Wadau habari za mjengoni naomba niulize wataalamu wa vitunguu saumu.. kwa kanda ya pwani vinakubali kulimwa mm nipo zanzibar naomba ushauri au maelekezo kwa anaejua anisaidie tafadhali.
Ahsante
 
Habari wanaJF naitwa Pierre ni mkulima wa kitunguu swaumu pia ni suplier kwa mikoa ya dar morogoro pia na zanzbar kama kuna mtu anauhitaji wa kitunguu swaumu na anauhakika na soko kwenye maeneo yake kwa kiasi chakuanzia gunia moja na kuendelea tuwasiliane kupitia namba 0785092386,0758176570,0620630514,kitunguu kinalipa ulioko mkoa wowote kinafikika ukishakua na uhakika wa soko ntafute tufanye biasharaView attachment 1251709
IMG_20191027_112628_5.jpeg
IMG_20190728_100223_3.jpeg
 

Attachments

  • FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    64.2 KB · Views: 27
  • FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    64.2 KB · Views: 26
  • FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    64.2 KB · Views: 25
  • FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    64.2 KB · Views: 18
  • FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    64.2 KB · Views: 19
  • FB_IMG_1571760278470~2_1572680738095.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2_1572680738095.jpeg
    51 KB · Views: 20
Nawasalimu kwa pamoja ndugu zangu
Mm nimejiunga huku kwa nia ya kujifunza kwa namna ya kipekee sana mmenipokea na kunionyesha ushirikiano hasa pale nilipohitaji msaada wa mawazo .
Asanteni sana kwa hilo
Pili
Nilisema awali ndoto yangu ni kilimo japo wachache walinidhihaki ila hazima yangu ipo palepale,
Kwa jasho na kujinyima nimefanikiwa kupata shamba Hekari 15 maeneo ya chalinze barabara ya kwa mwarabu
Nb
Nilinunua kupitia utaratibu ambao ni muongozo niliupata hapa jf.
Ombi langu tena,
Nnielekeze naweza kulima zao gani maeneo hayo?
WAZO LANGU
Kulima maharage ya soya
Kulima mahindi
Kulima nanasi
au zao lingine mtakalolipendekeza.
Ukweli nina nia na hili swala



Natanguliza shukran
Ni mategemeo yangu mtanishauri vema
 
Upo mkoa gan kaka.
Habari wanaJF naitwa Pierre ni mkulima wa kitunguu swaumu pia ni suplier kwa mikoa ya dar morogoro pia na zanzbar kama kuna mtu anauhitaji wa kitunguu swaumu na anauhakika na soko kwenye maeneo yake kwa kiasi chakuanzia gunia moja na kuendelea tuwasiliane kupitia namba 0785092386,0758176570,0620630514,kitunguu kinalipa ulioko mkoa wowote kinafikika ukishakua na uhakika wa soko ntafute tufanye biasharaView attachment 1251709View attachment 1251713View attachment 1251718

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau nahitaji kufahamu kuhusu kilimo cha vitunguu kuanzia mbegu, mbolea madawa umwagiliaji nk. nitashukuru kwa anaefahamu akanisaidia kunipa maarifa ya kilimo hiki.
 
Habari wana JF,

Kama mada ilivyo hapo juu, Mwaka huu 2020 nimejipanga nijikite katika kilimo cha umwagiliaji wa kilimo cha vitunguu mwezi wa sita mwishoni naanza kazi, MUNGU ajalie uhai tu, nimejipanga kulima heka moja.

Naombeni wataalam mje na uzoefu mliona hapa.

KARIBUNI SANA.
 
Nakutia moyo mkuu lakini kilimo si rahisi km wengi wanavyozani. Lazma ugangamale kweli kweli kitunguu kinahitaji close up management and care. La sivyo kinaweza kukata hadi mtaji. Kila raheri lakni
 
garlic-as-a-remedy-for-male-yeast-infection.jpg


UTANGULIZI

Vitunguu saumu ni zao ambalo lipo katika jamii ya vitunguu na hufanana sana na vitunguu maji, zao hili linatumika sana duniani kama kiungo cha chakula na wengine hutumia kama dawa.

ASILI YAKE

Vitunguu swaumu asili yake ni maeneo ya Mediterranean na China, Asia lakini pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.

hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

AINA ZA VITUNGUU SWAUMU

Vitunguu swaumu vipo vya aina mbalimbali nazo ni:=

i) Antichoke – Hii kwa mbali inaonekana kama ni nyekundu lakini sio iliyokolea

ii) Soft neck – Kwa rangi ni nyeupe inatumika sana kwasababu hachukua mda mfupi shambani

iii) Silver skin – Hivi vina rangi nzuri ya silver na mara nyingi hutumiwa na wasindikaji maana vinadumu mda mrefu bila kuharibika.

HALI YA HEWA & UDONGO

Vitunguu saumu hulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA

Shamba linapaswa kutayarishwa mapema kabisa, lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia unaweza kutengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda.

UTAYALISHAJI WA MBEGU

Mbegu ya kitunguu swaumu ni ile punje (vikonyo) inayokuwa imebanguliwa kutoka kwenye kitunguu au tunguu iliyokomaa kabisa, kiasi cha kilo 300 – 500 hutumika kwa hekari moja na inatakiwa uchague mbegu isio na magonjwa au isio dhaifu.

UPANDAJI

Tabia ya mmea wa Vitunguu swaumu humea huanza kuota kipindi cha baridi ( miezi yenye baridi), kwa Tanzania kipindi ambacho hakuna joto ni miezi ya May mpaka August, Unachukua kitunguu swaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 5 na kati ya mistari ni sentimeta 20 na kushuka chini kiwe na wastani wa inchi 2.5 .
Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kung’olewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu swaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu. Pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta.

MBOLEA

Mbolea huwekwa baada ya palizi, tumia mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi.

UPALILIAJI

Kuwa na juhudi ya kupalilia ili kuipa uhuru mimea kumea vizuri na kulifanya shamba lako kuwa safi, Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua na baada ya palizi ya kwanza ndipo weka mbolea.

Unaweza kupulizia dawa ya kuua magugu endapo vitunguu vimeshaota kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi. Mmea unapoendelea kukua na kutoa maua yaache majani yarefuke mpaka yajikunje, ndipo utayakata ili kuongeza uzalishaji.

MAGONJWA & WADUDU
MAGONJWA


Vitunguu swaumu havishambuliwi sana na magonjo, ila magongwa yake ni kama:=

i) Fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna

ii) Kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia

iii) Kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko na hakikisha store ni safi

iv) Baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao

v) Muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa.

WADUDU

Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

UVUNAJI

Baada ya miezi 6-7 tokea kupanda ndio mda muafaka wa kuvuna vitunguu swaumu kwani vinakuwa vimekomaa na majani na mashina huonesha dalili ya kukauka, ndipo viache vitunguu shambani mpaka majani yanape kukauka kabisa ng’oa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu. Kiasi cha tani 4 – 7 zinaweza kuvunwa katika heka moja.

SOKO

Soko lipo kwasababu Vitunguu Swaumu ni kiungo kinacho tumika na wengi, kwa bei ya shiling 3,000 – 3800 kwa kilo.
Kwa mtuu yoyote ambaye yuko dar anafanya biashara ya vitunguu swaumu au ambaye ni dalali naomba anicheki kwa namba 0627477368 Nina mzgo wangu wa vituunguu swaumu nautoaa shambani tufanye kaz pamoja
 
Mkuu unahitaji Nini sasa, bado hujafafanua. Mi Niko na project hii kwa sasa, ukiamua unaweza kikubwa kuwa makini hasa Mbegu inapokuwa kitaluni hasahasa inapoanza kuota kabla haijapata jani la pili mana hapo inaweza kufa ovyoovyo so usipokuwa makini utaipoteza.

Ila baada ya kuanzia wiki mbili hadi tatu kitaluni Mbegu uanza kusurvive fresh. Vitu vya msingi ni kumwagilia na kupiga dawa ya ukungu na sumu kwa ajili ya wadudu waharibifu mara tu Mbegu itakapoota
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom