Wataalam wa MAONO: Hali ya Mtanzania itakuwaje siku watuhumiwa wa ufisadi wakibalance CCM na CHADEMA?

Tunataka kujenga vyama viwili vyenye nguvu acha wabaki huko ili tutakapo wamaliza mafisadi tubaki na watu wenye akili timamu kwenye vyama vyetu viwili kujenga nchi aliyotuwekea misingi baba wa taifa letu. Tutakuwa tunashindana kwa nguvu ya hoja na si kwa nguvu ya matumbo na ukubwa wa vitambi.

Duuh...na sehemu tulisema giza likitanda nguvu ya neno hili litawavuta wote wenye nia moja sehemu moja na wale wengine watabaki wasiamini kinachotokea...Tumefanya tumemaliza kazi kwenu sasa kuendeleza vyama vyenu...

I rest my case!

Mwana wa Adam aenda zake kujipumzikia ale pension yake na baadaye uzima wa milele...For those expecting un expected too little too late to catch the train...Mchezo umekwishney bado manifestation tu!
 
Nawaza, najaribu kuwaza huku nikijitenga kabisa na ufisadi ktk level za kitaifa maana nimeamua kudeal na ule wa ngazi ya familia na mtaa maana unanigusa haraka na madhara yake ni haraka zaidi.

najaribu kufuatilia huu mtanange wa wanaosadikiwa kuwa watuhumiwa wa Ufisadi wa kitaifa wakibadilishana jezi huku mashabiki wakibadili aina za santuri katika kusifu na kuabudu v/s kuponda na kutuhumiana.
Najiuliza wataalamu wa kuona mambo ya kisiasa kwa kina, Hali ya mtanzania itakuwaje siku kukiwa na 50/50 ya watuhumiwa wa ufisadi katika vyama hivi viwili?

Mimi kama mwananchi mtaani ambae nimeamua kukubwisha siasa za nyumba kumikumi na siasa za familia na kudogosha siasa za Kibunge na kitaifa hali yangu itakuwaje katika njia panda hiyo?

Rafiki unadhani unaweza kuwagusa hao?Unaweza kuwagusa kama ukiamua sheria ifuate mkondo wake.Na moja ni kuondoa kitu hii inayoitwa KINGA.

Kinga ndiyo imetuharibu.Wanaotuibia ni hao tuliowapa Madaraka na bado kodi zetu zinaendelea kuwahudumia.Inawezekana ukiamua kumshtaki LN unaweza ukapata aibu kwanini white house =Satan house aka black house
 
Kiukweli watanzania tutakuwa na wakati mgumu sana.....Mfano mdogo tu leo Msigwa na Nyalandu wako timu moja.... baada ya kununuana kwenye utawala wa Kikwete.

Tuombe Mungu kizaliwe chama kingine cha upinzani mbadala wa Chadema....iliyoacha kukemea ufisadi hadi kutetea ufisadi na mafisadi.
Hivi vyama vimegeuzwa recycle bins,hatuna uhakika na ujio chama chenye maadili ya utu.
Maoni ya watu wengi kwa sasa hawasikitishwi na ufisadi uliokubuu tena,wanaona ni sawa imeishakuwa mazoea.Kuna wakati wengine wanadai ufisadi sio kosa ni mfumo.
 
Tunaona sawa sababu ccm na Chadema tuhuma zao zinafanana...kilichobaki ni kupima nani mwenye Tuhuma zaidi
 
Kati yao hao ninani aliye wahi kuludisha kadi ya ccm hayo ni matamko tu mdomoni kutuaminisha kuwa wamehama lengo lao kuudhoofisha upinzani waambieni waludishe kadi za ccm kwanza
 
Nawaza, najaribu kuwaza huku nikijitenga kabisa na ufisadi ktk level za kitaifa maana nimeamua kudeal na ule wa ngazi ya familia na mtaa maana unanigusa haraka na madhara yake ni haraka zaidi.

najaribu kufuatilia huu mtanange wa wanaosadikiwa kuwa watuhumiwa wa Ufisadi wa kitaifa wakibadilishana jezi huku mashabiki wakibadili aina za santuri katika kusifu na kuabudu v/s kuponda na kutuhumiana.
Najiuliza wataalamu wa kuona mambo ya kisiasa kwa kina, Hali ya mtanzania itakuwaje siku kukiwa na 50/50 ya watuhumiwa wa ufisadi katika vyama hivi viwili?

Mimi kama mwananchi mtaani ambae nimeamua kukubwisha siasa za nyumba kumikumi na siasa za familia na kudogosha siasa za Kibunge na kitaifa hali yangu itakuwaje katika njia panda hiyo?

Hii nadharia yako haiko sawa. Labda niongeze kuwa hauko honest hapa. Naamini unavyoona ni kuwa mafisadi walioko CCM wanatimkia CHADEMA. Sasa hiyo 50/50 inatoka wapi? Umeshaanza kuwa na mashaka kwamba CCM hata enzi hii nayo bado inalea mafisadi?
 
Back
Top Bottom