mikataba feki. Pia wachunguzwe wenye migodi waliokuwa na wanao hamisha mabox ya dhahabu toka migodini kwenda nje ya nchi direct. Box moja huwa na dhahabu na trip moja inaweza kuwa na box 30 au zaidi. Ichunguzwe kwa mwezi huhamisha kiasi gani, kwa mwaka na kwa miaka yote waliyotuibia Botswana ni 50/50 serikali na muwekezaji kwa nini sisi ni 96/4. Ulaji umezidi mikataba ichunguzwe hatua stahiki zichukuliwe imetosha tulivyoibiwa.
 
Kinachoumiza zaidi hii Nchi wasomi sana ndio wanaoongoza kuliingizia taifa hasara
 
Nyerere alipata kusema ''mzungu anakupa kipande cha chupa na wewe unampa almasi kisha unakimbia kama zuzu''...pili, wabongo wengu humuamini mtu anayezungumza kiingereza.
Ripoti ya kupika ...
Kinachoumiza zaidi hii Nchi wasomi sana ndio wanaoongoza kuliingizia taifa hasara
Mkuu tatizo la udanganyifu kwenye mchanga wa dhahabu sio la mkataba, kimsingi ni watanzania wabinafsi wala rushwa.
Mkuu Zungu Pule, karibu mitaa ya Masaki, Osterbay, Mbezi Beach na Mbweni, utembelee ma apartments ya waserekali hawa, ndipo utaelewa!. tunachoonyeshwa ni makontena tuu ya vitabu, ila yale makontena ya ma vogue na ma escallades, hatuonyeshwi, bali tunapishana nato tuu mabarabani, sisi tukiwa kwenye bajaj na boda boda, huku wake zao, watoto wao na vimada wao, wakiyaburuza mitaani!. Tanzania ni zaidi hii uijuayo!. Paskali
Nakubaliana karibu na wote, na nakumbuka msemo wapoti toka Bariadi akijigamba kabisa kwamba yeye ni "..nyoka mwenye makengenza" na alijibu kwa jeuri kabisa bila kujali na kwa kiburi alipoulizwa kuhusu £500K zilizopo Isle of Jersey kuwa ni "...vijisenti tu"!. Huyu hasa wakati wa mchonga sijuwi angeishia wapi, cha kushangaza hakupata adhabu iliyostahili wala nini, kwanza ndiyo anapeta bungeni kama sio kuliendesha sometimes! Kweli hii ndiyo TZ yetu, twashangaa nini?!
Pia sishangai mtoto wa shule ya msingi akiwaza mambo ya magari na majumba, au wazee wetu kuwakashifu watoto wao kwa kutokuwa mafisadi kisa eti wanafanya kazi sehemu nyeti serikalini...
Tulishapoteza mwelekeo siku nyingi, yale ya Mwalimu kusomesha watoto wake kwenye shule zetu za mitaani zilishapita, ni wao dhidi yetu, labda tukubali twaishi kibepari, ila basi hela za umma zisichotwe na viongozi kuishi kibepari, wajuwe wao ni watumishi wa umma...
Ebu tumsaidie MAGUFULI JEMBE, asafishe kabisa huu uchafu kule, yatosha...
 
Back
Top Bottom