Wataalam wa moyo wa Kikwete sasa waanza kuvuka anga la Tanzania

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,403
Wataalamu wa moyo wa taasisi ya Jakaya Kikwete wako Kigali kufanya upasuaji wa moyo, hongera JK kwa hili hapa uliona mbali sana. JPM hebu waandalie ka hafla kafupi Ikulu kuwapongeza.
7f5c4fe3-1068-474c-b470-c1744dc66f90.jpg
 
Kusema ule ukweli kama jk asingekua mpole na kuwaamini sana wasaidizi wake ambao baadhi walifanya ndivyo sivyo, nchi hii ingefika mbali! Alijitahidi kiasi chake na maadam tulihitaji aina ya watu kama jpm baada ya utawala wa jk, basi huenda tukafanikiwa kufika pale tunapo pataka. Ni mtazamo tu.
 
Ni kasumba ya binadamu baya moja analowezakulifanya binadamu hufuta mema laki moja aliyofanya. Kikwete anamema yake ni Kweli lakini kushindwa kuthibiti uhujumu uchumi, uzembe KAZINI NA uswahiba na kazi ndiyo yanaweza kumfanya afutiwe mema Yote aliyofanya utawala wake wote. Japo kila binadamu anamapungufu yake pia.
 
Ni kasumba ya binadamu baya moja analowezakulifanya binadamu hufuta mema laki moja aliyofanya. Kikwete anamema yake ni Kweli lakini kushindwa kuthibiti uhujumu uchumi, uzembe KAZINI NA uswahiba na kazi ndiyo yanaweza kumfanya afutiwe mema Yote aliyofanya utawala wake wote. Japo kila binadamu anamapungufu yake pia.[/QUOTEAc

Acheni uongo mpango wa taasisi ya moyo ulianza kipindi cha mkapa.wakati huo CEO WA Muhimbili alikuwa Dr. Tregon mwingereza ndiye alifanya ukaeabati WA hospital na kubadilisha mishahara ya wafanyakazi.strategic plan ilikuwa kujenga, maabara kubwa ambayo ilijengwa na theatre kubwa pamoja na hospital ya moyo.semeni ni serikali.Makosa yanayofanyika ni kuyapa majina
 
Kusema ule ukweli kama jk asingekua mpole na kuwaamini sana wasaidizi wake ambao baadhi walifanya ndivyo sivyo, nchi hii ingefika mbali! Alijitahidi kiasi chake na maadam tulihitaji aina ya watu kama jpm baada ya utawala wa jk, basi huenda tukafanikiwa kufika pale tunapo pataka. Ni mtazamo tu.
UMEONGEA UKWELI, Kiukweli Kikwete amefanya Mengi tu mazuri, na kama binadamu kulikuwa na kasoro zake ambazo hata kwa Magufuli au yoyote zinaweza kutokea, Watendaji aliowaamini ndio waliomuangusha, ila angeweza kutuvusha kama angekuwa mkali kama Magufuli, kila mtu na roho yake, JK alikuwa na kamoyo kaimani flani ambacho kilizidi kumponza Zaidi, Binafsi namkubali sana tu na Mungu amemleta Magufuli nae pia tumemkubali tutafika tu, hofu yangu akimaliza Magufuli siioni wakushika kijiti.
 
Naombeni majina yao hao Madr. na mikoa waliotoka naona kama wote wamefanana kama Ndugu, ila hao wakaka wanasura tamu kweli. WAMEOA TAYARI??;);););););)
 
Wataalamu wa moyo wa taasisi ya Jakaya Kikwete wako Kigali kufanya upasuaji wa moyo, hongera JK kwa hili hapa uliona mbali sana. JPM hebu waandalie ka hafla kafupi Ikulu kuwapongeza.
7f5c4fe3-1068-474c-b470-c1744dc66f90.jpg
halafu ni vijana watupu hadi raha, hadi wafikishe miaka sitini watakuwa wamekula bata sana.
 
Naombeni majina yao hao Madr. na mikoa waliotoka naona kama wote wamefanana kama Ndugu, ila hao wakaka wanasura tamu kweli. WAMEOA TAYARI??;);););););)
Dr.Godwin Godfrey, Dr.Naiz Majani na Dr. Onesmo Mhewa. Haya ndio majembe ya kazi.
 
Mazuri ya Kikwete
Miundombinu : Mabarabara nchi nzima, Madaraja makubwa kwa madogo mfano, Kigamboni, Malagarasi, Mradi wa mabasi yaendayo kasi.

Mawasiliano: Mkongo wa Taifa, Mitandao lukuki ya simu hadi vijijini.

Elimu: Shule za Kata, vyuo vikuu mfano UDOM, Nelson Mandela, na kuongezeka kwa udahili

Nishati: Umeme hadi vijijini kupitia mpango wa Rea

Demokrasia: vyama vya siasa na wananchi walikuwa huru sana kushiriki katika mchakato wa kisiasa nchini, pia uhuru mkubwa wa habari.

Uchumi: Uliendelea kukua kati ya asilimia 6 mpaka 7, yakiambatana na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kutoka bilioni 177 mwaka 2005 hadi bilioni 900 mwaka 2015

Uboreshaji wa Jeshi: Jeshi liliboreshwa kw zana za kisasa za kijeshi na katika medani

Diplomasia ya hali ya juu: kuanzia kule Comoro, Madagadcar, mgogoro wa uchaguzi kenya, M23, Burundi kote Tanzania ilichukua uongozi.

Kijamii: Kuwawezesha akina mama kisiasa na kiuchumi

Utafiti: kuanzisha mfuko wa Utafiti unaosaidia tafiti mbalimbali nchini na kuendesha incubator programmes.

Uchumi wa Gesi: Mradi wa gesi utaipropel Tanzania kuingia katika uchumi wa kati

Sanaa na michezo: Kuwaundia wasanii sheria ya hati miliki, kuleta na kuwalipa makocha wa kigeni kwa michezo mbalimbali, kukarabati uwanja wetu wa Uhuru ( Shamba la bibi) sasa hivi unakaribia kuisha, Kuanzishwa kwa Kikwete Academy kwa ajili ya kukuza vipaji vya michezo mbalimbali.

Afya: Kujenga kituo cha Moyo cha Kisasa, Kupambana na Malaria, Upatikanaji wa ARV kwa waathirika bure, kupungua kwa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Maji: Mradi wa maji kutoka Ruvu Chini unakaribia kukamilika, muda si mrefu utakamilika.

Ajira ndogondogo: Mpesa, Tigopesa, vijana wa bodaboda, bajaji n.k

Acheni Masikhara, JK amefanya mambo mengi sana ya msingi!
 
Wataalamu wa moyo wa taasisi ya Jakaya Kikwete wako Kigali kufanya upasuaji wa moyo, hongera JK kwa hili hapa uliona mbali sana. JPM hebu waandalie ka hafla kafupi Ikulu kuwapongeza.
7f5c4fe3-1068-474c-b470-c1744dc66f90.jpg
Huyu kazi ni kufukuza. Watumishi walioko mashuleni wanaitwa wafanyakazi hewa.
 
Back
Top Bottom