Waliopo Kilimanjaro, moshi

Naomba nisaidie bei za kukodia mashamba na shamba nahitaji kulima vitunguu na nyanya.
 
Dah kuna jirani yangu kapanda kilo tatu za red creole, hazijaota , sijui ndio utapeli wenyewe
Huwa inatokea. Niliwahi kununua kilo 3 pia za red creole. ( Moja kwenye lipo, mbili zilikuwa kwenye packet)
Iliota moja tu iliyokuwa kwenye kopo.
Nilifuatilia inaoneka Kati ya Mambo mawili:-
1. Eidha zilie zilizokiwa kwenye packets muda wake Ulikwisha (zili expair)
2. Eidha packet zilitobolewa na wadudu na kusababisha hewa iliyokuwa ikizihifadhi kutoka na baada ya muda mbegu kuharibika.

Unaponunua mbegu jiridhisha Kwa hayo. Nashauri nanua za kopo.

Sasa natumia za kopo hazisumbui kuota. Na kama ni packets zisiwe za muda mrefu tangu ziwe packed.
 
mwenye uelewa anisaidie nimewatika mbegu zimeota lakini zimeanza kunyauka tatizo ni nini?
1. Maji inaweza kuwa tatizo, kama juankali Sana mwaga maji kutwa mara mbili Kila siku.
2. Hujasema mbegu zina muda gani. Ila unaushauriwa wiki moja au mbili baada ya mbegu kuota uulizie dawa za fungus (ukungu)
Ukungu ugonjwa mbaya Sana na ndio unaathiri Sana mimea mingi. Pulizia dawa za ukungu, booster. Na siku 14 baada ya kuota weka mbolea.
 
Mkuu unahitaji Nini sasa, bado hujafafanua. Mi Niko na project hii kwa sasa, ukiamua unaweza kikubwa kuwa makini hasa Mbegu inapokuwa kitaluni hasahasa inapoanza kuota kabla haijapata jani la pili mana hapo inaweza kufa ovyoovyo so usipokuwa makini utaipoteza. Ila baada ya kuanzia wiki mbili hadi tatu kitaluni Mbegu uanza kusurvive fresh. Vitu vya msingi ni kumwagilia na kupiga dawa ya ukungu na sumu kwa ajili ya wadudu waharibifu mara tu Mbegu itakapoota
Nimeweka kitalu cha vitunguu tar 9/06/2020, nafanya majaribio kama vitastawi vizuri mwakani Mungu akipenda niingie rasmi. Nitakuwa naomba ushauri kutoka kwako kadiri itakapobidi, Natanguliza shukrani.
 
Nimeweka kitalu cha vitunguu tar 9/06/2020, nafanya majaribio kama vitastawi vizuri mwakani Mungu akipenda niingie rasmi. Nitakuwa naomba ushauri kutoka kwako kadiri itakapobidi, Natanguliza shukrani.
Nipo Tanga, kando kidogo kutoka Tanga mjini
 
Nimeweka kitalu cha vitunguu tar 9/06/2020, nafanya majaribio kama vitastawi vizuri mwakani Mungu akipenda niingie rasmi. Nitakuwa naomba ushauri kutoka kwako kadiri itakapobidi, Natanguliza shukrani.
Pamoja mkuu, your welcome!!
 
Mambo vipi wadau! Nahitaji kujua gharama za kilimo cha vitunguu kwa heka moja. Anaejua anielekeze tafadhali
 
Hapo awali kitungu kilikuwa ni zao lililokuwa linapatikana porini katika ukanda wa bahari ya Mediterania. Zao hili hulimwa katika nchi nyingi za magharibi, nchi za milima zilipo kaskazini mwa dunia, likwemo bara la Afrika. Vitunguu hustawi katika hali ya hewa ya jotoridi 13°C – 24°C, hali ya hewa inayofaa kwa kuotesha na kukuzia miche kwenye kitalu ni jotoridi 20°C – 25°C. Kwa kawaida vitunguu huhitaji kiasi cha joto nyuzi 20°C-25°C ili kuweza kustawi na kukua vizuri. Joto zaidi ya hapo hufanya vitunguu kudumaa na kutoweza kutengeneza viazi (bulbs).


Matumizi
Kitunguu hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha kwenye chakula, na pia hutumika kama dawa ya kansa ya tumbo, vidonda na majipu.

Ustawi
Zao la vitunguu hustawi katika udongo wa tifu tifu wenye mbolea ya kutosha, ukiwa na uchachu wa udongo (PH) kiasi cha 6 – 6.8. Udongo wa mfinyanzi haufai kwa zao la vitunguu kwa kuwa hauruhusu viazi vya vitunguu (bulbs) kutanuka. Hivyo uwezekano wa kupata mazao ni mdogo. Pia udongo wa kichanga haufai kwa zao la kitunguu kwa kuwa hauna mbolea na hivyo vitunguu huwa vidogo sana, jambo ambalo ni vigumu kupata mazao yanayofaa kwa soko.

Zao la kitunguu huhitaji unyevu muda wote wa ukuaji wake. Zao hili lina mizizi mifupi hivyo linahitaji kumwagiliwa maji mara kwa mara.




Aina za vitunguu

Kuna aina mbili za vitunguu ambazo zimezoeleka
:
  • Vitunguu vya asili kama vile Singida, na Rujewa (aina hii ina rangi ya kahawia iliyopauka).

  • Chotara: Hii ni aina ya vitunguu inayojulikana kama vitunguu vya kisasa. Katika kundi hili kuna vitunguu kama Texas grano, Red creole, Bombay red, White granex, na Super rex.
Mgawanyiko
Zao la vitunguu limegawanyika katika makundi mawili. Hii inatokana na uhitaji wa mwanga na ukuaji wake. Aina ya kwanza inahitaji mwanga kwa saa 8-13 ili kuweza kuchanua na kutoa mbegu.

Aina ya pili inahitaji mwanga kwa saa 13-15 kuweza kuchanua na kutoa mbegu.


Kupanda
Vitunguu hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo husiwa kwenye vitalu. Kitalu kinaweza kuwa na upana wa mita 1, urefu unategemeana na ukubwa wa eneo ulilo nalo.

Unaweza kupanda vitunguu kwenye matuta mbonyeo (Sunken bed). Aina hii ya upandaji hutumika kwenye eneo lenye shida ya maji. Upana wa tuta uwe mita moja.

Kupanda kwenye matuta mwinuko (Raised bed) upandaji wa iana hii hutu mika sehemu yenye maji mengi au yanayotuama.

Tahadhari: Maji yakituama kwenye vitunguu hufanya vitunguu kuoza, hivyo kuathiri mavuno.

Nafasi
Vitunguu vipandwe kwa nafasi ya sentimita 7.5 kutoka mche hadi mche, sentimita 12.5 kutoka mstari mmoja hadi mwingine kwenye matuta.



Mbole ya kupandia
Unaweza kutumia mboji, au samadi iliyo oza vizuri kupandia. Baada ya hapo unaweza kuongeza mboji baada ya miezi miwili. Endapo unafanya kilimo kisichozingatia misingi ya kilimo hai, unaweza kupanda kwa kutumia mbolea aina ya NPK (20:10:10) baada ya mwezi na nusu, unaweka mbolea ya Urea.

Palizi
Vitunguu ni zao lenye uwezo mdogo sana wa kushinda na magugu. Hivyo, inabidi shamba liwe safi muda wote wa ukuaji hadi kuvuna.



Uvunaji
Kwa kawaida, vitunguu huchukua muda wa miezi 5-6 tangu kupandwa hadi kuvunwa. Unaweza kuanza kuvuna vitunguu baada ya asilimia 75 ya shingo za vitunguu kuvunjika. Baada ya kuvuna, unaweza kuweka kwenye madaraja (grades) kwa kufuata ukubwa, rangi na unene wa shingo ya kitunguu. Vitunguu vyenye shingo nyembamba hudumu zaidi, vyenye shingo nene huoza haraka.

Ukataji
Hakikisha kuwa shingo ya kitunguu inabaki kiasi cha sentimita 2. Hii husaidia kuzuia kuoza haraka.

Namna ya kuhifadhi vitunguu
Baada ya kuvuna, hifadhi vitunguu kwenye kichanja chini ya kivuli na uvitandaze vizuri. Unaweza kuhifadhi vitunguu kwa kufunga kwenye mafungu na kuvitundika. Vitunguu vikihifadhiwa vizuri vinaweza kukaa hadi miezi minne bila kuharibika, hii hutegemeana na aina ya uhifadhi.

Wadudu wanaoshambulia vitunguu
Kuna aina nyingi za wadudu wanaoweza kushambulia vitunguu. Hawa wafuatao ni baadhi ya wadudu waliozoeleka kwenye zao la vitunguu.



Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe.

Madhara: Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia.



Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.

Minyoo fundo (Nematodes): Aina hii ya minyoo hushambulia mizizi ya vitunguu. Hali hii husababisha kudumaa kwa vitunguu kwa kuwa hushindwa kufyonza maji na chakula kutoka ardhini.

Vidomozi (Leaf minor): Hushambulia majani kwa kujipenyeza kwenye ngozi ya jani na kusababisha michoro ambayo huathiri utendaji wa majani.

Utitiri mwekundu (Red spider mites): Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani na kusababisha vitunguu kunyauka.

Funza wakatao miche: Funza hawa hutokana na wadudu wajulikanao kama Nondo, na hushambulia shina na kulikata kabisa.

Namna ya kukabiliana na wadudu hawa
Unaweza kukabiliana na wadudu hawa kwa kufanya kilimo cha mzunguko. Usioteshe vitunguu sehemu moja kwa muda mrefu, au kufuatanisha mazao jamii ya vitunguu kama vile leaks.

Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kutoka kwenye kampuni zinatambuliwa kisheria na kibiashara. Kupanda kwa wakati unaotakiwa; vitunguu visipandwe wakati wa kiangazi. Vipandwe wakati wa majira ya baridi na kuvunwa wakati wa joto. Tumia dawa za asili za kuulia wadudu, au dawa nyinginezo zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo.


Magonjwa yanayoshambulia vitunguu

1. Purple blotch: Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus). Ugonjwa huu husababisha mabaka ya zambarau na meusi katika majani ya vitunguu. Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu unyevu mwingi.
Madhara: Ugonjwa huu hupunguza mavuno mpaka asilimia hamsini (50%).

2. Stemphylium leaf blight: Hukausha majani kuanzia kwenye ncha hadio kwenye shina.; Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu na ukungu mwingi.
Madhara: Hupunguza mavuno hadi kwa asilimia sabini na tano (75%).

3. Magonjwa ya virusi (Onion yellow draft virus): Ugonjwa huu husababisha vitunguu kuwa na rangi iliyochanganyika, kijani na michirizi myeupe au njano. Vitunguu hudumaa kwa kiasi kikubwa;Ugonjwa huu husababishwa na kimamba.

Madhara: Huathiri mavuno kwa asilimia 80 mpaka asilimia 100%.

4. Kuoza kwa kiazi (Bulb rot): Husababishwa na fangasi. Ugonjwa huu hutokea vitunguu vikishakomaa, huku udongo ukiwa na maji maji. Vitunguu vikishakomaa visimwagiliwe tena.

Uharibifu wa vitunguu usiotokana na magonjwa
1. Kuchipua baada ya kuvunwa: Hali hii hutokea endapo vitunguu vitavunwa kabla ya muda wake. Endapo vitunguu havitakaushwa vizuri baada ya kuvunwa. Hali hii husababisha uharibifu mpaka asilimia themanini (80%). Sehemu ya kukaushia vitunguu iwe na hewa inayozunguka na mwanga wa kutosha. Vitunguu vikiwekwa gizani huchipua kwa urahisi.

2. Muozo laini (Soft rot): Ugonjwa huu hushambulia vitunguu baada ya kukomaa; husababishwa na vimelea (bacteria). Vitunguu hutoa harufu mbaya ya uozo. Kuepuka hilo vuna kwa wakati unaofaa, hifadhi sehemu yenye mwanga na hewa inayozunguka.



Virusi
Unaweza kuzuia vimamba ambao ndio wanaoeneza virusi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu.

Vitunguu vinalipa
“Vitunguu vinatofauti kidogo na mazao mengine ya mboga mboga kwa kuwa si rahisi kukosa soko, na endapo bei si nzuri unaweza kuhifadhi kwa muda ili kusubiri bei iwe nzuri.” Ni maneno ya mkulima Peniel Rodrick (pichani) ambaye amejikita zaidi katika kilimo cha vitunguu kibiashara.

Mkulima huyu kutoka kijiji cha Oloigeruno anasema pamoja na kwamba anazalisha pia mazao mengine, lakini ameamua kujikita zaidi kwenye vitunguu baada ya kugundua siri na namna ya kupata faida zaidi.

Toka aanze kilimo cha vitunguu miaka 12 iliyopita, ameweza kuendesha maisha yake vizuri, ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mingine kama ufugaji wa ng’ombe, kujenga nyumba ya kisasa na kuitunza familia yake ya watoto watatu ipasavyo. Pamoja na hayo anasema tatizo kubwa la vitunguu ni magonjwa na wadudu. Anasema si rahisi sana kugundua mara moja kuwa kuna ugonjwa unaoshambulia vitunguu, na mara unapogundua unakuwa umefikia kwenye hali mbaya.
 
KILIMO BORA CHA VITUNGUU SAUMU

UTANGULIZI
Vitunguu saumu ni jamii ya vitunguu maji asili yake ni nchi za Asia lakin pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.

hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

AINA YA VITUNGUU SAUMU
Kitaalam bado aijafahamika kunaaina ngapi za vitunguu saumu lakini kuna aina mbili ambazo zinalimwa hapa nchini ni Kienyeji na kisasa.
Aina ya kisasa uzaa vitunguu vikubwa venye ngozi nyeupe napia aina ya kienyeji uzaa vitunguu vyekundu vyenye harufu kali sana na pia havia haribiki mapema ukilinganisha na vya kisasa vitunguu saumu havizai mbegu halisi kwa hyo uzalishwa kwa kutumia vikonyo vyake



TABIA YA MMEA

Tunguu la vitunguu saumu utokana na vikonyo na hiv vikonyo ndo vinatumika kama mbegu

HALI YA HEWA
Vitunguu saumu ulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.

KUANDAA SHAMBA
Andaa shamba mapema lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia unaweza kutuengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda au wakati wa kupanda pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta

KUPANDA
Panda vikonyo vilivo anza kuchipua vilivo safi na visivyo na dalili ya ugonjwa kwa nafasi ya sm 5 kikonyo hadi kikonyo na sm 15 mstari hadi mstari.

PALIZI NA MATUMIZI YA MBOLEA
Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua na baada ya palizi ya kwanza weka mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi unaweza kupulizia dawa ya kuua magugu endapo vitunguu vimeshaota kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi.

MAGONJWA
  • fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna
  • kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia
  • kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko na hakikisha store ni safi
  • baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao
  • muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa
WADUDU
Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

KUVUNA
Vitunguu uvunwa vikifika miezi 6-7 baada ya kupanda majani na mashina unyesha dalii ya kukauka viache vitunguu shambani mpaka majani yanap kauka kabisa ngoa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom